Toleo la Novemba la Wanawake katika Kanisa,Ulimwenguni:Kutoka mtaguso hadi Sinodi
OSSERVATORE ROMANO
Toleo la Novemba 2023 la "Donne Chiesa Mondo", ambalo kichwa cha habari katika jarida la kila mwezi la wanawake la Osservatore Romano, linaloratibiwa na Rita Pinci, linarejesha juu ya mchakato wa safari ya wanawake katika Kanisa, tokea Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican hadi Sinodi ya Kiinodi ya hivi karibuni iliyohitimishwa awamu ya kwanza Oktoba 29,2023. Kwa hiyo katika toleo hili la Novemba, linaongozwa na kichwa cha "Kutoka ukimya hadi neno" ambapo katika jalida hili linaoneshwa picha mbili, ambazo utafikiri kama kioo japokuwa ni tofauti sana. Picha ya kwanza ilichukuliwa mnamo Septemba 1964: yenye kichwa wao ni "mama wapatanishi" siku walipoingia katika Kanisa la Mtakatifu Petro, wanawake 23 (wa kitawa na walei) walikubali kazi lakini kama wasikilizaji tu.
Picha ya pili ni ya mwezi Oktoba 2023: ni " mama wa sinodi" walioingia katika Ukumbi wa Paulo VI kwa ajili ya Sinodi ya Maaskofu, ambapo kwa mara ya kwanza wanawake 54 waliweza kupiga kura. “Ulimwengu wa Kanisa la Wanawake wa Kanisa Ulimwenguni” wanaeleza jinsi ambavyo nafasi, jukumu na mwamko wa wanawake katika Kanisa umebadilika katika miaka sitini; maendeleo lakini, kwa miongo kadhaa, pia baadhi ni kinyume, kama ilivyosisitizwa na Mercedes Navarro Puerto, mtawa wa Shirika la Mercedaria na mwana Biblia, ambaye anaandika kuhusu watawa baada ya Mtagusi na kutoa ushuhuda wake akiwa mstari wa mbele.
Kulikuwa na uingiliaji mwingi wa wale walioelewa na kupata uzoefu wa Mtaguso kama waamini, na kama mtawa au katika maisha yao ya kitaaluma na kisiasa. Cettina Militello, kati ya wanawake wa kwanza wa Italia walioandikishwa katika kitivo cha Kitaalimungu; Sr. Nicla Spezzati, kati ya wa kwanza kuwa na nafasi ya juu ya Curia; Rosy Bindi, kiongozi wa( Chama Matendo Katoliki) na baadaye waziri wa Jamhuri ya Italia. Kama mwandishi, Carola Susani anasimulia kupitia barua ya kuwazika kwa msichana wa leo hii tafakari za mama wa Mtaguso. Na kuna uzoefu katika harakati za wanawake walei, katika Chama cha Matendo ya Kikatoliki, katika skauti, katika Harakati ya Wafocolari kwamba: Wakatoliki ambao tayari kabla ya Mtaguso na walikuwa mstari wa mbele wamegundua uhusika mkuu wa wanawake nje ya nyumba na ndani ya Kanisa.