Kard.Parolin: kinachoendelea katika Mashariki ya Kati ni zaidi ya kufikiria
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Akianza hotuba yake mjini Camaldoli, mwishoni mwa semina ya siku nne iliyoandaliwa na Il Regno na Jumuiya ya Watawa wa Kibenediktini juu ya mada Swali la tatu. Kanisa, Wakatoliki na Italia," tarehe 8 Oktoba 2023, Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican alionesha wasi wasi unaongezeka wa ghasia nchini Israeli. "Mawazo yetu kwa wakati huu yanageukia kile kinachotokea Mashariki ya Kati, Israeli, Palestina na Ukanda wa Gaza," alisema Kardinali Parolin huku akikumbusha kwamba ombi la Papa Francisko la kuombea amani wakati wa sala ya Malaika wa Bwana "limerudiwa na karibu kila mtu na serikali za dunia ili kukomesha vurugu. Matukio haya yanaweka hatari zaidi ya matumaini dhaifu ya amani ambayo yalionekana kuibuka katika upeo wetu hata kwa makubaliano na Saudi Arabia."
Juhudi za kidiplomasia
Kardinali Parolin pia alisema, "Zaidi ya juhudi za kidiplomasia ambazo hazionekani kuwa na matokeo makubwa na pia ninasema hivyo nikirejea vita vya Ukraine ni lazima sote tuungane katika sala ya kwaya kwa ajili ya amani." Na kwa upande wa mahojiano yaliyofanyika kando ya mkutano huo wasiwasi mkubwa wa Kardinali alisema: "Hatujui jinsi itakavyobadilika na itaishaje. Kinachotokea kinakwenda zaidi ya yale tunayoweza kufikiria."
Matumaini tete ya amani
Akiwa amehuzunishwa,Kardinali Parolin alisema kuwa "ulimwengu unaonekana kuwa wazimu, na inaonekana kwamba tunategemea nguvu, vurugu, migogoro tu, kutatua matatizo yaliyopo ya kweli, lakini mahitaji hayo ni ya kutatuliwa kwa njia nyinginezo. Zaidi ya uharibifu wa maisha ya wanadamu, ambao tumeshuhudia kwa njia ya kutisha, Kardinali Parolin aliendelea kusema kuwa matumaini tete ya amani ambayo yalionekana kuibuka kwa kiasi fulani katika upeo yanapanda kabisa moshi. Kwa hivyo itahitaji juhudi kubwa zaidi la kuchukua hatua na kujaribu kufikia suluhisho la amani ambalo ndilo suluhisho pekee sahihi na suluhisho pekee la ufanisi ambalo litaepuka kurudiwa kwa hali hizi".
Umoja wa Ulaya ulianzishwa kwa msingi wa amani
Kardinali Parolin aliitilia shaka juu ya Ulaya na jukumu lake kwamba, "Kwa sababu Ulaya ilianzishwa hasa kama uzoefu wa kimsingi wa amani baada ya majanga makubwa ya karne ya ishirini na sio tu ndani bali hata nje yake. Hata hivyo alisema kuwa, anaamini kwamba matatizo yaliyopo ndani ya Umoja wa Ulaya,na ugumu wa kuhusiana na njia ya haki na hali halisi nyingine, kufanya jukumu hili la amani ambalo Ulaya inapaswa kujihusisha na duniani kuwa gumu. Hivyi ni matumaini kwamba Ulaya itarejesha jukumu hilo na mwelekeo huu, lakini yeye haoni uwazi huo. Hata hivyo Ulaya kama upeo wa amani ilikuwa ndiyo mada ya mchango wake katika hotuba huko Camaldoli. Uvamizi wa Ukraine, vita na uharibifu wa eneo lake pia unahusisha uharibifu wa sheria na haki za kimataifa ambazo uwezekano wa kuishi pamoja kwa amani unategemea, hadi tishio la matumizi makubwa ya silaha za nyuklia Kardinali Parolin alisema katika hotuba ya kwamba "Ulaya haiwezi kukubali kurudi kwa mfumo unaoweka upya mipaka kwa nguvu".
Doa lipo katika historia ya Ulaya
Katika hilo alitaja kile alichokiita "vita vya ubeberu mamboleo" na maono ambayo yanakumbuka mambo ya nyuma ambayo "yaliaminika kuwa yamepitwa na wakati". Kwa hiyo ni muhimu kusisitiza tena kulaani utaifa, hasa wale wenye asili ya kikabila. Ni doa linaloelemea historia ya Ulaya na ni kielelezo cha majanga mapya. Misingi na utaifa wa aina mbalimbali hauwezi kuhalalishwa, kama ilivyo kwa yoyote." Zaidi ya hayo, anaamini kwamba ingawa ni lazima tuchukue hatua ili kurejesha ulazima kamili wa utaratibu wa kimataifa unaounga mkono na wa amani, hatuwezi kushindwa kutambua thamani kamili ya mifumo ya kitaasisi inayojikita katika ushirikishwaji wa kidemokrasia wa wananchi, ambao ni muhimu kuepusha dhana ya vita".
Mchakato wa Sinodi inayoendelea
Katibu wa Vatican alikemea kiwango cha mgawanyiko wa jamii ya kisasa "iliyojaa maswali kwa kuzingatia uchunguzi huu, alitualika kwa mara nyingine tena kuleta ujumbe wa Injili kwa Ulaya na kwa Wazungu. Neno ndilo linalookoa, kwa hiyo linaalika "tangazo la furaha, utamaduni wa mazungumzo, heshima, wajibu, kujitambua". Sala yake pia inahusu kazi inayoendelea ya sinodi kuwa : "Mchakato unaoendelea wa sinodi utusaidie kugundua tena ushirika kama njia ya uinjilishaji, kuwa mashahidi thabiti na wa kuaminika zaidi wa umoja na amani leo, kwa bara la Ulaya". Alihitimisha.