Papa amemteua Balozi wa Vatican nchini Colombia
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 19 Julai 2023 amemteua Balozi wa Vatican nchini Colombia, Askofu Mkuu Paolo Rudelli,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Zimbabwe.
Askofu Mkuu Rudelli alizaliwa huko Gazzaniga (Bergamo) Italia mnamo tarehe 16 Julai 1970. Alipata daraja la Upadre kunako tarehe 10 Juni 1995 na kuwa masomo ya juu ya Sheria ya Kanisa na Shahada ya Taalimungu Maadili. Alianza shughuli za kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe 1 Julai 2001.
Katika shughuli zake za kidiplomasita aliweza kuwakilisha Vatican katika nchi ya Equador na Poland, katika kitengo cha Mahusiano kwenye Ofisi za Katibu Mkuu. Na amekuwa katika Ofisi za Uwakilishi wa Vatican wa Kudumu katika Baraza la Ulaya Strasburg, tangu tarehe 20 Septemba 2014. Askofu Mkuu Rudelli anazungumza lugha 5: kingereza, kifaransa, kispanyola, kipoland na lugha yake ya taifa Kiitaliano.
19 July 2023, 16:48