Baba Mtakatifu, Jumatatu tarehe 27 Novemba 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Santiago Peña Palacios wa Paraguay. Baba Mtakatifu, Jumatatu tarehe 27 Novemba 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Santiago Peña Palacios wa Paraguay.  (Vatican Media)

Rais wa Paraguay Akutana na Kuzungumza na Papa Francisko Mjini Vatican

Baba Mtakatifu, Jumatatu tarehe 27 Novemba 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Santiago Peña Palacios wa Paraguay ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa. Mkazo: Uhusiano wa Kidiplomasia, Mapambano dhidi ya umaskini; haki na amani duniani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko bado anakabiliwa na changamoto za kiafya na hivyo ameendelea kufanya shughuli muhimu katika ratiba yake ili kujipatia mapumziko ya kutosha kadiri ya ushauri wa madaktari. Baba Mtakatifu, Jumatatu tarehe 27 Novemba 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Santiago Peña Palacios wa Paraguay ambaye baadaye amekutana na kuzungumza na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican aliyekuwa ameandamana na Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje, Ushirikiano na Mashirika ya Kimataifa.

Papa akutana na kuzungumza na Rais wa Paraguay
Papa akutana na kuzungumza na Rais wa Paraguay

Baba Mtakatifu pamoja na mgeni wake katika mazungumzo yao ya faragha wameelezea kuridhishwa kwao na uhusiano mwema wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili na kwamba, wametia nia ya kuimarisha mahusiano haya. Baadaye wamegusia changamoto na fursa za Serikali ya Paraguay, ya kutaka kujikita kikamilifu katika mapambano dhidi ya baa la umaskini linalosigina na kuyanyanyasa malioni ya watu nchini Paraguay. Viongozi hawa wawili baadaye wamegusia mada mbalimbali hasusan kuhusu utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, hali halisi ilivyo nchini Paraguay sanjari na mchakato wa kujikita katika kutafuta na kudumisha misingi ya haki, amani na upatanisho kati ya watu wa Mataifa.

Paraguay
27 November 2023, 14:59