Tafuta

2023.05.29 Sr Veronica, Monsinyo Luiz, Dk Ruffini na Sr  Nathalie wakati wa uwakilishi wa hati yaKuelekea Uwepo Kamili. Tafakari ya Kichungaji juu ya Ushirikiano na Mitandao ya Kijamii”(#FullyPresent), 2023.05.29 Sr Veronica, Monsinyo Luiz, Dk Ruffini na Sr Nathalie wakati wa uwakilishi wa hati yaKuelekea Uwepo Kamili. Tafakari ya Kichungaji juu ya Ushirikiano na Mitandao ya Kijamii”(#FullyPresent),  

Dk.Ruffini:Mitandao ya kijamii ina uwezo wa kujenga ulimwengu bora!

Mitandao ya kijamii ni njia ya Kanisa ya kuwa miongoni mwa watu na kufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wote na sio kuhatarisha ukweli ili kupata wafuasi au kupendw.Alisema hayo Dk. Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano wakati wa kuzungumza na Vatican News,mara baada ya kuwasilisha tafakari mpya ya kitaalimungu na kichungaji ya kwenye mitandao ya kijamii.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini, alisema kuwa mitandao ya kijamii ni muhimu kwa uwepo katika ulimwengu wa kisasa unaoendelea kukua kwa kasi. Alisisitiza hayo katika mahojiano na Vatican News,  huku akisisitiza kwamba si kwa ajili ya kupata wafuasi wengi  au kupendwa, bali ni kufanya kazi katika kuelekea ulimwengu bora. Mkuuwa Baraza la Mawasiliano alisema katika muktadha wa  baada ya uwasilishaji wa Hati iliyopewa jina: “Kuelekea Uwepo Kamili. Tafakari ya Kichungaji juu ya Ushirikiano na Mitandao ya Kijamii”(#FullyPresent), iliyochapishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, siku ya Jumatatu tarehe 29 Mei na kuwakilishwa  katika Ofisi ya Waandishi wa  vyombo vya Habari Vatican.

Kauli mbiu: Kuelekea Uwepo Kamili

Lengo la Hati hiyo ni kukuza tafakari ya pamoja juu ya ushiriki wa Wakristo katika mitandao ya kijamii, ambayo imezidi kuwa sehemu ya maisha ya watu. Ikiongozwa na mfano wa Msamaria Mwema, hati hiyo inatoa fursa ya kuanza tafakari ya pamoja kuhusu jinsi ya kukuza utamaduni wa kuwa majirani wenye upendo katika ulimwengu wa kidijitali pia. Alipoulizwa juu ya hitaji la hati kama hiyo na umuhimu wake, Dk. Ruffini alikumbuka kwamba, tangu mwanzo wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano , waliona hitaji la kufanya tafakari na hati juu ya mada hiyo, hasa kwa sababu  teknolojia imekuwa ikibadilika kwa  haraka. Kilichotafutwa, alisema, kilikuwa ni “tafakari kuanzia Injili, kwa mtazamo wa kitaalimungu na wa kichungaji juu ya jinsi ya kukabiliana na teknolojia inayobadilika.”

Kutopotosha ukweli halisi

Mitandao ya kijamii ambayo tunapaswa kuwepo ndani mwake, kwa mujibu wa Dr Ruffini, alibainisha kuwa “haipaswi kuchochea matamshi ya chuki, habari za uwongo, na kugushi, bali kumwilisha ukweli, upendo na huruma.” Jambo muhimu zaidi, alisema: “ni kufahamu kiasi kwamba tunaweza pia kusema katika historia ya wanadamu, kuwa daima kuna uovu. Na kwa sisi waamini, kuna shetani ambaye anafanya kazi kila wakati kwa njia ambayo historia inakua.” D Ruffini vile vile  alibainisha kwamba  kuwa teknolojia si kitu ambacho kinapaswa kutuvumbua,  badala yake, ni lazima tujadili sheria na kanuni za kushiriki na kufanya kazi kwa ajili ya  manufaa ya wote, ambapo “alitoa onyo kuwa, mara nyingi tunasahau”. “Tunajua kwamba labda habari za uwongo zitakuwa na wafuasi wengi kuliko ukweli, lakini je, hii ndiyo njia tutakayoendeleza ili ulimwengu uwe bora?  Ni swali lake, na kujibu kwamba: “Sidhani hivyo na kwa maana yoyote, sidhani hivyo.”

Sr. Becquart Lazima kuwa na njia na utambuzi unaoendelea

Vatican News pia ilimhoji Sr.  Nathalie Becquart, Katibu Msaidizi wa Sinodi ya Maaskofu  ambaye alijadili juu ya mbinu sahihi ya majukwaa ya kijamii. Kwa mujibu wake alisema ni upambanuzi unaoendelea, na ndio maana ninataka sana kumulika kwamba waraka huu unatokana na majadiliano ya  sinodi inayohusisha watu wengi kwa sababu hakuna mtu peke yake mwenye suluhisho la kimazingaombwe, la kuwa na uwepo mzuri kwenye mitandao ya kijamii halafu muktadha ukawa ni tofauti. Na kwa hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kwamba waraka huu uwasaidie watu kufanya utambuzi wao wenyewe, hasa na wengine kama Wakristo katika jumuiya yao wenyewe, kutafuta na kutambua njia na utambuzi unaoendelea.” Kwa njia hiyo Sr Natalie alibainisha kuwa “kazi hii ni yetu, kama Kanisa linalotoka nje, ili kufikia kila mtu, katika pembe zilizopo. Tunahitaji kwenda, tunahitaji kutoka nje.”

Monsinyo Ruiz: Kuwasiliana na kucgania uinjilishaji mpya

Kwa upande wake  Monsinyo Lucio Ruiz, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano  alisema ni utamaduni, siku hizi, na palipo na mwanadamu, pale, Kanisa linahitaji kuwepo. Kwa hiyo tafakari ya kazi hiyo, alimulika jinsi tunavyoweza kujifunza kutoka kwa wamisionari, ambao, kabla ya kazi yao kubwa sana, walijifunza 'lugha' ili kuwasiliana na kuchangia uinjilishaji mpya. Baba Mtakatifu Francisko, alisema, anatoa mchango mkubwa zaidi kwa tafakari za watangulizi wake, ili kuzoea wakati wa sasa, kwa njia ambayo inafaa zaidi na yenye athari kwa nyakati, kukumbatia vyombo, ipasavyo, kwa kipimo chake. Kwa maana hiyo alipendekeza kuwa majukwaa ya kijamii ni muhimu, na yanahusu kuimarisha kile ambacho ni halisi. Kanisa linahitaji kwenda chini kwenye ‘shamba,’ jambo ambalo Yesu alituambia tufanye, akibainisha kuwa haiwezekani kuwapo.

Licha ya uwepo wa Teknolojia hautaondoa huhalisia wa mkumbatio na uwepo 

Sr. Veronica Donatello, S.F.A., mkuu wa Huduma ya Kitaifa ya Huduma ya Kichungaji ya Watu Wenye Ulemavu ya Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) na mshauri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, anayetambuliwa mara nyingi kwa kutoa huduma ya lugha ya ishara wakati wa matukio ya Kipapa, wakati wa mkutano huo  kwa  waandishi wa Habari yeye alisema jinsi mitandao ya kijamii inaweza kuwa zana muhimu kwa watu wenye ulemavu. Alibainisha jinsi ambavyo mara nyingi inavyowawezesha kuhisi hali kubwa ya kuwepo. Lakini hata hivyo, Sr Veronica alionya kwamba licha ya thamani kubwa ya nyenzo hizo za kiteknolojia, lakini hazitaweza kamwe kuchukua nafafi ya  mambo halisi, kama vile kuwepo au kukumbatia mtu moja kwa moja.

Dk Ruffini kuhusu hati mpya iliyochapishwa 29 Mei
01 June 2023, 16:04