Tafuta

Kardinali Zuppi,Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia ametumwa tena na Papa kwenda huko Washington,Marekani. Kardinali Zuppi,Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia ametumwa tena na Papa kwenda huko Washington,Marekani.  

Kard.Zuppi anakwenda mjini Washington,kuendeleza utume wa amani nchini Ukraine

Rais wa CEI aliyetumwa na Papa,atakuwa katika mji mkuu wa Washongton kuanzia 17 hadi 19 Julai 2023.Vatican inasema:"Madhumuni ya ziara hiyo ni kubadilishana mawazo na maoni juu ya hali mbaya ya sasa na kuunga mkono mipango ya kibinadamu ili kupunguza mateso ya watu dhaifu zaidi hasa watoto.”

Na Salvatore Cernuzio & Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican imetoa taarifa kuwa “kuanzia tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, Kardinali Matteo Maria Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia,(CEI) akifuatana na Afisa wa Sekretarieti ya Vatican, anasafiri kwenda Washington  Marekani kama Mjumbe wa Baba Mtakatifu Francisko. Ziara hiyo inafanyika katika muktadha wa ujumbe wa kuhamasisha amani nchini Ukraine na inalenga kubadilishana mawazo na maoni kuhusu hali mbaya ya sasa na kuunga mkono mipango ya kibinadamu ili kupunguza mateso ya watu walioathirika zaidi na udhaifu zaidi, hasa watoto.”

Kardinali Zuppi wakati yuko Ukraine
Kardinali Zuppi wakati yuko Ukraine

Katika mukutadha huo ni  wazi kuwa Utume wa Kardinali  Zuppi kama mwakilishi wa Papa wa kupunguza mivutano haujaisha huko Kyiv, Ukraine  na Moscow, Urussi bali unaendelea  hadi Washington tangu Jumatatu  17 hadi Jumatano tarehe 19 Julai kwa ajili ya utashi wa Baba Mtakatifu anayetaka “kupunguza mzozo katika nchi ya Ulaya Mashariki inayoteswa. Katika utume wa kwanza wa Kardinali Zuppi alikwenda Kyiv mnamo tarehe  5 na 6 Juni 2023  na jijini Moscow mnamo  tarehe 28 na 29 Juni.  Wakati mnamo mwezi Mei, hata hivyo Vatican ilikuwa imewasilisha habari za utume huo wa rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Italia (CEI) aliyekabidhiwa na Papa Francisko  ambaye  tayari alikuwa ametaja Papa Francisko mwenyewe kwenye ndege ya kurudi kutoka  Ziara ya Kitume nchini Hungaria.

Kardinali Zuppi alikutana na kuzungumza na Rais wa Ukraine
Kardinali Zuppi alikutana na kuzungumza na Rais wa Ukraine

Kadhalika huo ni ujumbe ambao, kama Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin alielezea baadaye, kuwa haukuwa na madhumuni ya upatanisho wa  haraka, lakini lengo lake  ni kujaribu zaidi ya yote kupendelea hali ya mazingira ambayo yanaweza kuleta njia za amani”. Kardinali Parolin, pia akihojiwa na waandishi wa habari kando ya tukio moja jijini Roma kuhusu  uwezekano kwamba mpango wa Vatican ulifikiria maingiliano mengine pamoja na Urussi na Ukraine, kama vile Marekani (USA) na China, alikuwa amesema kwamba “kutokana na mazungumzo hayo yaliyotarajiwa na Papa hawakutaka kumtenga mtu yeyote.”

Kardinali Zuppi akiwa Ukraine alizungumza na viongozi wake
Kardinali Zuppi akiwa Ukraine alizungumza na viongozi wake

Kwa muda wa siku mbili akiwa Kyiv, Kardinali Zuppi alifanya mfululizo wa mikutano, ikiwa ni pamoja na Rais Volodymir Zelensky na Dmytro Lubinets, kamishna wa bunge wa Kiukraine wa haki za binadamu na pia na wajumbe wa Baraza la makanisa na mashirika ya kidini. Katika siku hizo, Kardinali pia alisimama katika maombi huko Bucha, mji ulio kilomita chache kutoka Kyiv ambayo iligonga vichwa vya habari mwanzoni mwa mzozo wa mauaji ya kiholela ya raia, yaliyoachwa mitaani au kutupwa kwenye makaburi ya pamoja. Matokeo ya mazungumzo hayo "bila shaka yatakuwa na manufaa kwa kutathmini hatua za kuendelea kuchukua katika ngazi ya kibinadamu na katika kutafuta njia za amani ya haki na ya kudumu", inasomeka maelezo ya Vatican.

Kard Zupi akiwa Moscow alizungumza na Patriaki wa Moscow Kirill
Kard Zupi akiwa Moscow alizungumza na Patriaki wa Moscow Kirill

Siku tatu za Kadinali Zuppi akiwa huko Moscow pia alifanya mikutano mbalimbali. Kardinali huyo hakukutana na Rais Vladimir Putin lakini alikuwa na mazungumzo marefu na Yuri Ushakov, msaidizi wa Rais wa Shirikisho la Urussi kwa masuala ya sera za kigeni, kisha na Maria Lvova-Belova, kamishna wa Rais wa Shirikisho la Urussi kuhusu haki za mtoto . Hizi zilikuwa matukio mawili ambapo kipengele cha kibinadamu cha mpango huo kilisisitizwa, pamoja na hitaji la kuweza kufikia amani inayotarajiwa sana.

Picha ya pamoja akiwa na Patriaki Kirill, Patriaki wa Moscow
Picha ya pamoja akiwa na Patriaki Kirill, Patriaki wa Moscow

Mjumbe wa Papa alianza utume wake kwa kutulia katika sala mbele ya sanamu ya Mama Yetu wa Vladimir; na wakati wa  siku ya pili ya safari,Mjumbe wa Papa pia alikuwa na mkutano, ulioelezewa kuwa wenye matunda na Vatican na Kirill, patriarki wa Moscow na Urussi yote, ambaye aliwasilisha salamu za Baba Mtakatifu na ambaye pia alijadili mipango ya kibinadamu ambayo inaweza kuwezesha suluhisho la amani”. Katika muda wa saa 72 katika ardhi ya Urussi, kulikuwa na mkutano na Baraza la Maaskofu Katoliki Urussi, ambao, pamoja na kundi kubwa la mapadre na mbele ya Mabalozi na Wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Zuppi aliongoza maadhimisho ya sherehe katika Kanisa kuu la Jimbo kuu la Mama wa Mungu huko Moscow.

Kardinali Zuppi alipata kuzungumzia na mhusika Tume ya haki za watoto huko Urussi, Maria Lvova-Belova
Kardinali Zuppi alipata kuzungumzia na mhusika Tume ya haki za watoto huko Urussi, Maria Lvova-Belova

Jijini Roma, kwenye hafla ya uwasilishaji wa kitabu cha Andrea Riccardi “Kilio cha amani” mnamo  tarehe 4 Julai iliyopita, Kardinali Zuppi alithibitisha kwa waandishi wa habari kwamba alikutana na Papa Francisko na kumwambia kuhusu utume wake na akisisitiza kwamba kipaumbele ni sasa kufanya kazi kwa ajili ya watu wasiojiweza, kama vile watoto, na kuona kama tunaweza kuanzisha utaratibu kwa ajili yao na kusaidia upande wa kibinadamu."

Kardinali Zuppi kwa hiyo baada ya utume wa Ukraine na Moscow sasa ni Marekani kuzungumzia suala la Ukraine
Kardinali Zuppi kwa hiyo baada ya utume wa Ukraine na Moscow sasa ni Marekani kuzungumzia suala la Ukraine

Kardinali Zuppi pia alielezea matumaini kwamba wanaanza na wadogo zaidi, na wale ambao ni dhaifu zaidi. Watoto lazima waweze kurudi Ukraine. Kwa hivyo, hatua inayofuata itakuwa ni kuangalia watoto na kuona jinsi ya kuwarudisha, kuanzia na wale waliodhaifu zaidi.  Kwa hiyo lengo hiyo  limethibitishwa tena tarehe 17 Julai, kwa kuzingatia kituo kinachofuata katika mji mkuu wa Marekani.

Kardinali Zuppi huko Washington

 

17 July 2023, 14:42