Kongamano la mafunzo,Kipimo cha Jumuiya ya Utakatifu Nov 13-16
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza Watakatifu mwaka huu 2023, limeandaa Kongamano katika misingi ya kuelewa vizuri juu ya utakatifu ikiongozwa na mada ni: "Kipimo cha Jumuiya ya utakatifu". Kuanzia kwenye katiba ya imani ya Lumen Gentium, kutafakari juu ya wito wa ulimwenguni pote kwa utakatifu wa watu wa Mungu. Katika muktadha huo Kongamamo hilo lilifunguliwa kuanzia Jumatatu tarehe 13 Novemba 2023 kwa uchambuzi wa kina wa mada kutoka katika mtazamo wa kibiblia na kijamii. Utakatifu si tu kama utimilifu wa utimilifu wa maisha ya kimaadili, lakini ni kama msukumo wa uhusiano, uzoefu wa 'kugusa' wa maisha halisi ya Mungu. Ndiyo kilikuwa ni kiini cha tafakari ya Kadinali José Tolentino de Mendonça, mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu ambayo ilizindua Kongamano hilo katika Chuo Kikuu cha Kipapa la Baba wa Kanisa Agostiniano, ambalo ni kongamano la siku tatu hadi 16 Novemba 2023.
Aliyesimamia tafakari hizi tarehe 13 Alasiri na 14 Asubuhi alikuwa ni Dk. Alessandro Gisotti, naibu mkurugenzi mwariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano na kama mwenyenyeji, aliyetoa utangulizi wa kuanza kongamano hilo alikuwa ni Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu ambaye alielezea roho ya mtazamo uliopitishwakwa kongamano hili la mwaka huu 2023 kwamba ni kutazama kwa kina Kanisa kama makazi ambayo utakatifu unastawi. Alitaja hata Waraka wa Rerum novarum uliokuwa unahusu mabadiliko ya mapinduzi" au Haki na Wajibu wa Mtaji na Kazi, uliotolewa na Papa Leo XIII tarehe 15 Mei 1891. Na kwamba ni wito wa utakatifu na mwito wa mapambano. Alikazia pia juu ya Barua za Mtakatifu Paulino wa Nola aliyomwandikia Mtakatifu Agostino. Hiyo ilikuwa ni mnamo mwaka 395 Mtakatifu Paulino wa Nola alitoa sifa kubwa kwa Agostino kwa vitabu vile vitano vya kutetea imani ya Kikristo dhidi ya Wamanichaeans, vitabu alivyoviita “Pentateuco”, vilivyopokelewa na Alypius na kuomba kazi nyingine zinazowezekana dhidi ya uzushi na wakati huo huo alimsihi awe kiongozi na mwalimu wake katika kupaa kwa Kikristo, ambako kulianza kuchelewa, katika kutenda jambo ambalo bado halijakamilika sana (n. 3-4). Katika muktadha huo pia Mtakatifu Paulino wa Nola alimtumia mkate kama ishara ya maelewano (n. 5).
Kardinali Semeraro akiendelea alikumbusha utakatifu wa walio wadogo ambapo alimtaja Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu ambaye ndani yake Roho Mtakatifu alifuatilia njia ya uhalisi kwamba hakuwahi kutafuta kitu kingine chochote isipokuwa ukweli ambao ulifunua kwake kina cha Upendo wa Utatu na njia ya kuufikia, bila wasiwasi wowote kwani kila kitu kilitoka katika maisha, katika matukio ya kila siku kusoma tena kwa nuru ya Neno la Mungu. Na ndiyo neema na nuru. "Kuna msemo kutoka kwa mwandishi wa zama za kati, Fulgentius wa Ruspe, ambaye alisema kwamba katika Kanisa tumeunganishwa kwa kila mmoja na tukijitenga na sisi si kitu. Hii inatumika pia kwa utakatifu.
Wakati Jumanne tarehe 14 Novemba 2023, Kongamano linaakisi mwelekeo wa kiroho wa "kuishi pamoja", juu ya ushirika katika mwanga wa Majisterio ya Papa Francisko na wito wa utakatifu katika Kanisa mahalia pamoja na uwasilishaji wa baadhi ya shuhuda. Katika sehemu ya kwanza alikuwa ni Profesa Massimo Borghesi Mfalsafa na profesa wa Chuo Kikuu cha Perugia amejikita na mada ya Utakatifu ujenzi wa umoja katika nuru ya Magisterio Papa Francisko. Baada ya kuelezea historia ya Upapa wa Papa Francisko, uchaguzi wa jina la Mtakatifu Francis na kabla akiwa huko Bueno Saires, tasaufi ya Ignatius wa Loyola na mengine mengi kuhusu watakatifu Profesa Borghesi alisema huwa anakasirika sana anaposikia watu wakisema kuwa Mafungo ya Kiroho ni ya Ignatian tu kwa sababu yanafanywa kimya kimya. Kiukweli Mafungo yanaweza kuwa ya Ignatian kabisa hata katika maisha ya kila siku na bila ukimya. Ile inayosisitiza kujinyima, ukimya na toba ni mawazo mabovu ambay yameenea pia katika Jumuiya, hasa katika muktadha wa Kihispania. Badala yake yuko karibu na mawazo ya fumbo, y aule wa Louis Lallemant na Jean-Joseph Surin. Na Favre alikuwa mtu mtafakari wa mafumbo." Huu ni ushawishi ambao Papa alisisitiza tena katika mahojiano na La Croix, mnamo Mei 2016.
Wazo la Favre ni "kurudi kwa maisha ya Kanisa la awali". Ni jibu kwa mzozo wa kimaadili na wa kidini wa Kanisa la kiulimwengu la wakati huo. Ni kutokana na mabadiliko ya maisha, kutoka katika ushuhuda halisi wa imani na mapendo kwamba tunahitaji kuanza tena, kwa sababu uovu hauishi, kwanza kabisa, katika akili, katika mawazo, lakini katika nafsi: Kwa Savoyard, mpasuko unaongeza juu zaidi ya maadili au kiakili; mwanzo uko moyoni, kwa hiyo pia mwanzo wa kila mkutano. Tunahitaji kutunza moyo. Hivi ndivyo Mazoezi ya Ignatiu yalilenga, Mageuzi ya Kanisa kupitia mageuzi ya kibinafsi. Mpango ambao unafanana kwa karibu na ule wa Bergolio Papa Francisko akiwa kijana wa Mkoa katika Kanisa la Argentina la miaka ya 1970. Katika kumbu kumbu yake ya Favre anaelezea maisha haya ya kitume: “Mwili wa Kristo, maisha ya Kanisa, kazi ndogo ndogo za maisha ya kila siku, maskini na watoto, kila kitu ambacho kinamhusisha Favre na ulimwengu huu pia kinamfanya aguse shughuli isiyoeleweka na isiyoonekana pia inajitoa yenyewe chini ya kivuli cha vinavyoonekana na hasa, katika uaminifu wa kila siku. "Utakatifu katika maisha ya kawaida ya watu wa Mungu, usiofungamana na mavazi ya kikanisa, unafungua maono ya maisha ya Kikristo yanayovuka upeo wa "Ukristo" katika maana ya zama za kati-kisasa. Kama Luigi Accattoli alivyoandika mnamo 2012: Kwa ukumbusho huo, Papa mpya anajionesha kuwa mfuasi wa kufikiri upya kwa "utakatifu wa kisheria" ambao unafungua njia ya utambuzi wa aina za "ukamilifu wa Kikristo" ambazo hazikidhi kiwango cha "nguvu za kishujaa" za kijadi. Papa Wojtyla alikuwa ametaka ziznzishwe michakato kwa nia ya kuwatangaza wenyeheri, watu walioishi katika ndoa na taaluma yoyote. Kardinali Ratzinger katika Kitabu chake cha La mia vita yani maisha yangi (San Paolo 1997) alikuwa ametaja suala hili hivi: "Nina hakika kwamba watakatifu hawa 'wadogo' ni ishara kuu kwa wakati wetu."
Kwa kufikiri upya "utakatifu wa kisheria" haimaanishi kuushinda, wala, kwa hakika, kuachwa kwake. Kwa mujibu wa misemo ya watu ambayo ni sifa ya mawazo ya Jorge Mario Bergoglio tunakabiliwa umaarufu. Mvutano uliooneshwa vyema katika hotuba iliyoelekezwa kwa washiriki wa mkutano ulihamasishwa na Braza la Kipapa la Mchakato wa Kuwatangaza Watakatifu tarehe 6 Oktoba 2022. Hapa Papa, baada ya kuelezea juu ya utakatifu katika watu watakatifu wa Mungu, alibainisha jinsi ambavyo Kando, au tuseme, kati ya umati huu wa waamini, ambao Profesa amewafafanua kama watakatifu wa mlango wa karibu" (Gaudete et exsultate, 7), kuna wale ambao Kanisa linawaonesha kama mifano, waombezi na walimu. Watakatifu wanakuwa "ishara" wanapomwakilisha, bila kutenganishwa, Yesu na watu wanaoamini. Wanamwakilisha Mungu, mkubwa asiye na kikomo, kwa kiwango ambacho wamezama katika udogo usio na kikomo, nafasi na wakati wa watu. Hii ndiyo ilikuwa maana ya uimbaji wa mazishi ya Ignatius ambayo lazima yalimgusa sana kijana Bergoglio. Kuwa ishara inatolewa na ukweli kwamba kila mtakatifu ni hatua ya awali kati ya umaalum na wa ulimwengu wote, kati ya Mungu na ulimwengu. Kwa maneno ya kikanisa: kati ya maana ya Kikatoliki ya Unam Sanctam yaani waraka wa kipapa uliotolewa na Papa Boniface VIII tarehe 18 Novemba 1302 anbao uliweka mapendekezo ya kidogma juu ya umoja wa Wakatoliki na utamadunisho katika hali fulani.
Watakatifu Thomas More, Vincent wa Pauli, Philip Neri, ambao tunapaswa kuongeza Fransis wa Assisi na Mwenyeheri Yohane Paulo I na Charles Acutis, ni watakatifu wenye furaha, wale ambao kwao, si vigumu kufikiria, upendeleo wa Papa unakwenda kwao pia ni watakatifu wa kijamii ambao walijua jinsi ya kuunganisha furaha ya Mungu na huruma kwa wengine. Wao ni tofauti na wale Wakristo wanaotenganisha madai haya ya Injili kutokana katika uhusiano wao binafsi na Bwana, kutoka katika muungano wa ndani Naye, kutoka katika neema. Kwa hivyo Ukristo unabadilishwa kuwa aina fulani ya Shirika lisilo la Kiserikali (NGO), na kuinyima ule mwanga wa hali ya kiroho ya kutishia ambayo Mtakatifu Fransis wa Assisi, Mtakatifu Vincent wa Pauli, Mtakatifu Teresa wa Calcutta na wengine wengi waliishi na kudhihirisha vyema. Kwa watakatifu hawa wakuu, wala maombi, wala upendo wa Mungu, wala usomaji wa Injili ulipunguza shauku na ufanisi wa kujitolea kwao kwa wengine, lakini ilikuwa ni kinyume kabisa. Watafakari na matendo, kama vile Pierre Favre, ni muunganisho wa maisha ya Kikristo ambayo kiini chake ni Kristo. Kitovu sio wazo tu, dhahania, lakini halisi, kiontolojia.
Katika Waraka wa Gaudete et exsultate Papa anaingiza sura, isiyo ya kawaida katika maandishi juu ya utakatifu: ya pili iliyowekwa kwa maadui wawili wa hila, Gnosticism na Pelagianism(wakana Mungu au wasio amni). Yote mawili yanawakilisha namna za kujihesabia haki, za kujionesha nafsi yao wenyewe ambayo inachukua nafasi ya Mungu, na kuifanya isiwezekane kwa neema yake kufanya kazi. Ni kinyume cha utakatifu. Mtakatifu sio shujaa anayemtazamia Mungu, anayemtangulia, bali ni yule anayemfuata, anayemtegemea kabisa. Mtakatifu ndiye anayesukumwa na ukweli kwamba Mungu alifanyika mwanadamu, ambaye anashangaa na kustaajabishwa, ya kushangaza, ya Kupata Mwili kutoka kwa Mungu. Kwamba asiye na kikomo amekuwa na kikomo, kwamba Bwana wa kuwa amekuwa mtumishi, asiye na kitu, siri hii kuu, ambayo inakuwa dhahiri na ya kawaida kwa Wakristo waliokwisha kufanywa, waliozoea, wataalimungu, ni moyo wa imani ya watakatifu ambayo msingi wake ni shukrani, kwa kushukuru daima. Kwa sababu hii, kwa msisitizo ambao haujaonekana vya kutosha, Papa Fransisko anaweka uwezekano wa utakatifu leo hii katika ufahamu mpya, uliojaa shukrani, wa moyo wa imani: Mungu alifanyika Mwili akawa mwanadamu.
Huu ndio moyo wa Kerygma ambao, katika Waraka wa Evangelii gaudium, yaani Furaha ya Injili, lazima itangulie, hasa katika ulimwengu usio na dini, matokeo ya kimaadili-maadili ya imani. Papa alisema haya mara nyingi. Katika mojawapo ya hayo alirejea, kwa mara nyingine tena, kwa Joseph Malègue. Ilikuwa katika mpango wa programu "Ave Maria", iliyoandaliwa na Padre Marco Pozza, ambayo ilitangazwa mnamo 13 Novemba 2018. Katika tukio hilo Papa Francisko , akizungumza juu ya dhana ya "tabaka la kati la utakatifu", alifafanua: Si yangu. Niliiba kutoka kwa mwandishi Mfaransa, Joseph Malègue. Ni yeye aliyethubutu kusema: "Kashfa na ugumu sio kuelewa ikiwa Mungu yuko, lakini kuelewa kwamba Mungu alifanyika Kristo."Hii ndio kashfa. Na Mama Maria yuko katikati ya kashfa hii. Utakatifu ndiyo kitovu cha kashfa hii. Hatuwezi kuelewa utakatifu bila kuelewa kashfa hii: kwamba Mungu alifanyika Kristo, yaani, mwanadamu kama sisi. Kwa hilo hatuko tena katika upeo wa Usomaji Mamboleo, unaotawaliwa na tatizo la uthibitisho wa kuwepo kwa Mungu, bali katika ule wa Wazalendo ambao kwao tatizo lilikuwa ni jinsi gani inawezekana kwa Mungu kufanyika mwanadamu. Watakatifu walio karibu nasi leo hii ni wale wanaojiweka kwenye upeo wa Kanisa changa ambalo, katika ulimwengu wa kipagani,linaitwa kushuhudia uwepo wa Mwana wa Mungu,amehitimisha.