Tafuta

2023.11.24  Parolin akiwa chuo kikuu cha Kipapa cha Gregoriana katika kongamano kuhusu Papa  Luciani (foto ©Teresa Tseng Kuang Yi) 2023.11.24 Parolin akiwa chuo kikuu cha Kipapa cha Gregoriana katika kongamano kuhusu Papa Luciani (foto ©Teresa Tseng Kuang Yi) 

Kard.Parolin:Elimu ni muhimu ili kuepuka vitendo vya kutisha vya ukatili dhidi ya wanawake

Kando ya Mkutano kuhusu Papa Albino Luciani Kardinali Parolin akiulizwa maswali kuhusu siku ya kutokomeza ukatili duniani alisema,"Tunahitaji kazi kubwa ya ushirikiano kwa upande wa mashirika yote ya elimu bila ujumbe unaopingana.Na kuhusu mzozo wa Mashariki ya Kati alisisitiza ukaribu wa Papa"kwa yeyote anayeteseka" na alihimiza msamaha ambao sio rahisi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kardinali Petro Parolin, Katibu wa Vatican akiwa kando ya Kongamano kuhusu Papa Luciani katika  Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma, tarehe 24 Novemba 2023 lililoandaliwa na Mfuko wa  Vatican wa Yohane  Paulo I ambao yeye ni rais,  alijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya matukio mbali mbali ya sasa. Kwanza kabisa, alielezea juu ya kesi za mauaji ya wanawake, katika usiku wa  Mkesha wa maandamano  makubwa ya tarehe 25  Novemba jijini Roma katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Kukomesha ukatili dhifdi ya wanawake duniani. Kwa hiyo Unyanyasaji dhidi ya wanawake, jukumu la  Vatican  kwa ajili ya ufumbuzi wa kimataifa juu ya mgogoro wa tabiachi, vita tena, Papa ambayo si kitu kingine zaidi ya ukaribu na maumivu ya kila mtu, thamani ya msamaha wa kukabiliana na vurugu yoyote au hisia ya vurugu. Kwa siku ya tatu mfululizo katika mazungumzo na waandishi wa habari pembezoni mwa tukio, hilo  Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, alielezea juu ya  masuala ya sasa yanayotoa ufafanuzi na tafakari la kufikiria

Mada ya umuhimu mkubwa baada ya mauaji ya kikatili ya kijana Giulia Cecchettin ambaye atakuwa katikati ya maandamano ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake yaliyoandaliwa tarehe 25 Novemba2023, siku iliyotengwa kwa mada hiyo, kwenye Uwanja wa Circus Maximus huko Roma. Kardinali Parolin anarejea maneno ya Papa Francisko ambaye, katika Mkutano wa  mashirikisho ya vyombo vya habari vya Kikatoliki, aliwataka kuwaelimisha vijana "kukuza mahusiano mazuri". "Lazima tusisitize juu ya elimu. Papa anapozungumza juu ya mafunzo, anazungumza juu ya elimu hasa ya vizazi vipya ili kuondokana na mawazo ambayo yanaweza kusababisha vitendo hivi vya kusikitisha, vya kutisha na kuanzisha utamaduni wa heshima. Kuna hitaji la kweli kwa kazi kubwa ya ushirikiano kwa upande wa mashirika yote ya elimu, juu ya yote yanaenda kwa mwelekeo huo huo na hayatumii ujumbe unaopingana, kwa maana ya kuimarisha maadili  msingi ya kuishi pamoja na pia uhusiano kati ya jinsia hizo."

Palipo na watu wanaoteseka, Papa yupo

Alipoulizwa kuhusu shutuma zilizotolewa hivi karibunu na Mkuu wa Kiyahudi Italia  kwa Papa na baadhi ya maneno yake kuhusiana na mzozo wa Mashariki ya Kati, Kardinali Parolin  anarejea kusema: "Sio usawa wowote bali ni kugawana maumivu ya kila mtu". "Nasisitiza juu ya hili: ni mtazamo wa kibinadamu, Papa yupo na yuko karibu na wale wote wanaoteseka. Hii haimaanishi kutotambua kwamba kuna tofauti, tofauti, ina maana kwamba wakati watu wanateseka Papa yupo". Katika hali ambayo aina tofauti za unyanyasaji zinaonekana kutawala, Kardinali Parolin alihimiza "kukuza aina nyingi za maadili ambayo huturuhusu kujibu kwa amani chokochoko hizi". Kwanza kabisa, msamaha: “Bila msamaha hatuwezi kusonga mbele, ni sheria ya kulipiza kisasi pekee inatumika. Na mduara haufungi kamwe. Ninaelewa kuwa kusamehe sio rahisi, tunapitia sisi wenyewe - alikubali Kardinali Parolin - lakini ikiwa mtu ana ujasiri, ikiwa ana ujasiri wa kuvunja mduara huu, kitu kipya kinatolewa ulimwenguni".

Mamlaka ni huduma

Akikumbuka maneno ya Alessandro Manzoni yaliyoripotiwa na Papa Luciani katika kitabu chake Illustrissimi, kadinali huyo anakariri kwamba "mamlaka yote ni huduma kwa wengine, kwa sababu vinginevyo inakuwa ni matumizi ya kidhalimu ya mamlaka, kwa hiyo ikiwa mtu anawekwa juu ya wengine kwa sababu anashikilia nyadhifa wajibu lazima aishi hivi si kwa maslahi binafsi, si kupata matokeo ya kibinafsi ya aina mbalimbali bali kujiweka kikweli katika huduma ya wengine." Hivi ndivyo Mafundisho ya Kijamii ya Kanisa yanavyosisitiza: “Siasa ni huduma kwa manufaa ya wote. Na hii inawahusu mapadre, inawahusu maaskofu, pia inamhusu Papa”, anasema katibu huyo wa serikali.

Papa katika Cop28

Hatimaye alijibu maswali kuhusu safari za baadaye za Papa. Kadinali "hajui kama kuna ziara iliyopangwa  kuelekea Ukanda; ikiwa amepokea mwaliko, "itakuwa ni yeye, Papa, anayezingatia, kutafakari na kuamua nini cha kufanya, lakini sidhani kama ni mpango uliotoka kwake". Kinyume chake, kuhusu safari inayokaribia ya Papa kuelekea Dubai kwa ajili ya COP28, Kardinali Parolin alisisitiza jinsi hii itakavyokuwa mchango zaidi katika dhamira ambayo Baraza Kuu linatekeleza "kwa umakini na kwa kina" juu ya suala la hali ya hewa. "Kuanzia Laudato Si' kumekuwa na juhudi kubwa kwa upande wa Holy See kuongeza kiwango cha ufahamu wa shida na suluhisho", anasisitiza kardinali huyo. "Kiti cha Holy See haitoi masuluhisho ya kiufundi, sio kazi yake, haina njia, lakini inaweza kuwa dhamiri ya maadili juu ya suala hili na juu ya mengine mengi kwa Jumuiya ya Kimataifa na kusisitiza kuwa umakini ulipwe na kutafutiwa suluhisho kimataifa."

Maswali na majibu kwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican.
25 November 2023, 11:25