Tafuta

2023.12.18 Jopo la waamuzi wa Tuzo ya Zayed kwa ajili ya Udugu wa Ubinadamu walikutana na Papa Francisko. 2023.12.18 Jopo la waamuzi wa Tuzo ya Zayed kwa ajili ya Udugu wa Ubinadamu walikutana na Papa Francisko.  (Vatican Media)

Jopo la Uamuzi wa Tuzo ya Zayed kutoka kwa Papa,Sandri:tunatafuta mifano halisi ya udugu

Jopo la majaji kwa toleo la 2024 lililoanzishwa mnamo 2019,baada ya kutiwa saini kwa Hati ya kihistoria huko Abu Dhabi kati ya Papa Francisko na Imamu Mkuu wa Al-Azhar Ahmed Al-Tayeb,limekutana na Papa tarehe 18 Desemba 2023.Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki,alizungumzia juu ya Jopo la Tuzo kuwa:“Mazungumzo ndiyo njia pekee ya kujenga ulimwengu bora.”

Vatica News

Hati, ile ya Udugu wa Kibinadamu, iliyotiwa saini karibu miaka mitano iliyopita huko Abu Dhabi na Papa Francisko na imamu mkuu wa Al-Azhar Ahmed Al-Tayeb, na Tuzo iliyofuata ya Zayed, ambayo iliunda hali mpya ya kiakili na harakati za ulimwengu kuhusu mazungumzo, udugu na ushirikiano kati ya dini na tamaduni mbalimbali ndiyo  Tuzo sasa inayotaka kuwa thabiti zaidi na kujulikana, lakini tayari kutoka katika uteuzi watu 40 uliowasilishwa mnamo 2019  ambao umekwenda kwa zaidi ya mia moja. Hivyo  ndivyo Mohammed Abdelsalam,wa Mistri ambaye ni  katibu mkuu wa  Jopola Uamuzi wa Tuzo ya Zayed kwa Udugu wa Kibinadamu, na Mwarabu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya  upapa na kuwasilisha Waraka wa kipapa wa Fratelli tutti, alikumbukasha muktadha  na matokeo ambayo  hati hiyo ya kihistoria, na tuzo iliyofuata, imekuwa katika ulimwengu wa leo. Alifanya hivyo katika meza ya duara iliyoandaliwa tarehe 18 Desemba 2023 na Vatican News - Radio Vatican, katika chumba cha mikutano cha Baraza la  Kipapa la Mawasiliano, na kusimamiwa na Sr. Bernadette Reis, wa uratibu wa uhariri wa vyombo vingi vya habari Vatican.

Waliokaa katika Meza ya Mduara waamuzi wa tuzo ya Zayed
Waliokaa katika Meza ya Mduara waamuzi wa tuzo ya Zayed

Wahusika wakuu walikuwa wajumbe wa Jopo la uamuzi wa toleo la 2024 la Tuzo, ambao walikuwa wamekutana  na Papa Francisko muda mfupi kabla ya kufanya  Meza ya Mduara huo. Rebeca Grynspan Mayufis, katibu mkuu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na maendeleo(Unctad), hakuwepo  kwa sababu ya kutoweza kushiriki, jopo la waamuzi lilikutana mjini Vatican kutathmini mapendekezo ya uteuzi huo, utakaotolewa tarehe 4 Februari 2024, katika kumbukumbu ya miaka mitano tangu kutiwa saini kwa Hati hiyo, sanjari na Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu iliyoanzishwa mnamo Desemba 2020 na Umoja wa Mataifa

Rais wa zamani wa Indonesia na waziri wa zamani wa Bulgaria 

Jopo la waamuzi  wa Tuzo ni  huru, linaloundwa na wataalam katika uwanja wa ujenzi wa amani na kuishi pamoja, kama vile Megawati Sukárnoputrì, rais wa zamani wa Indonesia (tangu 2001 hadi 2004) na mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo, na vile vile mwanamke wa kwanza kuongoza Serikali ya Uislamu wa Kisasa. Mnamo 2004 aliwekwa kwenye namba nane kwenye orodha ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi ulimwenguni iliyoandaliwa na jarida la Forbes. Sukárnoputrì alizungumzia na Papa tatizo la ongezeko la joto duniani na umuhimu wa upatikanaji wa elimu bora kwa vizazi vichanga, hasa wanawake, ambao lazima wapate fursa sawa kama wenzao wa kiume. Karibu naye  alikuwa ni Irina Bokova, Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Bulgaria na mwanamke wa kwanza na Mzungu wa kwanza kutoka kusini-mashariki kushikilia nafasi ya  kuwa mkurugenzi mkuu wa UNESCO kwa mihula miwili, na tangu 2020 ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Udugu wa Kibinadamu, iliyoanzisha kutoa uenezi na uthabiti kwa Hati ya Abu Dhabi.

Waamuzi wa Tuzo ya Zayed wakati wakikutana na Papa 18 Desemba
Waamuzi wa Tuzo ya Zayed wakati wakikutana na Papa 18 Desemba

Katika hafla hiyo alisema kuwa: “Hati hiyo inapaswa kuonekana kama hati ya kimsingi ya maadili ya wakati wetu, ambayo vijana wanaweza kupata majibu na ambayo inapatana na kipengele cha nne cha Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa kuhusu elimu.” Alipokutana tena na Papa Fransisko, alimfafanua kuwa “ana ubinadamu mkuu,” na akirejea kwenye mada ya elimu, huku akikumbuka kuwa mnamo 2015, katika Katekesi yake, Papa alifafanua elimu kama “sarufi ya mazungumzo ambayo misingi yake ni udadisi, kusikiliza na kuheshimu.”

Mkuu wa Kiyahudi Cooper: Papa, mtu wa shauku

Mkuu wa Kiyahudi Abraham Cooper, na rais wa Tume ya Marekani ya Uhuru wa Kidini wa Kimataifa, ambayo inafuatia ukiukwaji wa uhuru wa kidini katika nchi 28 duniani kote, alizungumza.  Kwa njia hiyo Cooper pia ni mkuu mshirika na mkurugenzi wa hatua za kijamii duniani katika Kituo cha Simon Wiesenthal, ambalo ni shirika kuu la haki za binadamu la Kiyahudi. Kwa upande wake alimfafanua Papa kuwa “mtu mwenye shauku, na hamu kubwa ya amani, ambaye anahimiza watu binafsi na watu kufanya mema.” Kwa vizazi vichanga, Mkuu wa Kiyahudi wa  Kiamerika alisisitiza, “lazima tufundishe kwamba maisha ni juu ya kufanya uchaguzi na kuwajibika, kuwasiliana nao pia kupitia mitandao ya kijamii, madaraja ya kuwafikia.”

Sr Bernadette akizungumza na waamuzi wa Tuzo ya Zayed 2024
Sr Bernadette akizungumza na waamuzi wa Tuzo ya Zayed 2024

Jaji Abdelsalam, akichochewa na msimamizi, pia alizungumzia mada ya mabadiliko ya tabianchi, akifafanua kuwa “changamoto kwa ubinadamu, na kwa sababu hii Kamati Kuu iliandaa mkutano kati ya viongozi wa kidini kabla ya COP28 huko Dubai. Kwa hiyo alisema, ni changamoto kwa kanuni za kuishi pamoja na maisha kwa amani na utangamano, kwa sababu mabadiliko ya hali ya hewa yanatishia maisha ya watu.” Alimnukuu Imamu mkuu  Al-Tayyeb alipokumbuka kuwa “unyonyaji huu ukiendelea hatutakuwa na mazingira tena kwa vizazi vijavyo”.

Sandri: kutoka kwa Papa ni  mwaliko wa kuendelea na mazungumzo

Hatimaye, alikuwa Kardinali Leonardo Sandri wa Italia na Argentina, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la kipapa la makanisa ya Mashariki ambaye alihudumu katika diplomasia nchini Madagascar, nchini Marekani kama mwakilishi wa Kipapa wa Shirika la Mataifa ya Marekani, huko Venezuela, na Mexico, alisisitiza hati ya Abu Dhabi, iliyotiwa saini,  ilikuwa ni ya kinambii na ambayo ilifungua njia mpya ya uelewa na mazungumzo. Mwishoni mwa meza ya duara alishirikisha maoni yake hata na  Vatican News  akielezea hisia zake kwa Mkutano na  Papa na kuhusu toleo la Tuzo  2024. Kwa mujibu wa Kardinali Leonardo sandri amesema kuwa Papa alisisitiza umuhimu wa Waraka wa Abu Dhabi juu ya udugu wa ulimwengu wote, juu ya mazungumzo ya amani na akakumbuka hali ya vita ambayo bado iko ulimwenguni baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mnamo 1945. Tumeishi miaka hii yote, hadi leo, na vita vilivyopandwa hapa na pale na ili kutatua drama ya ubinadamu katika vita, iliyogawanyika ndani ya nchi na baina ya nchi, tunahitaji kujenga ulimwengu wa amani na udugu. Ndiyo njia pekee ya kuweza kusema: “Tuishi kama ndugu katika dunia hii, tukisaidiana”. Kisha akasisitiza umuhimu wa kuendelea, kwa njia ya mazungumzo, kujenga ulimwengu huu bora.

Kardinali Sandri
Kardinali Sandri

Akishirikisha juu ya kuzungumzia umuhimu wa elimu, ili maadili yaliyomo katika Hati ya Udugu wa Kibinadamu pia yawafikie vizazi vichanga Kardinali Sandri alisema “Mmoja wa washiriki wa jJopo la uamuzi ni mkurugenzi mkuu wa zamani wa UNESCO na kwa hivyo Papa alisisitiza thamani hii ya elimu, ili ulimwengu wa vijana usiwe ulimwengu mtupu, usio na maadili, lakini wenye maadili haya ya mazungumzo na udugu na  kuwa na amatokeo chanya katika maisha yao ya kila siku. Ili wakue katika elimu hii ya amani, kwa sababu vinginevyo hakuna mustakabali wa ubinadamu unaoendelea na vita na migawanyiko. Kardinali ajibu swali la mwandishi kuhusu hali  ya kutisha ya mzozo kati ya Israeli na Hamas, katika nchi ambayo ni takatifu kwa dini tatu za Kiabrahamu, na kwamba ni ujumbe gani anaweza kutoka katika Tuzo la Zayed kwa Udugu wa Kibinadamu? Alisema kuwa “Kunaweza kuwa na mwito wa kuzingatiwa na Papa alirudia jambo hili pia katika mkutano wa leo. Wale wanaofaidika na vita hivi ni watengenezaji wa silaha tu. Zaidi ya yote, alikumbuka machozi, uchungu, uchungu, kukata tamaa kwa maisha ya vijana wengi ambayo yalipunguzwa katika vita hivi. Alikumbuka kutua huko Normandy, ambayo iliadhimishwa katika kumbukumbu ya miaka 75 mnamo 2019 na wakuu wote wa nchi, waliposherehekea kwenye mchanga wa fukwe hizo ambazo walizikwa waathirika wa vita.

Mkutano wa Papa na waamuzi wa Tuzo ya Zayed 2024
Mkutano wa Papa na waamuzi wa Tuzo ya Zayed 2024

Kardinali Sandri aidha alikumbuka ziara yake ya mwisho, mnamo Novemba 2, 2023 kwenye makaburi ya Wamarekani jijini  Roma ambapo aliadhimisha Misa na kutembea kati ya makaburi, kusoma majina  ya vijana wenye umri wa miaka 20 hadi 23, ambao wameona maisha yao yakikatishwa hapo hapo. Kwa njia hiyo Papa aliuliza kuwa “Ni nini maana ya hii? Ni mchango gani unaotolewa kwa ulimwengu kwa kifo, kwa chuki, kwa vita,  na kwa silaha? Na leo  hii akakumbuka kwamba alilia mbele ya makaburi haya.” Kardinali alisisitiza Kardinali Sandri vile vile  ameelezea juu ya uteuzi wa toleo hilo la tuzo kama kuna wagombe wengi wazuri waliojitokeza, na ni sifa gani wamezitafuta ndani mwao: “Kuna uteuzi mwingi na kuna mipango mingi, vitendo vya ajabu vinavyofanywa ulimwenguni ili kumwondolea mwanadamu maradhi, umaskini na udhalilishaji wa watu kutokana na biashara haramu ya binadamu. Juhudi nyingi zinakuja kwetu  ili kuwasilisha matokeo yao kuhusu masuala haya ya kuhuzunisha. Tunachotaka, angalau kwa upande wangu ni kupata mifano halisi ya maisha kati yao, kuwaambia vizazi vipya:”Tazama ikiwa unataka kuwa na maisha ambayo yana maana, ambayo sio tupu, bila tumaini, njia ni kuiga watu hawa na mashirika ambayo yanafanya mambo haya makubwa kwa ajili ya binadamu.”

Tuzo ya Zayed 2024
19 December 2023, 15:43