Tafuta

Kuna hatari ya uharibifu wa vyakula Ulimwenguni wakati  sehemu nyingine watu wanakufa kwa njaa  na utapiamlo. Kuna hatari ya uharibifu wa vyakula Ulimwenguni wakati sehemu nyingine watu wanakufa kwa njaa na utapiamlo. 

Paglia:uchumi ukitawaliwa na mantiki ya mshikamano,chakula hakipotezwi!

Rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha alizungumza huko Santiago ya Chile katika mkutano wa FAO,akisisitiza kwamba ili kukabiliana na hali ya kusikitisha ya upotevu wa chakula,wahusika wa kiuchumi wanapaswa kutambua wajibu wao wa kijamii na uhusiano uliopo kati ya watu wote.Lakini takwimu fulani na mabadiliko ya tabia ya kula pia inahitajika.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Matumizi mabaya ya vyakula huashiria hatima ya mamilioni ya watu na suala la chakula haliwezi kushughulikiwa katika mantiki ya kiuchumi na soko tu. Hayo yamesisitizwa na Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, akizungumza kwenye mkutano wa mada:“Kuzuia na kupunguza upotevu wa chakula na upotevu katika muktadha wa usalama wa chakula na lishe. Changamoto kati ya sekta” uliyoandaliwa huko Santiago ya Chile, tarehe 24 Agosti, 2023 katika makao makuu ya Uwakilishi wa FAO kwa Amerika ya Kusini na Carribean. Askofu Mkuu  ambaye amekuwa Amerika ya Kusini tangu tarehe 23 Agosti 2023  kwa safari ambayo, pamoja na zile za Chile, pia inajumuisha vituo vya Argentina hadi tarehe 30 Agosti 2023,  alizungumzia mada hiyo akikumbuka, kwanza kabisa, kile ambacho Papa Francisko alisema mnamo tarehe 18 Mei 2019 katika hotuba yake kwa Shirikisho la Ulaya la Benki za Chakula. Kwa kunukuu alisema: “Kutupa chakula kunamaanisha kutupa watu”, kisha aliongeza kuwa upotevu huu wa watu  “hauvumiliki, na hauwezi kuvumilika, hauwezi kutekelezeka, chanzo cha aibu kubwa na kwamba kila mtu anawajibika mbele ya Mungu na historia.

Upotevu wa chakula na utapiamlo

Ikiwa utupaji wa chakula katika bara la Amerika ya Kusini lina asilimia ndogo, kwa kuwa linashughulikia asilimia 6% tu ya ulimwengu, kuna, hata hivyo, watu milioni 47 wenye utapiamlo katika bara hilo, alisema Askofu Mkuu  Paglia, huku akisisitiza kwamba kiwango cha utapiamlo katika miaka ya hivi karibuni kimeongezeka, lakini kwamba kwa kilo 69 za chakula zinazopotea kila mwaka na kila mkazi, takwimu zilizotolewa  na UN, tunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kwa lishe ya milioni 30 ya watu hawa. Kuna hali za kusikitisha katika baadhi ya nchi, aliongeza kusema Askofu Paglia ambaye alisimulia kuhusu ziara yake nchini Haiti miaka miwili iliyopita na makazi duni ya mji mkuu Port au Prince, ambako alikutana na watu waliovimba kwa vyakula visivyofaa au waliodhoofika kwa utapiamlo wa kudumu. Inawezekanaje kuendelea kujifanya kuwa hakuna kilichotokea, kuvumilia, na kutofanya chochote? ilikuwa tafakari yake ya uchungu, na mwaliko  wa kushughulikia suala hilo kwa umakini na uwajibikaji.

Mantiki ya mshikamano

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Paglia  alibainisha kuwa inatokea kwamba muundo wa kiuchumi ambao msingi wa uzalishaji, usambazaji na mabadiliko ya chakula unazidi, ni mkubwa, hata hivyo uchumi hauwezi kuzingatiwa kama lengo kuu lakini kama njia ya huduma ya watu, maisha na ujenzi wa jamii yenye uadilifu. Baba Mtakatifu Francisko alibainisha hayo katika Ujumbe wake kwa Siku ya Chakula duniani kwa mwaka 2021, akiandika kwamba mapambano dhidi ya njaa yanahitaji kushinda mantiki baridi ya soko, kwa pupa kulenga faida za kiuchumi na kupunguza chakula kuwa bidhaa kama nyingine yoyote, na kuimarisha mantiki ya mshikamano. Katika muktadha huo, Askofu alisema, lazima lielekeze katika kuzingatia kwamba kila uzoefu wa binadamu, ikiwa ni pamoja na uzoefu wa kiuchumi, umepandikizwa na kushirikiana katika ujenzi wa familia ya kindugu ya kibinadamu kama Papa mwenyewe alivyosisitiza katika ‘Waraka wa  Fratelli Tutti’, yaani ‘Wote ni Ndugu.’ Kwa hiyo, kwa watendaji wa kiuchumi ina maana ya kutambua wajibu wa kijamii wa kazi zao, muunganisho kati ya masomo tofauti, ulinzi wa watu na ulimwengu wanaokaa.

Jinsi ya kuzuia utupaji wa chakula

Kwa rais wa Chuo cha Kipapa,  alisema kuwa ili mtu yeyote asitengwe katika meza ya uzima, kuna njia tatu thabiti za kazi za kufuata. Kwanza kabisa, onesha la takwimu juu ya utupaji wa chakula na kwa hivyo tathmini ya uzito wa kijamii wa jambo hili, kuhusiana na ambayo idadi ya masaa ya kazi iliyopotea au gharama ya nishati ya shughuli kama hizo ambazo hazijakamilika hazijalishi, kwa hiyo itakuwa muhimu pia kueleza ni hasara gani katika masuala ya kijamii na kibinadamu iko nyuma ya upotevu wa bidhaa ya kilimo. Pili, ni muhimu kutazama mnyororo mzima wa chakula, aliendelea Askofu Mkuu Paglia kuelezea  kwa sababu utupaji wa chakula unaweza  kushughulikiwa  tu kupitia maono ya jumla ya ukweli, kwa hivyo mtu lazima azingatie mgawanyiko mkubwa uliopangwa wa maduka makubwa na masoko yasiyo rasmi pamoja, teknolojia iliyosafishwa zaidi na hekima ya zamani zaidi ya wakulima.

Kuonesha thamani ya Chakula na mezani

Hatimaye, ni muhimu kuonesha thamani ya chakula na meza. Ni njia ya kiutamaduni. Kwa hiyi “Tunahitaji mtazamo wa kuwajibika, hata wa kiroho, alisisitiza Askofu Mkuu huku akionesha kwamba baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa moja ya hatua muhimu za kupunguza upotevu wa chakula ni elimu ambayo inaruhusu mabadiliko ya tabia mbaya za nyumbani. Ikiwa mtu anafahamu hadhi na wema wake mwenyewe, wa wapenzi wake na mali alizonazo basi anapoteza kidogo na hufanya chakula kuwa kitendo cha kibinadamu, alihitimisha.

Hotuba ya Askofu Mkuu Paglia kwa FAO huko Amerika Kusini
26 August 2023, 14:24