Tafuta

2023.07.12 Makamu Rais wa Dunia wa SIGNIS,Padre Paul Samasumo akisoma Ujumbe wa Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika katika Warsha la SIGNIS Afrika kuhusu uhamiaji na ukimbizi,huko Kampala Uganda. 2023.07.12 Makamu Rais wa Dunia wa SIGNIS,Padre Paul Samasumo akisoma Ujumbe wa Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika katika Warsha la SIGNIS Afrika kuhusu uhamiaji na ukimbizi,huko Kampala Uganda.  

Warsha ya SIGNS Afrika:'Kuripoti juu ya wahamiaji na wakimbizi'

Katika Warsha iliyoandaliwa na SIGNIS Afrika kuhusu“Kuripoti juu ya wahamiaji na wakimbizi” mjini Kampala kuanza tarehe 10 -16 Julai 2023, Dk Riffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ametuma ujumbe wake akiwataka vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika kusaidia kujenga madaraja na sio kuta.

Na Angella Rwezaula, - Vatican & Paul Samasumo- Kampala

Warsha ya SIGNIS Afrika kwa ajili ya mashirika ya vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika ilifunguliwa rasmini Jumanne asubuhi tarehhe 11 Julai 2023. Warsha hiyo inafanyika katika seminari Kuu ya kitaifa ya Ggaba, ambayo ipo kilomita 9, kutoka mjini Kampala nchini Uganda na inawakutanisha waandishi wa habari wapatao 50 kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Warsha hiyo iliyoandaliwa na Signs Afrika kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, inayotafuta njia za kipekee za Kiafrika za kuweza kuzungumzia juu ya wahamiaji katika vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika kutoka katika dhana hadi ripoti za huruma zaidi zinazohifadhi heshima ya wahamiaji na wakimbizi. Kwa mujibu wa tarifa za Warsha Makamu Rais wa Signs Duniani, Padre Paul Samasumo anayeudhuria Warsha hiyo amesema kuwa  Mkutano wa juma moja kwa  wanahabari wa Kikatoliki wa Afrika ulifunguliwa Jumanne kwa ujumbe muhimu kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paulo Ruffini. Katika ujumbe wake aliouelekeza kwa Padre Walter Ihejirika, Rais wa SIGNIS Afrika na uliosomwa kwa niaba yake kwa washiriki na Padre Paul Samasumo, Makamu Rais wa Signis duniani,  Dk. Ruffini ambaye hakuweza kuhudhuria binafsi aliwataka vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika kusaidia kujenga madaraja na sio kuta. Aliipongeza nchi ya Uganda kwa ukarimu wake wa kipekee kwa wakimbizi na wahamiaji wa Kiafrika.

Washiriki wa Warsha kuhusu Wakimbizi na wahamiaji huko Kampala Uganda ulioandaliwa na Signis Afrika
Washiriki wa Warsha kuhusu Wakimbizi na wahamiaji huko Kampala Uganda ulioandaliwa na Signis Afrika

Dk. Ruffini alieleza kwa jinsi ambavyo kwa siku hizi alishiriki “katika ukumbusho wa kumi wa ushuhuda wa ajabu wa Papa Francisko, kwa safari yake ya mara ya kwanza ya kipapa nje ya Roma hadi Lampedusa, Italia. Katika kitendo kirefu cha toba, Papa Francisko amekuwa akiomba msamaha kuhusu kutojali kwetu kwa kaka na dada zetu wengi. Katika safari hiyo ya upapa wake, Baba Mtakatifu  Francisko alipenda kutikisa dhamiri za ulimwengu na kutuongoza kutafakari kuelekea badiliko thabiti la moyo.” Katika ujumbe huo, Dk Ruffini kwa njia hiyo alielezea masikitiko yake kutokuwa nao “nchini Uganda, ambayo ni nchi ya mashahidi wa Kiafrika ambapo pia inajulikana sana kwa kuwa nchi ya mfano ya kuhifadhi wakimbizi. Huku maelfu ya wanaume, wanawake na watoto waliokata tamaa wakikimbia mizozo na misiba ya asili wakitafuta mahali pa kukimbilia, Uganda imefungua milango yake sikuzote ili kukaribisha idadi kubwa ya ndugu na dada zetu”, alibainisha

Baadhi ya washiriki wa Warsha kuhusu wahamiaji na wakimbizi iliyoandaliwa na Signis Afrika
Baadhi ya washiriki wa Warsha kuhusu wahamiaji na wakimbizi iliyoandaliwa na Signis Afrika

Dk. Ruffini vile vile  aliwapongeza kwa kuchagua “mada yenye manufaa makubwa kwa mafunzo haya: si tu kwa bara la Afrika bali pia kwa mustakabali wa binadamu kwa ujumla. Mpango wao unajumuisha mpango wa kutambua na kutoa mwongozo wa SIGNIS Africa kwa watendaji wa vyombo vya habari vya Kikatoliki kuhusu kuripoti masuala ya wahamiaji na wakimbizi. Kando na kuwalenga waandishi wa habari wa Kikatoliki, miongozo kama hiyo itawajali na kuwavutia waandishi wa habari kutoka katika vyombo vya habari vya kilimwengu kwa kuripoti habari za kiutu zaidi kuhusu watu ambao tayari wamehuzunishwa na matatizo na mateso”. Ujumbe wa Mkuu wa Mawasiliano Vatican  umebanisha kwamba: “Katika ujumbe wake wa hivi karibuni kwa siku ya 57 ya Mawasiliano Duniani, Baba Mtakatifu Francisko anatualika kutakasa mioyo yetu ili kuwasilisha ukweli kwa upendo, kuzingatia kuzungumza kwa moyo, kupinga kwa kiasi kikubwa mwelekeo wa kizazi chetu kutojali na kukasirika nyakati fulani hata kwa msingi wa habari potofu zinazopotosha na kutumia ukweli.” Na “Ikiwa kweli tunaweza kutazama na kuona uhalisi na wengine kwa macho ya moyo, ikiwa tunaweza kusikiliza kwa masikio ya moyo na zaidi ya yote tukijizoeza kusema kwa moyo, tutaweza pia huruma, uwezo wa huruma ya kweli.”

Washiriki wa Warsha kuhusu uhamiaji na ukimbizi iliyoandaliwa na Signis Afrika huko Kampala Uganda.
Washiriki wa Warsha kuhusu uhamiaji na ukimbizi iliyoandaliwa na Signis Afrika huko Kampala Uganda.

Kwa maana hiyo Dk. Ruffini anaamini juhudi zao za bara katika “kushiriki mchakato wa sinodi ambao unatusukuma kama Kanisa Katoliki kufuma ushirika zaidi kwa kuangaza mioyo, na kutunza majeraha ya kila mmoja wetu kutazaa matunda mengi”. Kwa upande wake ni mategemeo ya kuimarisha “kiungo kati ya Roma na Makanisa mahalia. Vyombo vya habari vya Vatican vinatazamia na viko tayari kushiriki historia zao zaidi katika mawasiliano ambayo yanaweka uhusiano na Mungu na jirani, hasa wahitaji zaidi, waliotengwa na waliotupwa katika jamii. Hawa ni pamoja na kaka na dada zetu wanaoteseka, wanaotafuta hifadhi, watu waliohamishwa na hali ya tabianchi, wakimbizi wa ndani (IDPs), na waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Masimulizi ya kanisa la Kiafrika yanaweza kusaidia katika kumulika safari yetu ya pamoja.” Akiendelea na ujumbe huo, hata hivyo Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano alielezea hata mpango ulioanzishwa hivi karibuni na Baraza ambapo anasema “Kupitia Mpango wa Pentekoste wa Baraza la Mawasiliano, Vyombo vya Habari vya Vatican viko tayari vinasikiliza na kushiriki historia na watawa kutoka Afrika na kwingineko kama mashuhuda wa matendo makuu ya Mungu”

Rais wa SIGNIS kimataifa, Bi Helen Osman katika Warsha ya SIGNIS AFRICA kuhusu wahamiaji na wakimbizi, Kampala Uganda
Rais wa SIGNIS kimataifa, Bi Helen Osman katika Warsha ya SIGNIS AFRICA kuhusu wahamiaji na wakimbizi, Kampala Uganda

Aidha, amebainisha kuwa ndani ya mpango wa ‘Sauti za Wahamiaji’ tunashiriki katika jitihada za wamisionari kuhamasisha ushirikishwaji wa wahamiaji katika ulimwengu wa kazi kupitia elimu na mafunzo ya ufundi. Kushirikisha historia, habari muhimu na pia kuonesha katika nyanja ya umma ya ulimwengu, masuala ambayo yanaweza kupunguza shida za watu walio hatarini, ni ushuhuda wa kweli wa mshikamano katika Kanisa letu. Tunahitaji vyombo vya habari vinavyojenga madaraja na  siyo kubomoa kuta, na vinavyofanya kazi kuelekea uwiano wa kijamii. Warsha hii iweze kuchangia katika kujenga njia tofauti ya kutengeneza habari na kuzalisha uhusiano zaidi kwa hisia ya uwajibikaji zaidi miongoni mwa wadau wote wa mawasiliano ili waweze kutekeleza taaluma yao kama dhamira!”, Kwa kuhitimisha ujumbe wake, Dk. Riffini amebaimisha kwamba “Ninaomba wakati huu msaidie kila mmoja wenu kugundua upya uwezo wa Signis kuwa mtandao unaounganisha, mtandao uliofumwa kiukweli na uzuri, imani na matumaini. Siku hizi na ziwe nafasi ya mawasiliano katika huduma ya ushirika."

Askofu Giuseppe Franzello,M:C:C:I, mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Uganda akiwakaribisha washiri wa Warsha ya  SIGNIS AFRIKA kuhusu wahamiaji na wakimbizi
Askofu Giuseppe Franzello,M:C:C:I, mstaafu na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Uganda akiwakaribisha washiri wa Warsha ya SIGNIS AFRIKA kuhusu wahamiaji na wakimbizi

Naye Askofu Zziwa ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uganda na Askofu wa Jimbo la Kiyinda-Mityana aliwaambia washiriki wa Warsha hiyo kuwa uhamiaji si jambo geni. Alizungumzia jinsi Waisraeli walivyoishi Misri kama wahamiaji na watumwa hadi walipokombolewa na Bwana kupitia Musa. Askofu Zziwa alivihimiza vyombo vya habari vya Kikatoliki vya Afrika kuwa na malengo ya kujenga amani na upatanisho katika jamii. Naye Waziri wa Masuala ya Teso wa Uganda, Bwana Kenneth Ogalo Obote alizungumza historia ndefu ya Uganda ya ukarimu ambayo ilianza kati ya mwaka 1942 na 1944, wakati wakimbizi 7000 wa Poland hasa wanawake na watoto walipopata hifadhi nchini Uganda wakati wa Vita Kuu ya Pili. Wengine waliozungumza wakati wa afla ya ufunguzi ni Profesa Walter Ihejirika, Rais wa SIGNIS - Afrika pamoja na Rais wa SIGNIS Duniani, Bi Helen Osman. Kwa hakika Uganda ndiyo nchi kubwa zaidi barani Afrika inayohifadhi wakimbizi na nchi ya nne kwa ukaribisho zaidi duniani. Hii ni kutokana na sera zake za kimaendeleo kuelekea wakimbizi.

SIGNIS AFRIKA: Warsha kuhusu wahamiaji na wakimbizi inayofanyika Kampala Uganda
12 July 2023, 15:18