Dk.Ruffini:kuhifadhi thamani ya utu katika kazi ya huduma ya Kanisa
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Kutoa heshima kwa kazi ya huduma na ushirika na Kanisa na Papa, ndiyo yalikuwa mambo makuu matatu ambayo Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Ruffini, alisema wakati wa hafla ya kutunuku nishani za heshima kwa wafanyakazi ambao wamejipambanua katika taaluma zao katika shughuli zao za kawaida.
Heshima kwa huduma ya ushirika kwa Kanisa
Katika desturi ambayo inataka kwamba kila fursa ya Siku kuu ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano inayoadhimishwa kila mwaka mnamo tarehe 29 Septemba, ambayo ni sikukuu ya Malaika Wakuu Watakatifu Mikaeli, Gabrieli na Raphael, (ambapo Mtakatifu malaika Mkuu Gabrieli ndiye Somo wa Baraza,) iwe ishara ya sifa kwa kazi iliyofanywa na wanawake na wanaume walioajiriwa katika ngazi mbalimbali za muundo huo. Mwaka huu 2023, kutokana na kukaribia kwa Sinodi, tarehe ya sherehe hiyo haikufanyika siku hiyo na badala yake,iliahirishwa na ikafanyika tarehe 7 Desemba 2023 katika mkesha wa Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili. Siku hiyo ilianza na Misa Takatifu iliyoadhimishwa katika Kikanisa cha Jumba la Leone XIII iliyopo katika bustani ya Vatican na iliongozwa na Monsinyo Lucio Ruiz, Katibu wa Baraza hilo.
Ruffini: mashahuda wa ubinadamu wa kazi
Mara baada ya Misa Takatifu walioduhuria misa hiyo walihamia kwenye Chumba cha Bikira Maria Mpalizwa kwenye Jengo hilo hilo, tayari kwa kukabidhi tuzo hizo za heshima. Kabla ya kukabidhi, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Dk. Paolo Ruffini awali ya yotte alitoa shukrani zake za kibinafsi kwa kusisitiza thamani maalum ya jumuiya ya kazi ambayo kila mtu ana mwelekeo wa kusaidia kila mtu. “Sio utume rahisi, alikiri, ambapo aliongeza - “lazima tulinde maana ambayo ni huduma na ushirika, na wakati mwingine pia ni ngumu sana.” Dk. Ruffini alinukuu maneno ya Papa Francisko alipozungumzia juu ya Kanisa ambalo alisema: “halijijengi kwa misingi ya mpango wake lenyewe, na wala haliishi kwa kutegemea mikakati ya masoko bali lenyenyewe linaakisi mwanga wa Yesu ambao unashuhudia ubinadamu wa kazi inayoangazia nuru hiyo, si kwa wafanyabiashara bali na wale wanaomsaidia Mchungaji.” Akiendelea aaidha alikumbusha kwamba uwepo wa wengine lazima uwe na uzoefu kama zawadi na uwajibikaji.
Waliotunukiwa Heshima hizo
Utambuzi wa Heshima ya Juu ya Mtakatifu Silvestro ulitolewa kwa Si.ra Cinzia Marsicano (Katibu wa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano). Kutoka kitengo cha wahariri, wafuatao walipokea pongezi za Mtakatifu Silvestro Papa: Jean-Michel Coulet(Osservatore Romano, Timu ya Waariri wa Kifaransa), Adriana Masotti, (timu ya wahariri ya Italia). Padre Bernardo Suate (timu ya wahariri wa Kireno) ambaye alipokea heshima ya Msalaba(Croce pro Ecclesia et Pontifice. Kwa upande wa kitengo cha kiteknolojia, wakipokea Ushujaa wa Mtakatifu Silvestro Papa akuwa ni: Maurizio Corbo, Massimo Guerrini, Franco Orsini, Marcello Domenico Poli. Kurugenzi ya Masuala ya Jumla walitunukiwa: Roberto Valentini, Rita Colella (wa duka la vitabu la Mtakatifu Yohane Paulo II). Roberto Romolo (Mahusiano ya Kimataifa) alipokea heshima ya Mtakatifu Gregorio Magno. Kurugenzi ya Kitaalimungu - Kichungaji alikabidhiwa Felix Palacios Sanchez. Zaidi ya hayo, ilipokelewa Kibandiko cha Radio Vatican kwa Idhaa ya Kiskandinavia kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanza masafa yake ya matangazo.