Dubai-kujitolea kwa maendeleo ya mawasiliano na kuwezesha ufikiaji kwa wote
Vatican News
Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Radio (WRC-23) ulimalizika hivi karibuni ambao ulianzia tarehe 20 Novemba hadi 15 Desemba 2023 huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu, umewaona Wajumbe wakiongozwa na Katibu Mkuu Tawala wa Mji wa Vatican Sr. Raffaella Petrini na Katibu wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Monsinyo Lucio Adrian Ruiz kama katibu msaidizi mwakilishi wa Ujumbe wa Vatican katika Mkutano huo.
Thamani ya ubadilishanaji wa mawasiliano yasiyojua mipaka na umbali
Kwa njia hiyo Ujumbe wa Vatican ulithibitisha juu ya “thamani ya ubadilishanaji wa mawasiliano, ambayo hayajui umbali na kujibu hitaji la asili la watu binafsi la kuunda mawasiliano ya kibinadamu, kwa uangalifu maalum kwa maskini na wale ambao hawana njia za kutosha za kushiriki katika mazungumzo haya.” Waliokamilisha ujumbe wa Vatican ni Wakurugenzi na Viongozi wa miundo husika ya mji wa Vatican na pia wa Baraza la Mawasiliano: Mhandisi Antonino Intersimone, Mh.Luigi Salimbeni, Mhandisi Francesco Masci, Mhandisi Paolo Lazzarini na Bwana Sergio Salvatori.
Mikutano ya Kimataifa ya Mawasiliano ya Radio, inayoandaliwa na Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) kila baada ya miaka 4, ina mamlaka ya kurekebisha, katika sehemu zilizomo kwenye ajenda, Kanuni za Radio, ambazo zina hadhi ya Mkataba wa Kimataifa. Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 3,900 ambapo asilimia 22%walikuwa wakiwakilisha nchi 193, huku “wakifanya kazi kwa bidii kwa karibu siku 40 katika mfululizo wa makusanyiko ya jumla, mikutano ya nchi mbili, makongamano ya vyama, vikundi vya kazi na vikundi vya mafunzo na kuleta pamoja mchakato wa uamuzi mgumu.”
Sio rahisi utumiaji wa masafa na teknolojia zilizopo
Kulingana na ajenda ya mada zilizotazamiwa katika Mkutano huo, uchaguzi wa pamoja ulitambuliwa, sio rahisi kila wakati, katika utumiaji wa masafa na katika teknolojia zilizopo na zinazoibuka za radio, katika nyanja mbali mbali, kama radio na runinga, simu za mikononi, mifumo ya satelaiti, mifumo mingnie mengi zaidi, na kuhimiza maendeleo ya mawasiliano na kuboresha uwezekano wa upatikanaji hata kwa watu wasiojiweza.