Tafuta

2023.09.19 Papa  Francisko mbele ya Picha ya  Salus Populi Romani kwa ajili ya Ziara yake huko Marsiglia Ufaransa 22-23 Septemba 2023. 2023.09.19 Papa Francisko mbele ya Picha ya Salus Populi Romani kwa ajili ya Ziara yake huko Marsiglia Ufaransa 22-23 Septemba 2023. 

Papa akabidhi ziara yake ya kitume ya huko Marsiglia kwa Mama Maria

Kwa mara nyingine tena,Papa amekabidhi ziara yake kwa Bikira Maria ya kwenda Marsiglia kwenye mkutano kuhusu Mediterranea.Ziara hiyo ni tarehe 22-23 Septemba 2023.

Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko aliondoka kutoka Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, asubuhi tarehe 19 Septemba 2023 na kufika kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu ambako, kama kawaida yake, alikaa kwa ajili ya sala mbele ya Picha ya Salus populi romani, yaani Bikira Maria Afya ya Waroma akimkabidhi safari yake inayofuata ya kitume kwenda huko Marsiglia nchini Ufaransa kwa siku mbili ya 22-23 Septemba 2023. Mwishoni alirudi mjini Vatican. Ni taarifa iliyotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican, kwa waandishi wa habari.

Papa ajikabidhi tena kwa Maria Salus Populi Romani

 

19 September 2023, 13:25