Wolffsohn kitabu cha kiyahudi Yerusalemu Wolffsohn kitabu cha kiyahudi Yerusalemu 

Maktaba ya Vatican imezindua programu ya kujifunza hati za Kiebrania

Kuanzia tarehe 19 Julai 2023,mpango wa mafunzo maalumu utaanza kwa ushirikiano na Seminari ya Kiyahudi ya Amerika ya Kusini ‘Marshall T. Meyer’, na sehemu kubwa ya masomo ya kina itakuwa kwa ana na kwa mbali katika mtandao.

Vatican News

Jumatano  tarehe 19 Julai 2023, Maktaba ya Kitume ya Vatican itazindua programu maalum ya mafunzo ya Maandiko ya Kiebrania kwa ushirikiano na Seminari ya Kiyahudi ya Amerika Kusini “Marshall T. Meyer”, ambapo sehemu ya mafunzo ya kina kwa Juma moja itafanyika ana kwa ana, na  mbali kwa njia ya mtandao. itafuatiwa na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali duniani na wa dini mbalimbali. Mihadhara itafundishwa na kitivo mashuhuri ikiwa ni pamoja na, miongoni mwa wengine,Mkuu wa Kiyahudi  Adolfo Roitman, David Golinkin na Ariel Stofenmacher, Judith Olszowy-Schlanger, Craig Morrison, Leonardo Pessoa, Sarit Shalev-Eyni, Marco Morselli, Stephen Metzger na Delio Vania Proverb.

Uzinduzi huo

Uzinduzi wa kozi hiyo utahudhuriwa na viongozi wa mamlaka za kidini na Vatican, kama vile mtunza maktaba Monsinyo Angelo Vincenzo Zani, Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la  Maktaba ya Kitume Monsinyo Padre Mauro Mantovani, S.D.B., makamu Mwenyekiti Timothy Janz, Mkuu wa kiyahudi  Ariel Stofenmacher, Gambera wa Seminari ya Kiyahudi huko Amerika Kusini, na mamlaka ya serikali za Israeli na Argentina.

Wanafunzi na wataalamu

Mnamo Desemba 2022, katika kipindi cha  ziara ya kwanza, wenye mamlaka ya Seminari waliweza kuchanganua hati za Kiebrania kwa mara ya kwanza, na kupendekeza kwenye Maktaba ya Vatican programu ya mafunzo iliyohusisha wanafunzi na wataalamu kutoka sehemu zote za dunia. Claudia Montuschi, mwandishi wa kilatino na mkurugenzi wa Idara ya Maandishi ya Maktaba ya Kitume ya Vatican na Delio Vania Proverbio, mwandishi wa mambo ya mashariki na msimamizi wa makusanyo ya Afrika na Mashariki ya Kati na Mashariki, walishirikiana na timu ya wataalamu wa Semina kwa miezi sita juu ya maendeleo na kwa utekelezaji wa kozi hiyo.

Urithi wa thamani sana

Mamia ya hati za Kiebrania  kwa mujibu wa waandaaji  inaarifu kuwa zimehifadhiwa katika Maktaba ya Vatican, ushuhuda wa thamani wa urithi wa kiutamaduni na kidini wa watu wa Kiyahudi. Mkusanyiko huo unajumuisha hati-kunjo za Torati, maandishi ya Biblia na ufafanuzi, fasihi ya kiyahudi, falsafa ya Kiyahudi, vitabu vya kiliturujia, mashairi, sayansi na maandishi ya kabbali. Hati hizo ni za kuanzia karne ya 12 hadi 15 na, kwa kadiri ndogo zaidi, kuanzia karne ya 9 hadi 11, vipindi vyenye hata  Vita vya Msalaba, Baraza la Kuhukumu Wazushi na kufukuzwa kwa Wayahudi kutoka Hispania. Mkusanyiko huo ni mojawapo ya mambo muhimu zaidi ulimwenguni, zaidi ya yote kwa uhalisi wa nakala na matoleo ya maandishi ambayo yametoa mwanga juu ya utafutaji wa kazi za msingi za Uyahudi. 

Kozi ya mafunzo ya kiebrania
18 July 2023, 15:28