Daktari Ruffini akitoa taarifa kuhusu habari za Sinodi Jumamosi 14 Oktoba 2023 Daktari Ruffini akitoa taarifa kuhusu habari za Sinodi Jumamosi 14 Oktoba 2023 

Katika sinodi,maombi mapya kwa ajili ya Nchi Takatifu na duniani

Wito mpya wa amani ulitolewa kwa washiriki wa sinodi waliokusanyika katika chumba cha Paulo VI.Uongofu kwa kusikiliza,kukaribisha utofauti na jukumu la wanawake ndio mada zilizojitokeza wakati wa mkutano wa Jumamosi na waandishi wa habari katika Ofisi ya Vatican.Kuhusu upatikanaji wa hati zilizohifadhiwa na watu nje ya Sinodi,Dk.Paolo Ruffini alitangaza kwamba hazikuwa na siri yoyote.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Sinodi inayoendelea mjini Vatican, yote ilianza na dakika ya ukimya kufikiria juu ya matukio ya kutisha katika Nchi Takatifu na vita vilivyosahaulika ulimwenguni kote. Wajumbe 340 waliohudhuria Jumamosi tarehe 14 Oktoba 2023  kwenye Sinodi ya Kisinodi inayoendelea mjini Vatican, kwa mara nyingine tena walisali kwa ajili ya amani na maombi kama ya kwaya. Muda mfupi baadaye zilijitokeza habari za kifo cha Katibu wa Caritas Siria na kifo cha kaka wa mshiriki wa Sinodi z katika mkutano wote ambapo walishirikishana huzuni hiyo ambayo kama ilivyo furaha imekuwa  mtindo kamili wa sinodi, kwa urahisi, kama inavyotokea katika familia zote duniani. Hayo  yote yalibainishwa Jumamosi mchana  tarehe 14 Oktoba 2023 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ofisi ya Vyombo vya Habari mjini Vatican.

Sr. Maria aliongoza mkutano

Kwa mara ya kwanza, kikao cha Ijumaa kiliongozwa na mwanamke: Sr. Maria De Los Dolores Palencia Gómez, wa Shirika la Mtakatifu  José de Lyon. Kama Mtawa wa zaidi ya miaka 50, Sr Maria alijitolea kwa ukakamavu na upendo kukaribisha na kusaidia mamia ya wahamiaji katika muundo wa Jengo  linalokaribisha wanaume, wanawake na watoto kutoka Amerika ya Kusini na maeneo mengine yaliyosahaulika. Wakati wa sinodi, Sr.  Maria alileta uzoefu wake wa usaidizi usio na masharti na ushirikishwaji wa watu ambao mara nyingi wamesahaulika na kutengwa katika jamii. Kwa mujibu wake alisema "Tunachopitia ni njia ya kusikiliza kwa makini ambayo inaakisi  sauti ya Roho Mtakatifu," aliwaambia waandishi wa habari wakati wa kuingilia  kwake kati. Mtawa huyo pia alitaka kusisitiza kwamba kazi za sinodi zinazoongozwa kwa mara ya kwanza na mwanamke haziwakilishi tukio la bahati mbaya “bali ni mtindo wa kuishi unaoendelea katika Kanisa, ukiwaita wabatizwa wote kuwajibika pamoja na, wakati huohu  kuwa na  heshima kwa kila aina na kila mtu.

Uongofu kwa kusikiliza

Uzoefu wa kushiriki katika Sinodi iliyosimuliwa na Padre Mauro Giuseppe Lepori, Abate Mkuu wa Shirika la  Cistercian, unarejeea aina  ambayo kwa namna fulani ni ya kimapinduzi: ubadilishaji wa kusikiliza.  Kwa upande wake alisema mwenyewe, akithibitisha zaidi ya mara moja kwamba anajifunza njia halisi ya maisha kutoka kwa kazi hii.  "Katika njia hii mpya ya sinodi tunayoifanyia majaribio," alifichua, kuwa "tunaelewa kwamba washiriki wote wanatembea sehemu ya njia pamoja." Mtawa huyo ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa Umoja wa wa Wasimamizi Wakuu wa Italia, alisaidiwa na maelezo madogo ambayo yanaweza kuonekana kuwa yasiyo muhimu kwa mtazamo wa kwanza: umbo la meza ya mduara katika vikundi vidogo kuwa: "Wao ni mviringo, na kuwa bega kwa bega katika vikundi vidogo  ambavyo husaidia kujenga uhusiano wa kina na urafiki wa karibu." Na zaidi ya yote, vinakuza kumsikiliza Roho Mtakatifu: "hatimaye, yote muhimu ni kile alichosema," Padre Mauro alihitimisha.

Sauti ya watu wenye ulemavu

Kutoka katikakazi ya sinodi pia sauti inayogusa roho, ilitoka  ndani kabisa yenyewe. Ni ile ya Enrique Alarcón García, rais wa “Frater España”, yaani  udugu wa Kikristo unaoleta pamoja watu wengi wanaoishi na ulemavu nchini Hispania. Enrique alifika kwenye Chumba cha Waandishi wa Habari akiwa kwenye kiti cha magurudumu. Maneno yake ya kwanza kwa waandishi wa habari yalikuwa maneno ya shukrani. "Kwanza kabisa, kwa Baba Mtakatifu," alisema kwa tabasamu, "aliyetaka niwepo kwenye Sinodi. Kwa sababu uwepo wangu haukuwa utaratibu rahisi, sikuwekwa hapa ili kupeperushwa kama bendera. Enrique alisema kuwa , Papa Francis, "siku zote anavutiwa na jinsi watu wenye ulemavu wanavyoishi katika Kanisa na kile wanachofikiria kulihusu. Hatukuwa tumezoea hilo." Ikiwa katika ulimwengu, watu wanaoishi na ulemavu hawazingatiwi na kuteseka uzito wa ukosefu wa kuzingatia katika maeneo ya kazi, shule na mafunzo, hii sivyo katika Kanisa. Na Sinodi inathibitisha hilo, Enrique alitoa hoja: “Sasa, katika Kanisa, tuna hisia ya kuwa sehemu hai, ya kuwa washiriki wa kueneza Injili. Mabadiliko ya kweli yanafanyika."

Jukumu la wanawake

Katika swali la mwandishi wa habari ambaye alitaka kujua ikiwa uwezekano wa kuwekwa wakfu kwa wanawake ulijadiliwa wakati wa kazi ya Sinodi, Padre Mauro Giuseppe Lepori alijibu kwamba "katika Sinodi sio mada kuu: haikujadiliwa; lakini shemasi wa kike hakika lilijadiliwa.” Sinodi, ilimalizia ile ya kidini, ili “kuepuka kushughulikia matatizo kwa kuyaondoa katika muktadha. Kwa maoni yangu, jambo muhimu zaidi kwa wanawake ni suala la ushiriki wao katika maisha hai ya Kanisa.”

Dk.Ruffini:maelezo ya hati katika Cloud - wingu sio usiri 

Kwa upande wa Dk. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na rais wa Tume ya Habari, aliibua suala la usiri wa hati, akirejea nakala fulani zilizochapishwa juu ya ripoti za vikundi vidogo. Sekretarieti kuu ya Sinodi, alieleza, iliunda kitu kama Cloud yaani Wingui la  kushirikisha baadhi ya nyaraka na wajumbe wa Sinodi. Upatikanaji wa ripoti hizi ulihitaji utambulisho yaani - jina la mtumiaji na nenosiri - lakini kwa vile baadhi ya wajumbe, kwa sababu mbalimbali, hawakuweza kufikia, Sekretarieti Kuu iliamua kuunda kiunga kilicho wazi kwa wale wanaojua anwani ili waweze kupata hati za wingu moja kwa moja, bila vitambulisho. Hadi mwisho wa  sehemu ya kwanza, wingu (Cloud) lilikuwa na hati za umma pekee, yaani, maandishi ya ripoti walizopokea waandishi wa habari na picha ambazo zilishirikishwa kama ushuhuda na nyaraka. Mwishoni mwa sehemu ya kwanza, kutokana na ugumu huo kwa baadhi ya wajumbe, sekretarieti iliamua kupakia kwenye wingu (Cloud)mihtasari ya vikundi 35 vya kazi kwenye kipengele cha A.

Kwa upande mwingine, maudhui ya kibinafsi ambayo kila mjumbe alikuwa ameweza kushirikisha katika makutano kwa ujumla hazijapakiwa, alieleza kwa kina. Lengo ni kuruhusu wajumbe a wote kupata taarifa muhimu kwa ajili ya utambuzi wao wa sinodi. "Hizi sio hati," aliongeza kusema , "ambazo zinaweza kufafanuliwa kuwa "zilizoainishwa," lakini ni  hati za siri zenye lengo la kulinda nafasi ya utambuzi wa pamoja. Ili kuhakikisha usiri na utambuzi wa kawaida, alisisitiza, "iliamuliwa kurejesha wajibu wa jina la mtumiaji na nenosiri". "Hakuna siri," Ruffini alihitimisha, "lakini ni upendelea wa  Sekretarieti Kuu ya Sinodi ambayo ni kudumisha usiri kuhusu ripoti za kibinafsi za kila kikundi  kidogo."

 

16 October 2023, 15:10