.023.07.15 Kuwekwa wakfu wa kiaskofu kwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia na Malawi Askofu Mkuu Gian Luca Perici. .023.07.15 Kuwekwa wakfu wa kiaskofu kwa Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia na Malawi Askofu Mkuu Gian Luca Perici.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Kard Parolin:askofu hutoa maisha yake kwa ajili ya kundi lake na hawakimbii mbwa mwitu

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Katibu wa Vatican alimweka wakfu wa kiaskofu kwa Askofu Mkuu G.L Perici,aliyeteuliwa mwezi uliopita na Papa kuwa Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi:kazi ya askofu ni kuwa mlinzi ambaye anatunza uhai wa umoja na matumaini kati ya watu waliokabidhiwa kwake

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Askofu anaitwa kufanya nini? Ni Swali  muhimu lililoulizwa wakati wa mahubiri ya Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican katika Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumamosi tarehe 15 Julai 2023, kwa ajili ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu kwa Askofu Mkuu Gian Luca Perici, aliyeteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Francisko mnamo tarehe 5 Juni 2023 kuwa Balozi wa Kitume wa Vatican  katika nchi mbili Zambia na Malawi, barani Afrika. Kwa upande wake Kardinali Parolin alisema kuwa Askofu, anaitwa hasa kuleta habari njema kwa maskini, na kufunga majeraha ya mioyo iliyovunjika. Askofu ni ishara ya Kristo. Na wakati huo huo, alikumbusha hata kile ambacho Papa Francisko alisema wakati wa ziara yake ya kitume nchini Canada kwamba: “Kwa hakika kwa sababu sisi ni ishara ya Kristo, mtume Petro anatuhimiza kuwa lichunge kundi, liongoze, usiiruhusu lipotee unapoendelea na shughuli zako. Litunze kwa kujitolea na kwa upole”. Kwa maana hiyo Kardinali Parolin alisisitiza kuwa "Askofu ni kama mlinzi mzuri ambaye, akichunguza  kwa upeo,  huonya jamii juu ya hatari yoyote inayokaribia".

Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Vatican.
Misa ya kuwekwa wakfu wa kiaskofu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Vatican.

Mlinzi mzuri ambaye anaonesha kusikiliza Neno la Mungu, sala, kuhudhuria sakramenti mara kwa mara, unyenyekevu na mapendo ni silaha zenye nguvu za kushinda kila kikwazo na kudumisha mshikamano wa kidugu na matumaini hai.” Kufundisha kwa mamlaka na bila ubabe, kutawala kwa uthabiti na upole wakati huo huo, kugawa mkate wa uzima na kila ufanisi wa sakramenti, Askofu anaona ndani ya Kristo kielelezo bora na cha hali ya juu sana ambacho angeweza, hapo mwanzoni, hata kuwa na waoga fulani ndani yake wa kugandamana. Na inaweza kweli kuwa hivyo ikiwa makabiliano ya ajabu ya tendo la nguvu na la upole la Roho Mtakatifu ambaye huweka wakfu na kutia nguvu, ambaye hufariji na kuimarisha  kwa maombi haukuchukuliwi na kuwekwa tumaini na thabiti kwa yeye aliyeitwa kuwa askofu na wa Kanisa zima.”

Kardinali Parolin alitoa daraja la wakfu wa kiaskofu
Kardinali Parolin alitoa daraja la wakfu wa kiaskofu

Kwa hiyo Askofu, anaitwa kuelekeza macho yake kwenye moyo wa Yesu unaong'aa kwa upendo usio na kikomo kwa Mchungaji Mwema, aliye tayari kutoa uhai kwa ajili ya kondoo na kutokimbia mbele ya mbwa-mwitu. Askofu, anahimizwa kuzingatia moyo huo unaong'aa na kuangazia upendo kwa chanzo cha huruma hiki kisichokataa mtu yeyote na kinampa kila mtu tangazo la furaha la ukombozi wa kweli. Mwaliko ambao askofu anapaswa kuukubali ni kugeuza kabisa kila mapenzi ya moyo na kuyahamishia kwa Mungu. Yeyote anayemtazama Bwana Msulubiwa kwa mujibu wa  Kardinali Parolin akikumbuka maneno ya Mtakatifu Bonaventura ambayo Kanisa lilikuwa linakumbuka tarehe 15 Julai, huadhimisha Pasaka pamoja naye. Askofu, aidha  anaitwa kuonesha utamu wa nira ya Kristo ili kuondoa nira ya kusikitisha ya dhambi kutoka katika  mabega ya watu waliokabidhiwa kwake.

Furaha ya Askofu Mkuu Perici, Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia na Malawi.
Furaha ya Askofu Mkuu Perici, Balozi mpya wa Vatican nchini Zambia na Malawi.

Hatimaye  Kardinali Pietro Parolin alikumbuka kazi muhimu aliyokabidhiwa Askofu Mkuu  Perici kama Balozi wa Vatican hasa ile ya kupata neno la Papa  na kufikiasha katika Makanisa na serikali za mataifa alikotumwa. Lakini pia kuwa mleta amani asiyechoka katika ulimwengu huu unaoteswa na vita na migogoro ya umwagaji damu na kuhamasisha  utetezi wa haki za kimsingi za hadhi na utu ambazo mara nyingi zinatishiwa na itikadi zinazowanyonya na kuwadanganya kwa jina la ubinadamu ambao, kiukweli, haina tena kitu chochote cha kibinadamu kinachoihusu.

Kardinali Parolini akimbariki Askofu Mkuu mpya na Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi
Kardinali Parolini akimbariki Askofu Mkuu mpya na Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi

Na pia yeye kuwa daraja halisi lenye uwezo wa kuwasilisha mahitaji, matatizo, matumaini na hofu za Makanisa mahalia yaani binafsi kwa Kanisa la Ulimwengu,na kuwafanya watambue maombi ya kibaba ya mrithi wa Mtume Petro. Ikumbukwe, Askofu Mkuu Perici aliingia katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican mnamo  tarehe 1 Julai 2001 na kufanya kazi katika Ofisi za Ubalozi wa Vatican nchini  Mexico, Haiti, Malta, Angola, Brazil, Sweden, Hispania na Ureno.

Wakfu wa kiaskofu kwa Balozi wa Vatican nchini Zambia na Malawi
16 July 2023, 16:14