Kongamano Novemba 13-16 kuhusu Wito wa Utakatifu Ulimwenguni!
Vatican news.
Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza Watakatifu, hata mwaka huu 2023, limeandaa Kongamano kwa ajili ya msingi kuhusu Mchakato wa kutangazwa Watakatifu kwa kuongozwa na mda ya: "Kipimo cha Jumuiya ya utakatifu". Kwa kuanzia kwenye katiba ya imani ya Lumen Gentium, kutafakari juu ya wito wa ulimwenguni pote wa utakatifu wa watu wa Mungu. Kwa hakika, utakatifu kimsingi ni wa jumuiya kwa sababu unatoka kwa Mungu Utatu na, kwa sababu hiyo, katika mwili wa fumbo la Kristo ambao ni Kanisa Takatifu. Kwa upande wake, kila mtu aliyebatizwa anajibu kwa utakatifu wa kibinafsi, kwa sababu amemwilishwa na maisha ya kisakramenti na kusikiliza Neno.
Ratiba ya Kongamano kuanzia 13 hadi 16 Novemba
Katika muktadha huo Kongamamo hilo litafunguliwa kuanzia Jumatatu tarehe 13 Novemba 2023 kwa uchambuzi wa kina wa mada kutoka kwa mtazamo wa kibiblia na kijamii. Jumanne tarehe 14 Novemba 2023, Wataakisi mwelekeo wa kiroho wa "kuishi pamoja", juu ya ushirika katika mwanga wa Majisterio ya Papa Francisko na wito wa utakatifu katika Kanisa mahalia pamoja na uwasilishaji wa baadhi ya shuhuda. Siku iliyofuata, Jumatano tarehe 15 Novemba, itakuwa ni kujihoji juu ya uhusiano kati ya utakatifu wa jumuiya na mambo matatu msingi ya kuishi pamoja kama vile: Liturujia, maisha ya ndoa na siasa. Siku ya mwisho tarehe 16 Novemba 2023, Washiriki wa Kongamano watakutana na Baba Mtakatifu.
Kila siku ni kufunguliwa na Kardinali Semeraro
Kila siku Kongamano hilo limegawanywa katika muundo unaoanzia kutoa ripoti na hatimaye mwishoni mwa kila Kikao, kuna uwezekano wa mazungumzo katika ukumbi, shukrani pia kutokana na uratibu wa mwandishi wa habari. Katika mwendelezo wa Kongamano la mwaka 2022, Kongamano hilo linalenga kuwakilisha operesheni ya kiutamaduni na kitaalimungu ili kutumia, leo hii, kwa kuzingatia mienendo mipya ya tathmini, vigezo vya mapokeo ya Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na mjadala wa kitaalimungu. Kongamano hilo linatambulishwa na kuhitimishwa kwa uingiliaji kati Kardinali Marcello Semeraro ambaye ndiye Mwenyekiti wa Baraza hili.
Kwa yeyote anayetaka maelezo zaidi anaweza kubonyeza hapa:https://www.causesanti.va/it.html au https://www.causesanti.va/it/eventi/dimensione-comunitaria-della-santita.html