2023.06.09 maandalizi kabambe ya tukio la 'Not Alone' litakalofanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.Wote mnaalikwa! 2023.06.09 maandalizi kabambe ya tukio la 'Not Alone' litakalofanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.Wote mnaalikwa! 

Usikose katika 'Not Alone'kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro,10 Juni 2023

'Not Alone' ni tukio litakalofanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican,Jumamosi tarehe 10 Juni 2023 kwa kuwaleta watu wa mataifa yote duniani ambapo kutakuwa na kukumbatiana kati ya vijana wawili wa Ukraine na Urussi kwa lengo la kuonesha kuwa wote ni ndugu.Tamko litatiwa saini.Nyote mnaalikwa!

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Yamebaki masaa machache kabla ya  tukio lililoandaliwa hivi karibuni kufanyika la Mkutano wa Kimataifa juu ya 'Udugu wa Kibinadamu’ ambapo kwa mujibu wa Msemaji wa Mfuko wa Fratelli tutti, ametoa taarifa kuhusiana tukio hili hasa katika muktadha mweingine wa vita barani Ulaya na kwingneko kwamba: “Vijana wawili wa Kiukraine na Mrussi, watapeana mikono ili kuelezea shauku yao ya amani ya wanadamu wote”. Amebainisha hayo Kadinali Mauro Gambetti, Mkuu wa Kanisa la Mtakatifu Petro na rais wa Mfuko wa  Fratelli tutti ambao uliandaa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Udugu wa Kibinadamu.  Tukio hilo kwa hiyo litafanyika Jumamosi tarehe 10 Juni 2023,  saa kumi jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Tukio hilo, kwa mapenzi ya Papa, litazindua  kwa upya ndoto yake ya Udugu na  pia itakuwa fursa ya kumuombea  na kuwa karibu na Baba Mtakatifu Francisko ambaye amelazwa Hospitalini Gemelli.

Maandalizi mazuri ya tukio la tarehe 10 Juni kuhusu Udugu wa kibinadamu
Maandalizi mazuri ya tukio la tarehe 10 Juni kuhusu Udugu wa kibinadamu

Takriban washindi 30 wa Tuzo ya Nobel watashiriki, katika Tukio la ‘Not Alone’ ambapo Carlo Conti wa Televisheni ya Italia atawasilisha mashuhuda  wa udugu na wasanii mbali mbali kama vile: Andrea Bocelli, Al Bano, Amara Roberto Bolle, Giovanni Caccamo, Cristicchi, Hauser, Carly Paoli,  Kwanya ya  watoto ya Antony, Mr. Rain, Amii Stewart na Paolo Vallesi, watakuwapo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Viwanja vingine 8 duniani vitakavyounganishwa moja kwa moja mbashara

Kwa mujibu wa taarifa na ambazo zilikuwa tayari zimeelezwa zinathibitisha kuwa Viwanja 8 duniani vitaunganishwa kuanzia na: Brazzaville(Congo), Trapani (Mediterania Kuokoa Binadamu); Bangui (Jamhuri ya Afrika ya Kati); Ethiopia; Buenos Aires (Argentina); Yerusalemu(Israeli); Nagasaki(Japani); Lima(Peru).

Usikose katika tukio la Udugu wa Kibindamu Jumamosi 10 Juni 2023 katika Uwanja wa Mtakatifu Petro

Wavulana na wasichana kutoka duniani kote wataungaisha mikono kwa kutengeneza mduara mkubwa karibu kukumbatia mzunguko wa nguzo ya Bernini za Uwanja wa Mtakatifu Petro, kama ishara madhubuti ya udugu. Ishara hiyo ilipendekezwa na mwanahisani kutoka Argentina Alejandro Roemmers. Kutakuwa na familia na vyama na wale ambao leo hii wanaishi pembezoni mwa jamii, kutoka kwa maskini zaidi na wasio na makazi hadi wahamiaji na waathirika wa vurugu na biashara mbaya ya binadamu.

Tendo la udugu

Tamko la udugu basi litatiwa saini ili kusisitiza kwa ulimwengu lisemalo “hakuna kufanya vita ya Kanisa na kuwa na juhudi ya mazungumzo na ujenzi wa amani.” Chama cha Coldiretti kitatoa chakula kutoka mashambani mwao kama ishara ya kushiriki na udugu. Kila mtu atapewa bonge la udongo na mbegu ya kufanya mmea wa udugu ukue.

Wahisani wanaandaa Tukio hilo la Not Alone
Wahisani wanaandaa Tukio hilo la Not Alone

Tukio mchana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro litaanza saa 10.00 na linafunguliwa kwa watu wote bila kijiandolosja , na kuanza kuinga katika uwanja kuanzia saa 8.00. Kwa maelezo zaidi  ya ratiba unaweza kubonyeza kwenye ukuraza wa mfuko wa Fratelli Tutti: www.fondazionefratellitutti.org/notalone.

Jumamosi 10 Juni 2023 ni kivumbi na jasho cha udugu wa kibinadamu katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Jumamosi 10 Juni 2023 ni kivumbi na jasho cha udugu wa kibinadamu katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Mkutano huo hata hivyo utakuwa mbashara kupitia Televisheni ya Vatican CTV Vyombo vya habari Vatican, mondo visione ya  Televisheni ya Italia (RAI1) kuanzia Jioni saa 11.00  - 12:45 na utitirishaji kwenye mtandao wa Fondazionefratellitutti.org na majukwaa yote ya Facebook na  YouTube ya Mfuko wa Fratelli tutti.

Tukio la Note Alone katika uwanja wa Mtakatifu Petro 10 Juni 2023
09 June 2023, 15:49