Kwa mara nyingine tena Papa amkwenda kusali na kujikabidhi kwa Mama Maria na vijana katika hija yake. Kwa mara nyingine tena Papa amkwenda kusali na kujikabidhi kwa Mama Maria na vijana katika hija yake. 

Papa Francisko akabidhi kwa mama Maria vijana na hija yake

Tarehe 31 Julai 2023 mchana Papa Francisko kama kawaida amekwenda kujikabidhi kwa Mama Maria Salus Populi Romani katika kesha kabla ya kwenda Ureno.

Vatican News

Kwa mujibu wa taarifa kwa waandishi wa habari kutoka Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, tarehe 31 Julai 2023 inasema kuwa: “Leo mchana katika kesha la Ziara yake ya Kitume ijayo huko Ureno, katika fursa ya Siku ya Vijana Duniani, Papa Francisko amekwenda kama kawaida yake katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, mahali ambapo amekaa kwa sala  mbele ya Picha ya Bikira Salus Populi Romani, akimkabidhi safari na mamia elfu ya vijana atakaokutana nao katika siku sijazo.

Kwa hiyo kwa mara nyingine tena, katika mkesha wa kuondoka kwake kuelekea Ureno asubuhi ya tarehe 2 Agosti, 2023 Papa Francisko hakukatisha utamaduni wake wa muda mrefu kuelekea katika Kikanisa hiki pendwa.  Na hii ni mara  yake ya 109 kwenda kusali hapo. Papa Francisko alikuwa ametembelea Salus Populi Romani kwa mara ya mwisho mnamo Juni 16, ili kushukuru kwa matokeo ya mafanikio ya upasuaji wa laparatomy katika Hospitali ya Gemelli. Pia katika hafla hiyo, Baba Mtakatifu alikaribishwa mlangoni na wakati wa kutoka kwa salamu ya upendo ya waamini waliokusanyika katika uwanja wa kanisa kuu hilo  baada ya  kutulia katika sala kwa muda mfupi, wakati akiketi kwenye kiti cha magurudumu, mbele ya Picha ya Bikira Afya ya Watu wa Roma

Mbali na usimamizi wa Mama Maria Baba Mtakatifu pia   alikuwa amewaomba  wamini kusimndikiza katika safari hiyo iliyokaribia kwa sala. Alifanya hivyo mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana  kwa ajili ya vijana wa  kike na kiume ambao kutoka mabara matano watakusanyika Lisbon kwa tukio la ulimwengu. Kwa hiyo  alisema:"Nawaomba mnisindikize kwa maombi yenu katika safari yangu ya Ureno, ambayo nitaifanya kuanzia Jumatano ijayo", alisema  Papa Francisko, tarehe  30 Julai 2023.

Papa alikwenda kujikabidhi kwa Mama Maria Salus Populi

 

31 July 2023, 18:23