Askofu Mkuu Parra-kongamano la miaka 75 ya mahusiano ya Kanisa na serikali,Italia
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Askofu Mkuu Edigar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Vatican alitoa hotuba yake iliyojikita na mada: ”Mazungumzo na ushirikiano kwa ukuaji wa jamii,” wakati wa kuhitimisha Kongamano la “miaka 75 ya Mahusiano kati ya Serikali ya Italia na Kanisa Katoliki kwa utaratibu wa kikatiba,” lililofanyika Alhamisi tarehe 14 Desemba 2023 kwenye ukumbi wa Baraza la Manaibu Wabunge, jijini Roma. Askofu Mkuu Parra alisema kuwa: “Ushirikiano mzuri kati ya Serikali na Kanisa, kanuni iliyofichika katika mfumo wa makubaliano, imeibuka karibu kama mpango wa kufuata na kufanya usawa wa miaka hii kuwa mzuri, uliojengwa juu ya umuhimu wa mazungumzo, habari inayofaa na uthamini wa majukumu na miundo.”
Tangu mnamo 1948, mwaka ambao Katiba ya Jamhuri ya Italia ilianza kutumika, ambayo kati ya baba zake waalinzilishi ilikuwa na watu wa kweli wa imani kama vile Giorgio La Pira, Giuseppe Dossetti na Alcide De Gasperi, kwa “miaka 75 ya mahusiano kati ya Serikali ya Italia na Kanisa Katoliki kwa utaratibu wa kikatiba,” mahusiano hayo yamekuwa thabiti na yenye kujenga na kubaki hivyo kwa vile yanaelekezwa kwenye uhakikisho makini wa utu wa kila mtu kama mtu binafsi na katika makundi ya kijamii kama ilivyotolewa kifungu cha II cha katiba ya Katiba ya Italia.” Kama ushahidi wa hilo, Askofu mkuu Parra alisisitiza kuwa “makubaliano ya Ikulu ya 1984, ambayo Mkataba wa 1929 ulirekebishwa, pamoja na makubaliano na maelewano mbalimbali yaliyofuata juu ya vipengele vya kibinafsi vya maendeleo ya serikali na ya Kanisa.”Kwa hiyo haja ilihisiwa kusasisha sehemu hizo za Makubaliano ya Laterano yasiyoitikia tena mageuzi ya nyakati na kwa muktadha wa kisiasa na kijamii wa Italia, alifafanua Peña Parra, huku akithibitisha tena kwamba Serikali na Kanisa Katoliki, kila mmoja katika utaratibu wake wa kujitegemea na uhuru.” Hilo la mwisho, kimsingi, limetambuliwa kuwa na uhuru kamili wa kutekeleza utume wake wa kichungaji, kielimu na upendo wa uinjilishaji na utakaso, kuhakikisha kwamba lina nguvu za kujipanga yenye kudhibiti sio tu muundo wa kimuundo wa kikanisa, lakini pia mwendelezo na uwezo wa kuchangia kusaidia jamii ya Italia.”
Umuhimu wa maono ya mbali ya Mkataba
Askofu Mkuu Parra alisema kuwa umuhimu na juu ya maono yote ya mbali ya Mkataba wa Ikulu, haukuwa mdogo wa kurekebisha mkataba wa 1929 kwa mageuzi yaliyotolewa na uraia uliopo katika jamii ya Italia, ambayo ilikuwa na kupungua kwa nguvu ya mazoezi ya kidini nakwa kupunguza marejeeo ya kanuni na yaliyomo katika mafundisho ya Kikatoliki. Kiukweli, marekebisho ya suala zima la mashirika na mali ya kikanisa yalifafanuliwa kwa kuanzishwa kwa mfumo wa ufadhili wa Kanisa Katoliki kwa hiari na raia, kwa kile kinachoitwa “8 per mille,”yaani nane kwa elfu ambao ni mfuko wa hisani na hivyo kutambua kwamba sababu za mwamini lazima zihakikishwe na kamwe haziwezi kutenganishwa na zile za raia.”
Mabadiliko ya kijamii kiuchumi na kiutamaduni tangu 1948
Akikumbuka mabadiliko makubwa yaliyofanywa na jamii ya Italia katika kiwango cha udhibiti, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni tangu 1948 hadi leo hii, Askofu Mkuu Parra aliona jinsi ambavyo Kanisa lilivyojiweka na bado linajiweka kama marejeo ya upendeleo kwa watu walio katika shida, walioitwa kufanya kazi kwa ajili ya msaada huo muhimu ambao ni msingi wa mafundisho yake ya kijamii.” Kwa upande huo alisisitiza kuwa ni Kanisa mtaalamu katika ubinadamu ambalo Mtakatifu Paulo VI alizungumza, huko Askofu Mkuu Peña Parra akionya kwamba mtindo huu wa Utume
haupaswi kamwe kusababisha tamaa ya kuchukua nafasi ya taasisi za kiraia katika mipango na maelekezo ambayo siasa ya nchi inakuza na kutekeleza, lakini inapaswa kutafsiri katika roho ya kujenga ambayo huzaa matunda.”
Mfumo mpya wa CEI katika sekta ya ulinzi wa kiutamaduni wa kikanisa
Kwa kutolea mfano aliwaonesha wazi wa mfumo mpya wa kuunga mkono mapadre wa kishujaa wa Baraza la Maaskofu Italia ( CEI) na Mikoa katika sekta ya ulinzi wa urithi wa kiutamaduni wa kikanisa, wa mafundisho ya dini ya Kikatoliki katika shule za umma.” Kwa kuongezea alisema “hii inadhihirisha kwamba kuidhinishwa kwa Makubaliano ya Laterano hakukuwa na vikwazo kwa uhuru wa kidini, usawa bila ubaguzi wa dini na maendeleo ya jamii ya Italia katika maana ya kidini na ya tamaduni nyingi ambayo inaruhusu Kanisa kutekeleza kwa uhuru dhamira yake nchini Italia na ulimwenguni kote pia ikitoa michango madhubuti katika ukuaji wa jamii ya Italia.”