Video ya kuhuisha Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani pamoja Papa

Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limechapisha“muhtasari wa filamu ya toleo la Siku ya 109 Wahamiaji na Wakimbizi iliyoadhimishwa mnamo Septemba 24,2023na ambayo inajumuisha picha na ushuhuda wa sherehe nyingi katika Makanisa na jumuiya mahalia.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Siku ya 109 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani iliyoadhimishwa  manmo tarehe 24 Septemba 2023 na Makanisa yote duniani na katika jumuiya za waamini walikusanyika ili kujionea  na kutafakari kwa wakati huu pamoja wa sala na ushirika pamoja na kaka na dada zao wakimbizi kwenye makambi ya ndani na nje ya Nchi zao. Katika kufanikisha maadhimisho hayo, wengi wametuma  katika Baraza la Kipapa la  Huduma ya Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya  Binadamu picha na shuhuda mbalimbali za jinsi walivyoadhimisha siku hiyo. Majibu mengi pia yalipokelewa kutokana na maswali ambayo Baraza hili lilikuwa limeuliza wakati wa kampeni yenye kauli mbiu  hasa ya Waraka wa Baba Mtakatifu katika fursa ya Siku isemayo: Uhuru wa kuchagua kuhama au kubaki.”

Ni lazima kila mwanadamu apate maisha yenye hadhi

Kwa njia hiyo Baraza la Kipapa la Huduma ya  Kuhamasisha Maendeleo ya Binadamu, imekusanya Baadhi ya picha hizo ambazo zimeweza kutengeneza video ili kuiishi siku hiyo katika sehemu mbali mbali. Hata givyo ukumbukwe kuwa Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana katika  Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani 24 Septemba 2023 alibanisha jinsi ambavyo: “ni lazima kila mwanamume na kila mwanamke ahakikishwe uwezekano wa kuishi maisha yenye heshima, katika jamii anamojikuta na hivyo basi tujitolea kujenga “jamii zilizo tayari na wazi kukaribisha, kuhamasisha, kusindikiza na kufungamanisha wale wanaobisha hodi kwenye milango yetu.”

Wengi wanahama kutoka na matatizo

Hata hivyo katika Kauli mbiu kuhusu Uhuru wa kuchagua au kubaki ni kutaka kutafakari kwa kina na ufahamu mpya kuhusu haki ya kuhama au kubaki nyumbani na katika nchi yako mwenyewe. Baba Mtakatifu Francisko hata hivyo anabainisha jinsi ambavyo kuna sababu nyingi ambazo zinapelekea watu kulazimika kuyahama makazi nan chi zao, ili kutafuta: hifadhi, usalama na maisha bora zaidi. Haki ya kubaki nchini mwako ina mizizi yake katika maisha ya mwanadamu, kwani hii ni haki kwa ajili ya ustawi, maendeleo na manufa mwa wengi. Ni haki inayomwezesha mtu kuishi kwa kuzingatia utu, heshima na haki msingi na hivyo kujipatia maendeleo fungamani pia. Haki inapaswa kulindwa na kudumishwa na wote. Watu wengi wanateseka kutokana na migogoro ya ndani, umaskini na Mabadiliko ya tabianchi hali nyingine za kisiasa,ambazo pia ni sababu ya kuhama kwa watu walio wengi.

VIDEO KUHUAU AIKU Y wakimbizi na wahamiaji

 

26 October 2023, 15:21