Krajewski:Utume wa Vatican kwa upya kwa watu wanaoteseka Ukraine
Vatican News
Kuna masikitiko makubwa katika maneno ya Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la huruma ya Upendo ambaye alifikiwa kwa simu akiwa nchini Ukraine ambako amekwenda tena kupeleka msaada na faraja kutoka kwa Papa Francisko. Katika maneno yake wamesema “Ninahisi maumivu.” Hii inarejea kuhusu shambulio lililotokea usiku wa Jumanne tarehe 19 Septemba 2023 dhidi ya ghala la Caritas Ukraine lililoko huko Lviv. Bohari ambayo mara nyingi imetumiwa na Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo kwa ajili ya kuhifadhi vifaa ambavyo baba Mtakatifu alituma kwa ajili ya idada ya watu wenye shida. "Hapa, kwa mfano, jenereta za nguvu zilitumwa, kisha kusambazwa katika maeneo yaliyotengwa zaidi kutokana na migogoro." Caritas imetaarifau kuwa "ghala hilo na kila kilichokuwamo kiliteketezwa hadi chini, takriban tani 300 za misaada ya kibinadamu ziliteketea kwa moshi, kwa bahati nzuri hakukuwa na waathiriwa katika shambulio hilo.”
Kardinali Krajewski kwa hiyo amefikia eneo la Lviv kwa sababu, pamoja na kupeleka kuna msaada, uzinduzi wa makazi ya wanawake na watoto, “Casa del Riparo”, uliopangwa, ambali limejengwa kutokana na msaada wa Papa na wafadhili wengi na ambalo litasimamiwa na watawa wa Albertine. Kwa mujibu wa taarifa kuntoka Baraza la Kipapa la huduma ya upendo ni kwamba: “Nyumba hii ilijengwa wakati wa mzozo ili kusaidia watu wengi waliotoroka kutoka katik maeneo yaliyopigwa mabomu na ambao, hawakutaka kuondoka nchini, walitafuta hifadhi huko Lviv. Kwa hiyo hawa ni Mama wasio na waume pamoja na watoto wao na wanawake wasio na makao ambao watapata ukarimu huko katika vyumba vilivyotayarishwa vya kutosha.”
Ndani ya Jengo hili kuna jiko la kupikia supu pia inayotolewa kwa masikini na kuwapatia chakula cha moto na mahali pa kukaribisha. Kwa njia hiyo Mwakilishi wa Kipapa atazindua nyumba hiyo kwa jina la Papa Francisko, kama ishara ya msaada, na ukaribu kwa watu wengi ambao wamelazimika kukimbia kutokana na migogoro, na kuleta Baraka za Kitume. Kardinali Krajewski pia alipanga kutembelea jumuiya mbalimbali zinazowakaribisha wakimbizi na kuwashukuru wajitolea wote na wale wote wanaosaidia watu wanaoteseka na wanaohitaji, mbali na makazi yao.