Papa Francisko akutana na Waziri Mkuu wa Ureno
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 28 Septemba 2023, amefanya mkutano na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Ureno Mhs. Bwana António Luís Santos da Costa, ambaye mara baada ya Mkutano huo, alikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, Akisindikizana na Katibu wa Mahusiano na Nchi na Mashirikia ya Kimataifa, Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka vyombo vya habari Vatican, inabainisha kuwa wakati wa mazungumzo yao na Katibu wa Nchi, wameonesha kupongezana kwa ushirikano mwema wa maandalizi ya Siku ya vijana diniani iliyoisha na ziara ambayo Baba Mtakatifu alitimiza huko Ureno kuanzia tarehe 2 hadi 6 Agosti 2023
Na katika mazungumzo hato wamesisitiza juu ya mchango chanya wa Kanisa kwa Jambii ya Ureno , katika muktadha wa sasa wa kisiasa na kijamii na baadhi ya masuala yanayosiana kwa pamoja. Katika mwendelezo wa mazungumzo hayo pia kulikuwapo na kubadilishana mitazamo juu ya hali ya kimataifa, kwa namna ya pekee matokeo ya vita nchini Ukraine na matukio ya uhamiaji.