Askofu mkuu mteule Giovanni Cesare Pagazzi alizaliwa tarehe 8 Juni 1965 huko Jimbo Katoliki la Crema, Kaskazini mwa Italia. Askofu mkuu mteule Giovanni Cesare Pagazzi alizaliwa tarehe 8 Juni 1965 huko Jimbo Katoliki la Crema, Kaskazini mwa Italia.   (AFP or licensors)

Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi, Katibu mkuu Baraza la Utamaduni na Elimu

Askofu mkuu mteule Giovanni Cesare Pagazzi alizaliwa tarehe 8 Juni 1965 huko Jimbo Katoliki la Crema, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 23 Juni 1990 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Lodi, Italia. Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian na kubahatika kufundisha Taasisi kadhaa za Kanisa nchini Italia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Monsinyo Giovanni Cesare Pagazzi, Mratibu wa tafiti na Profesa wa Elimu kuhusu Kanisa na Jaalimu wa Taasisi ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo wa Pili, tarehe 30 Novemba 2023 ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu na kumpandisha hadhi ya kuwa ni Askofu mkuu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Giovanni Cesare Pagazzi alizaliwa tarehe 8 Juni 1965 huko Jimbo Katoliki la Crema, Kaskazini mwa Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 23 Juni 1990 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Lodi, Italia.

Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi, Katibu mkuu wa Utamaduni na Elimu
Askofu mkuu Giovanni Cesare Pagazzi, Katibu mkuu wa Utamaduni na Elimu

Baadaye alijiendeleza kwa masomo ya juu na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian na kubahatika kufundisha Taasisi kadhaa za Kanisa nchini Italia. Pamoja na nyadhifa mbalimbali alizobahatika kuwa nazo, Askofu mkuu mteule Giovanni Cesare Pagazzi ni Jaalimu katika Taasisi ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo wa Pili na pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Taasisi ya Sayansi ya Kidini ya “Sant’Agostino” Jimbo kuu la Lodi, Italia. Kuanzia mwezi Oktoba 2021 amekuwa ni Mshauri katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.

Uteuzi: Utamaduni na Elimu
04 December 2023, 13:41