Tafuta

2022.09.15  Picha ya Papa na rais wakati yuko ziara ya kitume nchini Kazakhstan. 2022.09.15 Picha ya Papa na rais wakati yuko ziara ya kitume nchini Kazakhstan.  (Vatican Media)

Mkataba wa Nyongeza kati ya Vatican na Kazakhstan kuanza

Imetolewa taarifa kwa vyombo vya habari Vatican,kuhusu Mkataba wa Nyongeza kati ya Vatican na Kazakhstan kuhusu uhusiano wa pande zote mbili za nchi wa tarehe 24 Septemba 1998.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican inabanisha kuwa “tangu tarehe 19 Julai 2023, utaratibu unaohitajika umekamilika kwa ajili ya kuanza kutumika kwa Mkataba wa Makubaliano ya Nyongeza kati ya Vatican na Kazakhstan kuhusu mahusiano ya pande zote  mbili za nhichi wa tarehe 24 Septemba 1998, uliotiwa saini huko Nur-Sultan, nchini Kazakhstan, mnamo tarehe 14 Septemba 2022. Kutokana na Mkataba huo unawezesha upatikanaji wa kibali cha kupata makazi huko Kazakhstan na wafanyakazi wa kichungaji.

Mkataba wa Vatican na Kazakhstan na Uteuzi wa balozi wa Colombia
19 July 2023, 15:12