Tafuta

Papa Francisko na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Papa Francisko na Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.  (Vatican Media)

WYD,Lisbon,Dk.Ruffini na SIGNIS:kunahitajika Mawasiliano ambayo ni ushirika!

Wajumbe vijana wa SIGNIS walioudhuria siku ya Vijana huko Lisbon,walikutana na Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano.SIGNIS ina wanachama zaidi ya nchi 100 na kuwaleta pamoja wataalamu katoliki wa radio,televisheni,sinema,elimu ya vyombo vya habari,uchapishaji na mawasiliano ya kidijitali.

Na Angella Rwezaula,- Vatican.

SIGNIS ni Shirika lisilo la kiserikali lenye wanachama katika zaidi ya nchi mia moja. Kama Chama cha Kikatoliki cha Mawasiliano Duniani kinawaleta pamoja wataalamu wa Kikatoliki katika radio, televisheni, sinema, elimu ya vyombo vya habari, uchapishaji na mawasiliano ya kidijitali. SIGNIS ilizaliwa mnamo mwaka 2001 kutokana na muungano wa mashirika mawili yaliyoanzishwa mnamo mwaka 1928 na Chama Kikatoliki cha Kimataifa kwa ajili ya Radio na Televisheni  (Unda), pamoja na  Shirika la Kimataifa la Kikatoliki la Sinema kwa ajili ya sinema na taswira za sauti ( OCIC).

Dk Ruffini akihutubia washiriki wa Mkutano Mkuu wa SIGNIS huko Korea Agosti 2022
Dk Ruffini akihutubia washiriki wa Mkutano Mkuu wa SIGNIS huko Korea Agosti 2022

Shughuli za SIGNIS hushughulikia nyanja zote za mawasiliano: ukuzaji wa sinema au filamu za TV (pamoja na majaji wa filamu na televisheni katika sherehe kuu za kimataifa kama vile: Cannes, Berlin, Montecarlo, Venice, Mtakatifu Sebastian, na kwingineko), uundaji, utengenezaji na usambazaji wa vipindi vya radio na TV, video, ujenzi wa studio za matangazo ya radio na televisheni, usambazaji wa vifaa, huduma za mtandao wa satelaiti, uhamasishaji wa matumizi ya teknolojia mpya, elimu ya vyombo vya habari na mengine. Lengo kuu la pamoja la shughuli zote hizi ni kukuza utamaduni wa amani kupitia vyombo vya habari. Hali kadhalika  SIGNIS ni kushirikiana na wataalamu wa vyombo vya habari na kusaidia wawasilianaji wa Kikatoliki. Kusaidia kubadilisha tamaduni zao  katika mwanga wa Injili, kuhamasisha hadhi na utu wa kibinadamu, haki na upatanisho.

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa SIGNIS Agosti 2022
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa SIGNIS Agosti 2022

Ni katika muktadha huo  ambapo katika fursa ya Siku ya Vijana duniani huko Lisbon nchini Ureno, 1-6 Agosti 2023, Chombo kama hiki kisingekosekana. Ambapo SIGNIS ikiwa katika WYD olifanya mkutano katika Jumba la Makumbusho la Mtakatifu Roque huko Lisbon, wakiwa na  washiriki wa vijana wa SIGNIS na waliohudhuria kwa kumkaribishwa kwa mchango Dk. Paolo Ruffini, Rais wa  Baraza la Kipapa la Mawasiliano, ambaye alifika na kuwakumbusha jinsi ilivyo muhimu kwa Kanisa kuwa na sauti za vijana. Tutegemee Baraza, lilikuwa kama mada lakini alisema  pia litusaidie kuelewa kile tunachoweza kufanya kwa sababu “Kanisa haliwezi kufanya peke yake ikiwa halina vijana pembeni mwake. Tunahitaji kuelewa jinsi tunavyoweza kuboresha mawasiliano, jinsi tunavyoweza kujenga ulimwengu wa mtandao, na jinsi ya kusombwa nao. Tunapaswa kuelewa kwamba kila kitu hutokana na ushirika, na kwamba mawasiliano ni ushirika. Yote hayo yanakuwa kitu kimoja!” Alisisitiza kwao  Dk.  Paolo Ruffini akihutubia kundi hili la vijana, hasa  kutoka Amerika ya Kusini  wa Argentina, Colombia, Mexico  na kwingineko kwa pamoja na vyombo vyao vya habari au kuwakilisha chombo hiki cha SIGNIS.

Papa FRancisko akipokea mikumbatio kutoka kwa vijana huko Lisbon
Papa FRancisko akipokea mikumbatio kutoka kwa vijana huko Lisbon

Walikusanyika kwa ajili ya salamu, huku wakiacha kituo cha vyombo vya habari na baadaye kukimbilia ili kuungana tena Njia ya Msalaba na Baba Mtakatifu Francisko. Na hata Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa mwenyewe alikimbia kwa haraka kufika, akiwaacha wasaidizi wa Papa, na  akionesha nia yake ya kuwasikiliza vijana hao. Kwa mujibu wake alisema: “Si  juu ya kuleta  Habari  tu katika ushirika lakini ni katika maisha. Hili ndilo litakalotufanya tuwe wawasilianaji, na Baraza la Mawasiliano haliwezi kufanya hivyo peke yake. Kwa hiyo, tusaidie! Tuko hapa kusaidia nchi zote, zilizopo na ambazo hazipo. Mawasiliano yanafaa tu ikiwa yanaruhusu mikutano, mdogo, kama huu na hata mikubwa kama ile ya Lisbon. Mawasiliano ambayo husafiri kupitia mitandao pekee haitoshi, hata ikiwa ni ya kipaji na yenye ubunifu; haitoshi ikiwa haiwezi kuleta na kufanya mambo kwa pamoja, kukutana mahalia. Mkutano huo ulizinduliwa kama kifungua kinywa kwa pamoja na madhubuti katika bustani ya kijani.

Vijana wa Kujitolea katika Tukio la WYD Ureno wakisiliza Papa
Vijana wa Kujitolea katika Tukio la WYD Ureno wakisiliza Papa

Turudi nyuma tena katika historia ya  SiGNIS, katika kongamano lake la kwanza la kimataifa (1929) Unda ilitafakari umuhimu wa radio kwa maisha ya kidini, kiutamaduni na kijamii. Katika miaka ya 1930 watangazaji wa Kikatoliki walikuwa na mtazamo wenye matumaini juu ya maendeleo ya radio, na baadaye, ya njia mpya ya televisheni. Inaweza kuvuka mipaka na kuleta watu na tamaduni pamoja. Radio ilifikiriwa kama ubora wa wastani wa upatanisho katika maeneo yenye migogoro, kwa ajili ya kukuza amani na urafiki kati ya mataifa. Kama OCIC, Unda pia ilikuza vipengele mbalimbali vya elimu ya vyombo vya habari.

Mataifa yote , rangi na kabila wananishuhudia ulimwenguni kote
Mataifa yote , rangi na kabila wananishuhudia ulimwenguni kote

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia na katika miaka iliyofuata , kanuni hizi zilipata  usemi mpya katika filamu, radio na televisheni. OCIC na Unda zilipanua shughuli zao na kuwa mashirika ya kimataifa ya kweli. Kuanzia miaka ya 1960 na kuendelea, Unda na OCIC walianza kufanya hafla za pamoja, makusanyiko na mipango, ikijumuisha njia ndogo za mawasiliano, maarufu ambayo yalikuwa yakiendelea polepole. Muongo wa miaka ya 1980 ulishuhudia kuenea kwa matumizi ya video, ikifuatiwa na mageuzi ya haraka ya teknolojia ya habari na ukuaji wa vyombo vya habari vya digitali na mtandaoni. Wanachama wengi wa Unda na OCIC walifanya kazi katika vyombo vya habari tofauti, na kwa vile usimamizi wa vyombo vya habari ulikuwa pia wa pande zote, msukumo kuelekea Jumuiya jumuishi ya Kikatoliki kwa Vyombo vya Habari vya Sauti na Muonekano ukiongezeka na kusababisha kuunganishwa kwa UNDA na OCIC kutoa jina moja la SIGNIS mnamo  tarehe 21 Novemba 2001.

Hata watoto waliudhuria Siku ya vijana wakiwa na wazazi wao vijana
Hata watoto waliudhuria Siku ya vijana wakiwa na wazazi wao vijana

Kwa sababu hiyo lengo lake kuu ni kufanya kazi na wanataaluma wa vyombo vya habari na kusaidia wanawasilianaji wa Kikatoliki kusaidia kubadilisha tamaduni zetu katika mwanga wa Injili, kukuza utu wa binadamu, haki, upatanisho." Mnamo Oktoba 2014, Vatican  iliidhinisha Sheria zake za Kisheria zinazoitambua SIGNIS kama Jumuiya ya Kimataifa ya Waamini. Askofu Romero na Mtakatifu ni Msimamizi wa  SIGNIS mnamo mwezi  Juni 2015, ambapo  Bodi ya Wakurugenzi ya SIGNIS, wakati wa mkutano wake huko Puerto España, Trinidad na Tobago, kwa kauli moja waliamua kumteua Askofu Mkuu wa Salvador Oscar Arnulfo Romero kama Msimamizi wa  SIGNIS, shukrani kwa kujitolea na ujasiri wake katika hali isiyoisha ya  ulinzi wa maskini na wanyonge. Anawakilisha mfano kwa wawasilianaji wote, kama mtu ambaye aliishi maadili aliyodai, tayari kutoa maisha yake badala ya kukaa kimya mbele ya ukosefu wa haki.

Vijana wawakilishi wa SIGNIS waliudhuria WYD
10 August 2023, 13:11