Kardinali Pironio ni mmoja watakaotangazwa wenyeheri wapya
Na Angella Rwezaula, Vatican.
Wakati wa Mkutano na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na Baba Mtakatifu, ametoa idhini ya Baraza hilo kuwatangaza wenyeheri wafuatao, kufuatia na muujiza wa maombezi ya mtumishi wa Mungu Kardinali Eduardo Francesco Pironio, wa Kanisa Takatifu la Roma; alizaliwa huko Nueve de Julio (Argentina) tarehe 3 Desemba 1920 na kifo chake Roma (Italia) itarehe 5 Februari 1998. Kardinali kwa walio wengi walimfahamu kama "rafiki wa Mungu", kama askofu mkuu wa wakati huo wa Buenos Aires Jorge Mario Bergoglio alivyomfafanua. Kwa kila mtu, yeye ndiye aliyeunga mkono na kisha kuandaa Siku za Vijana Ulimwenguni, akitimiza matakwa mazito ya Mtakatifu Yohane Paulo II.
Aliendeleza wazo la Papa kuunganisha vijana wote ulimwenguni WYD
Kama mkuu wa Baraza la Kipapa aliendeleza wazo la Papa la mkusanyiko mkubwa ambao ungehusisha wavulana na wasichana kutoka ulimwenguni kote. Wazo dogo ambalo liliibuka baada ya muda na kuwa moja ya hafla kubwa zaidi ya Kanisa Katoliki: Siku ya Vijana Ulimwenguni. Kwa Pironio, mwanzo wa utumishi wake katika Curia pia ulilingana na ugunduzi wa uvimbe wa kibofu ambao ulisababisha, kwa mateso makubwa, hadi kifo chake huko Roma mnamo 5 Februari 1998. Mwili ulihamishiwa Argentina, kwenye patakatifu pa Marian huko Luján. , mahali pale pale alipopokea ubatizo na kuwekwa wakfu uaskofu. Amri kuhusu asili ya fadhila za kishujaa za kutangazwa mwenyeheri zilikuwa ni tarehe 18 Februari 2022.
Mtumishi wa Mungu Padre Giuseppe Marrazzo
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Padre Giuseppe Marrazzo, Kuhani wa Shirika la Waroganisti wa Moyo wa Yesu; alizaliwa tarehe 5 Mei 1917 huko Mtakatifu Vito ya Normanni (Italia) na kifo chake tarehe 30 novemba 1992 huko Messina (Italia). Alikuwa wa Puglia akitoka katika familia maskini, tunamkumbuka hasa kwa ajili ya utume wake huko Messina ambako alijitolea kwa namna ya pekee kuungamisha akifuata mfano wa Mtakatifu Leopoldo Mandić Mkapuchi wa Croatia.
Mtumishi wa Mungu Sr Eliswa
Kwa njia hiyo wengine ni Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Eliswa wa Mwenyeheri Bikira Maria Zamanai aliitwa: Eliswa Vakayil), Mwanzilishi wa Shirika la Wakalmaenti wa Tatu wasio na vitatu, na sasa ni Watawa wakalmeri wa Teresa; alizaliwa tarehe 15 Oktoba 1831 huko Ochanthuruth (India) katika familia inayojiweza na kuwa na msingi wa dinia na alikufa tarehe 18 Julai 1913 huko Varapuzha (India); Hata hivyo akiwa mjane alichagua maisha ya sala na upweke, alijitolea kuwatunza maskini na aliishi katika kibanda cha kawaida. Mnamo mwaka wa 1862, pamoja na Padre Mkarmeli wa Kiitaliano asiye na viatu, Leopoldo Beccaro, aliunda Shirika la kwanza mahalia huko Kerala, Masista wa Wakarmeli wateresa, waliojitolea kwa ajili ya elimu ya wasichana maskini na mayatima na kuwasaidia walioachwa na wahitaji. Pamoja na shughuli zake, Mama Eliswa alichangia kukuza ubinadamu na kiakili kwa wanawake katika muktadha changamano wa kijamii na kidini wa India mwanzoni mwa karne ya 19 na 20.
Mtumishi wa Mungu Sr. Naria Francesca Foresti
Na hatimaye fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Maria Francesca Foresti (zamani aliitwa: Eleonora), Mwanzilishi wa Shirika la Masisita Wafransiskani waabuduo katika sehemu mbali mbali za udugu; alizaliwa tarehe 17 Februari 1898 huko Bologna (Italia) na alifariki mnamo tarehe 12 Novemba 1953 huko Ozzano Emilia (Italia). Hata hivyo katika mipango hiyo ambauo haikuwa daima rahisi na mwishowe ikawa nzuri. Mnamo 1919, alishiriki shana na Padre Pio wazo la kujitolea kwa ajili ya maisha ya tafakuri yaani ya ndani, kwa kukuza ibada maalum kwa Ekaristi. Alijitolea kwa ajili ya elimu ya vijana kwa mafundisho ya Katekisimu, akiwafundisha kuishi maisha ya utii huku akiheshimu uhuru wa kila mtu. Na afya mbaya, kutokana na matatizo ya moyo, ilisababisha kifo chake akiwa na umri wa miaka 55 tu.