Ratiba ya Maadhimisho ya kipapa kwa mwezi Septemba na Oktoba 2023
Vatican News.
Ofisi ya maadhimisho ya Litirujia za kipapa, imetoa ratiba ya maadhimisho yatakayoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi Septemba na Oktoba 2023. Kwa mwezi Septemba, Papa Francisko tarehe 22-23 Septemba 2023 anatarajiwa kufanya Ziara ya Kitume huko Marsiglia nchini Ufaransa kwa ajili ya kuhitimisha Mkutano wa “Rencontres Méditerranéennes”.
Tarehe 30 Septemba 2023 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 4.00 asubuhi unatarajiwa kufanyika mkutano wa Kawaida kwa umma na kutakuwa na uundaji wa Makardinali wapya. Tarehe hiyo hiyo 30 Septemba 2023, saa 12.00 jioni katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, kutakuwa na Mkesha wa Kiekumeni wa sala.
Tarehe 4 Oktoba 2023 ni Siku Kuu Mtakatifu Francis wa Asisisi, kwa hiyo saa 3.00 kamili asubuhi kutakuwa na Misa Takatifu na Makardinali wapya na kufunguliwa kwa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu. Tarehe 29 Oktoba 2023 katika Dominika ya 30 ya Kipindi cha Kawaida cha Mwaka A, Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, saa 4.00 asubuhi, itafanyika ibada ya misa Takatifu kwa ajili ya kuhimitisha Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Sinodi ya Maaskofu.