Ziara fupi ya Papa huko Gemelli kwa uchunguzi wa kimatibabu
Vatican News
Baba Mtakatifu alirudi Hospatalini Gemelli Roma, lakini kwa wakati huu, ukilinganishwa na zaidi ya miezi miwili iliyopita, ilikuwa ni kwa ajili ya uchunguzi wa haraka wa kimatibabu. Haya yaliwasilishwa na Msemaji wa Vyombo vya habari katika Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican, Dk. Matteo Bruni, wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari na kuripoti kwamba asubuhi tarehe 6 Juni 2023 Baba Mtakatifu Francisko alikwenda Hosptalini Gemelli kwa ajili ya vipimo vya kliniki na akarudi Vatican kabla ya saa sita mchana.
Machi iliyopita Papa alilazwa hospitalini huko Gemelli
Ikumbukwe mnamo tarehe 29 Machi, iliyopita Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amelazwa hospitali hiyo hiyo ya Gemelli Roma kwa sababu ya ugonjwa wa bronchitis ya kuambukiza na aliruhusiwa baada ya siku tatu, mnamo tarehe Mosi Aprili 2023.