Sinodi,Catacombs-Washiriki watembelea makaburi ya Wakristo wa kwanza
Ni Angella Rwezaula, - Vatican.
Ni mara ya kwanza kuyaona, ni uzoefu wa kina kujionea mwenyewe mahali ambapo Kanisa na imani yangu ilianzia. Haya yalikuwa ni maneno ya Askofu wa China Yohane, Yang Xiaoting aliyeguswa moyo, aliposhirikisha na baadhi ya waandishi wa habari hisia za hija hiyo ambayo, Alhamisi tarehe 12 Oktoba 2023 karibu washiriki 250 wa Sinodi ya kisinodi walipitia katika makaburi ya Mtakatifu Sebastian, Mtakatifu Calist na Mtakatifu Domitilla. Huu ulikuwa ni uzoefu wa kupumzika kidogo kwa washiriki wa sinodi waliokusanyika tangu tarehe 4 Oktoba 2023 katika Ukumbi wa Paulo VI, ulioandaliwa kuwaleta makardinali, maaskofu, wanaume na wanawake watawa, walei na wageni maalum kwenye mizizi ya imani ya Jumuiya za kwanza za Kikristo Roma.
Hapo ni pale ambapo njia ya Petro na Paulo ilifungamana, ishara ya ule umoja katika utofauti ambao Papa anatumaini kuwa itakuwa alama ya Sinodi yenyewe. Wakiweka kando viatu na kuvaa soksi, mkoba na koti kutokana na kutelemka chini ya ardhi, Washiriki wa sinodi walishuka hadi mita 12 kwa kina, kuingia chini kabisa ya ardhi ili kujionea makaburi ya Mapapa wengine wa karne ya III na IV kwenye kuta zilizochorwa samaki, njiwa, nanga mambo ambayo wakati ule yalikuwa ni alama za kuashiria Ukristo.
Kumbukumbu ya Mkataba wa Catacombs
Kwa njia hiyo kulikuwa na muda wa sala na pia wa historia na kumbukumbu ambayo ilifanyika siku moja baada ya ukumbusho wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican na ambao nyakati zile zile za Mtaguso huo zilikumbusha mara moja katika akili za wengi, waliorejea tarehe 16 Novemba 1965 ambao mababa 42 wa Baraza, hasa kutoka Amerika ya Kusini, walitia saini Mkataba maarufu wa Catacombs. Ni mapatano ambayo maaskofu na mapadre walijitolea kuunda "Kanisa maskini", lisilo na alama zote na mapendeleo ya mamlaka ili kuwaweka maskini katikati ya huduma ya kichungaji. Ahadi ambayo inaweka wazi sasa wakati huu wa kazi ya sinodi, inayolenga - kati ya mambo mengine - jinsi Kanisa linavyoweza kusindikiza kila aina ya "umaskini" leo hii kama vile: kutengwa, kubaguliwa wahamiaji, wahanga wa vita na unyanyasaji.
Mahali pa kukumbatiana kati ya Petro na Paulo
Kila mmoja akiwa na kijitabu cha lugha yake, kilicho sambazwa mlangoni wakati wa kuingia, washiriki wa hija hiyo walisali katika Basilika, wakibaki kimya kwa muda mfupi. Aliyemkaribisha kila mtu alikuwa Monsinyo Pasquale Iacobone, rais wa Tume ya Kipapa ya Akiolojia Takatifu ambayo ilishirikiana katika mpango huo. "Katika njia ya sinodi ni muhimu kuwasilisha maeneo haya muhimu sana ya wazo la Kanisa. Ni ziara ambayo tunataka kufufua katika hafla ya Jubilei ijayo," alisema. Katika sehemu hizi za umuhimu wa kihistoria na kiroho, Petro na Paulo walikutana. Hapa"maelewano ya mitume" yalipatikana, Monsinyo Iacobone alikumbuka, "mfano wa kwanza wa kukumbatiwa kwao na kuwa Kanisa moja". "Ujumbe" kwa Kanisa lakini pia kwa ulimwengu wa leo ili "tofauti zipatanishwe."
Hollerich: kwa hija kutoka kwa Mtakatifu Petro hadi Makanisa yetu
Naye Kardinali Jean-Claude Hollerich, Msemaji Mkuu wa Sinodi, alizungumza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Sebastian, akikumbuka maisha ya Wakristo wa kwanza wa Roma na ushuhuda wa wafiadini waliozikwa kwenye makaburi. "Hija hii kutoka kwa Mtakatifu Petro ni hija ya uhalisia wetu, kwa uhalisia wa Makanisa yetu", alisema, akitualika "kupata maana ya njia hii ya Mungu katika uhalisia wetu", ambapo daima kuna kuakisi msalaba. kwa kuongeza alisema, "Sisi maaskofu lazima tuangalie msalaba wetu na kusema: Bwana ninakupenda, ninachukua msalaba na kukufuata".
"Njia" katika imani ya asili
Wakiwa wamegawanywa katika vikundi vya lugha na ratiba zilizoundwa kwa ajili ya makadinali wakubwa na maaskofu, washiriki mbalimbali kisha walianza safari yao katika Catacombs tatu. Kwa kikundi cha Kiitaliano mbali na kuacha Makumbusho ya Mtakatifu Sebastiano ambapo kuna hata makaburi ya mwishoni mwa karne ya 5 yanayooneshwa. Kisha mteremko kupitia ngazi zenye mwinuko, wakishikilia kuta, ambazo zimeimarishwa na matofali ya kuchoma, ukipita kwenye korido chini ya mita mbili juu. Sauti ya "Attention Excellency, the head", yaani kuwa makini vishwa wadhama ilisikika kila mara kutokana na ufinyu . “Ya kuvutia”, “ya ajabu”, maoni mengine hasa kutoka kwa wale ambao, wakiwa wametoka katika mabara na nchi za mbali, walikuwa bado hawajapata fursa ya kutembelea sehemu zinazolinda ishara za imani asili, sakramenti na tumaini la ufufuko.