Cop28,Emilce Cuda:ni wakati wa kuanzisha njia ya haki ya kijamii&tabianchi
Na Marine Henriot na Alessandro Di Bussolo – Vatican
Kazi ya Mkutano mkubwa zaidi wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa wa COP28 huko Dubai, kuwahi kufanyika, inaendelea hadi tarehe 12 Desemba 2023. Baada ya hotuba na matamko ya Wakuu wa Nchi na Serikali katika siku chache za kwanza, sasa ni wakati wa mazungumzo ya kiufundi ili kufikia maandishi ya mwisho, ambayo lazima yapitishwe kwa kauli moja. Waraka uliotayarishwa na Uingereza na Singapore, ambao utakuwa msingi wa majadiliano kati ya wapatanishi katika muda wa majuma mawili yajayo, unasema nchi lazima ziandae “kupunguza/kutoka katika nishati ya mafuta.”Maandishi haya yatafafanua msimamo wa kisiasa kwa nchi 197, pamoja na Umoja wa Ulaya, waliotia saini Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC). Kiukweli, zaidi ya matangazo na mapendekezo yaliyotolewa na nchi mbalimbali, kwa mfano juu ya matumizi ya nishati ya nyuklia mara tatu au kuongeza kasi ya uondoaji wa makaa ya mawe, na hivyo maandishi ya mwisho tu ndiyo yenye mamlaka. Uchaguzi wa maneno katika maandishi haya ya mwisho ni muhimu na ni mada ya mazungumzo magumu yanayoendelea katika jiji kuu la Nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu.
“Tofauti kati ya kupunguza na kuondoa nishati ya mafuta ni ishara iliyotumwa, hasa katika soko na jumuiya pana ya biashara, ili kuonesha kwamba enzi ya mafuta inakaribia kuwa mwisho na kwamba tunahamia kwenye mfumo mpya wa nishati ambapo umuhimu zaidi utatolewa kwa ufanisi wa nishati na nishati mbadala hasa”. Alitoa maoni yake Lola Vallejo, mkurugenzi wa Mpango wa Tabianchi wa Taasisi ya Maendeleo ya kudumu na Ushirikiano kimataifa(Iddri - Institut du Développement Durable et des Relations Internationales). Nakala hiyo muhimu, ambayo inaweza kutumika katika hati ya matokeo ya COP28, kwa hakika ni tathmini ya kina ya makubaliano ya tabianchi ya Paris ya 2015. Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa mapema Septemba mwaka huu 2023, hatua zilizochukuliwa na Nchi mbalimbali hazitoshi kuzuia ongezeko la joto duniani hadi chini ya 2°C na, ikiwezekana, hadi 1.5°C ikilinganishwa na enzi ya kabla ya viwanda, ambayo ilikuwa mojawapo ya malengo yaliyowekwa katika COP21 huko Paris.
Kwa hiyo Emilce Cuda, katibu wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini, na profesa wa chuo kikuu katika Taalimungu ya Maadili na Jamii na mwandishi wa Argentina, pia alikuwepo katika Mkutano wa Dubai. Akizungumza kwenye jopo huko Dubai, alisisitiza jinsi wakati umefika kuanza mchakato wa mabadiliko ya haki, kama inavyofafanuliwa na Vatican, lakini pia na Umoja wa Mataifa”. Maneno ambayo mtaalam huyo aliyarejea tena katika vipaza sauti vya Radio Vatican - Vatican News, huku akisisitiza uharaka wa kuachana na mtindo wa uzalishaji viwandani unaoua, kama Papa Francisko alivyokumbusha. Huko Dubai nafasi tofauti zimewekwa mezani, lakini ni wakati wa kuanza njia ya haki ya kijamii kwa ardhi yetu," alisisitiza.
Mtazamo muhimu wa tatizo la kulinda mazingira asilia lakini pia ya kibinadamu ya fundisho la kijamii la Kanisa, lililozinduliwa tena na waraka wa Francisko wa Laudato Sì, unakubaliwa na washiriki katika Cop28, kulingana na Cuda, ambaye alifafanua ujumbe kwa video wa Papa kama ni muhimu sana kwa ajili ya uzinduzi wa Banda la Imani ndani ya Mkutano wa Wanachama hao wa Umoja wa Mataifa. "Papa alizungumzia amani, na hakuna mtu hapa anayeona mabadiliko ya tabianchi kama sehemu ya 'vita vya tatu vya dunia' - alisisitiza katibu wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini na badala yake ni vita vya teknolojia dhidi ya ubinadamu. Vita ambavyo havitoi kifo cha vurugu na mara moja, lakini kifo cha polepole japokuwa cha uhakika."