Tafuta

Papa na Makardinali washauri wake. Papa na Makardinali washauri wake. 

Kikao cha Makardinali 9 washauri wa Papa kufanyika mjini Vatican

Kuanzia Jumatatu 4 Desemba,Baraza la Makardinali(C9)litakutana kwa kikao cha mwisho cha 2023.Papa Francisko alikuwa ametangaza moja ya mada katikati ya tafakari na Makardinali kuwa ni ile ya nafasi ya wanawake katika Kanisa mnamo tarehe 30 Novemba 2023 akikutana na Tume ya Kimataifa ya Kitaalimungu.

Vatican News

Mkutano wa Baraza la Makardinali umeanza Jumatatu tarehe 4 Desemba 2023 mjini Vatican, mbele ya Baba Mtakatifu Francisko. Kama Papa alisvyokuwa amesema mnamo tarehe 30 Novemba 2023, wakati akikutana na Tume ya Kimataifa ya Kitaalimungu,kuwa kutakuwa na"tafakari juu ya mwelekeo wa kike katika  Kanisa."

Papa na Makadinali 9 washauri wake katika mkutano
Papa na Makadinali 9 washauri wake katika mkutano

Katika hotuba yake Papa Francisko alikuwa amesema akieleza kuwa" Kanisa ni la kike na moja ya dhambi kuu tulizokuwa nazo ni kulifanya kanisa kuwa la wanaume."  Alikuwa ameongeza kusema kuwa “tatizo, hata hivyo haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kihuduma lakini kwa njia ya fumbo na kwa njia ya kweli." Akipendekeza tofauti ya  kiBalthasari kati ya kanuni za Kipetro na Maria,kulingana na kwamba “Marian ni muhimu zaidi kuliko Petro,kwa sababu kuna Kanisa kama mchumba, Kanisa kama mwanamke",kwa hivyo alisisitiza hitaji la kugeuza  fikra za Kanisa.”

Baraza Makardinali 9

Mkutano wao wa mwisho wa  Makardinali 9 au C9 ulifanyika tarehe 26 na 27 Juni  2023 na kuwashuhudia Makardinali wakitafakari pamoja na Papa kuhusu masuala mbalimbali yakiwemo mgogoro unaoendelea nchini Ukraine,utekelezaji wa Katiba ya Kitume ya  Praedicate Evangelium yaani Hubirini Injili katika Makanisa mahalia,kazi ya Mkutano Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Watoto. Katikati,pia  ya majadiliano kulikuwapo na Mkutano wa Sinodi kuhusu mada ya sinodi iliyofanyika mjini Vatican kuanzia tarehe 4 hadi 29 Oktoba 2023.

Baraza la Makardinali, baada ya kupyaishwa muhimu wake mpya na Papa Francisko mnamo  tarehe 7 Machi 2023,limeunda kwa hiyo na makadinali:Pietro Parolin,katibu wa Vaticana;  Kardinali Fernando Vérgez Alzaga,Rais wa Tume ya Kipapa ya Mji wa Vatican na Mkuu tawala wa Vatican; Kardinali Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Kkuu wa Kinshasa(DRC); Kardinali Oswald Gracias,Askofu Mkuu wa Bombay; Kardinali Seán Patrick O'Malley,Askofu Mkuu wa Boston; Kardinalo Juan José Omella Omella,Askofu Mkuu wa Barcelona; Kardinali Gérald Lacroix,Askofu Mkuu wa Quebec; Kardinali Jean-Claude Hollerich,Askofu Mkuu wa Luxembourg; Kardinali Sérgio da Rocha,Askofu mkuu wa San Salvador de Bahia. Katibu ni AskofuMarco Mellino,wa Jimbo la Cresima. Mkutano wa kwanza wa Baraza  Jipya la Makardinali Washauri wa Papa 9 (C9) ulifanyika mnamo tarehe 24 Aprili 2023.

Kuanzishwa kwa Baraza la Makardinali

Ikumbukwe kwamba Baraza la Makardinali lilianzishwa na Baba Mtakatifu  Francisko na Hati yake ya Mkono  mnamo tarehe 8 Septemba 2013 kwa ajili ya jukumu la kumsaidia katika uongozi wa Kanisa la Ulimwengu na kusoma pamoja mpango wa marekebisho ya Curia Romana,ambapo mwisho wake ulitekelezwa na Katiba mpya ya Kitume iitwayo Praedicate Evangelium iliyochapishwa mnamo tarehe 19 Machi 2022. Na Mkutano wa kwanza kabisa  wa Baraza hilo la Makardinali 9 washauri wa Papa ulifanyika mnamo tarehe Mosi Oktoba 2013.

KIKAO CHA BARAZA LA MAKARDINALI WASHAURI WA PAPA
04 December 2023, 15:01