Padre E.Samwel Kyando ni Askofu mpya wa Jimbo la Njombe,Tanzania
Na Angella Rwezaula,- Vatican.
Alhamisi tarehe 19 Oktoba 2023, Baba Mtakati Francisko amemteua Padre Eusebio Samwel Kyando kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe Tanzania. Alizaliwa tarehe 7 Machi 1964 huko Njombe. Baada ya majiudo yake ya Seminari ndogo ya Mtakatifu Kizito Mafinga, Jimbo la Iringa, aliendelea na falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustine Peramiho, Songea. Na Alipewa daraja la upadre mnamo tarehe 19 Juni 1996 kuwa kuhani wa Jimbo la Iringa nchini Tanzania. Hadi uteuzi wake alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Maendeleo na Mwakilishi wa Kuteuliwa kama Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Njombe, Tanzania.
Nyadhifa
Katika maisha yake ya utume alishika nyadhifa kadhaa na masomo: Paroko Msaidizi wa Matamba, Mratibu wa Jumuiya ya Vijana UVIKANJO na Mwalimu wa Dini katika Shule ya Sekondari Itamba (1996-1997); Paroko Msaidizi wa Mlangali, Mratibu wa Parokia ya UVIKANJO na TYCS na Mwalimu wa Dini na Maarifa ya Biblia katika Shule ya Sekondari Ulayasi (1997-1999); Mwalimu na Mkufunzi katika Seminari Ndogo ya Mtakatifu Joseph, Kilocha(1999); Stashahada ya Juu ya Uhasibu na Fedha kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, Tanzania (SAUT) (1999-2002); Msaidizi wa Mafunzo katika Idara ya Uhasibu na Fedha katika SAUT (Mwanza) na Mshauri wa Kitaalamu wa Ofisi ya Uhasibu ya Chuo Kikuu (2004); Mwalimu wa Uhasibu wa Kitaalamu katika Chuo Kikuu cha Tasmania nchini Australia; Paroko msaidizi wa Parokia ya Kikatoliki ya Sandy Bay na Taroona na aliyehusika na huduma ya kichungaji ya wahamiaji wa Kiafrika katika Jimbo Kuu la Hobart, Australia (2005-2006);
Msaidizi na Mwalimu SAUT; Mwalimu wa Utawala wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Moyo Mtakatifu huko Milano; Mhasibu wa Umma Aliyethibitishwa (CPA-T)-Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (2007-2011); Mwasibu Mkuu, jimbo la Njombe (2011); Afisa Fedha na Ofisi ya Mrengo wa Hazina katika Benki ya Biashara ya Mkombozi, inayosimamiwa pamoja na Baraza la Maaskofu Tanzania TEC (2012-2015); Masomo ya Shahada ya Uzamivu katika Utawala wa Biashara katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki (CUEA),mjini Nairobi, Kenya (2015-2021); Hadi kuteuliwa kwake alikuwa Mwakilishi wa kuchaguliwa kama Msimamizi wa Kitume(tangu 2021).