Wakati wa Papa alipomtembelea Papa Benedikito XVI Wakati wa Papa alipomtembelea Papa Benedikito XVI  (Vatican Media)

Maisha,mawazo na urithi wa Benedikto XVI baada ya mwaka 1 wa kifo chake

Siku mbili za kutafakari ushawishi wake juu ya Kanisa na jamii baada ya mwaka mmoja wa kifo chake,ambapo wasomi,wataalamu na marafiki wa Hayati Baba Mtakatifu Benedikto XVI watakusanyika tarehe 30 na 31 Desemba.Tarehe 31 Desemba saa 2.00 asuhuhi katika Altare ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Askofu Mkuu Gänswein ataongoza Ibada ya Misa Takatifu ya kumbukumbu kifo

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Ukumbi wa Benedikto XVI, huko Campo Santo, mjini Vatican, mikutano miwili inafanyika kwa siku mbili ya tarehe 30 na 31 Desemba 2023 kwa ajili ya kutafakari maisha, mafundisho  na urithi wa Papa Benedikto XVI, baada ya mwaka mmoja tangu kifo chake kilichotokea tarehe 31 Desemba 2022. Walioandaa Mkutano huo ni Shirika la habari la EWTN, kwa ushirikiano wa Fundatio Christiana Virtus, yaani Mfuko wa Fadhila za kikristo na Mfuko wa Vatican wa Joseph Ratzinger-Benedikto XVI. Kwa njia hiyo ni siku mbili za kina katika kutafakari ushawishi wake juu ya Kanisa na jamii baada ya mwaka mmoja wa kifo chake, ambapo wasomi, wataalamu na marafiki wa Hayati Baba Mtakatifu wamekusanyika. Mpango huo unatazamia mikutano mitatu yenye mada tofauti.

Papa akibariki jeneza la Papa Mstaafu Benedikto XVI tarehe 5 Januari 2023
Papa akibariki jeneza la Papa Mstaafu Benedikto XVI tarehe 5 Januari 2023

Asubuhi ya Jumamosi tarehe 30 Desemba 2023, waliofungua mkutano huo ni Profesa Vincent Twomey na Padre  Federico Lombardi, ambaye ni Rais wa Mfuko wa Joseph Ratsinger -Benedikto XVI waliozungumzia juu ya mada: “Benedikto XVI, Kumbu kumbu na urithi”, wakati saa tano asubuhi, Kardinali Gerhard Ludwig Müller na Profesa Matthew Bunson walikabiliana na mada kuhusu: “kitovu cha Taalimungu ya Benedikto XVI: Yesu Kristo”, na hatimaye siku itahitimishwa alasiti na mada: “Kifo cha Benedikto XVI katika mwanga wa maisha ya milele” kwa kuratibiwa na Kardinali Kurt Koch na Profesa  Ralph Weimann.

Ni mwaka mmoja sasa tangu kifo cha Papa Benedikto XVI
Ni mwaka mmoja sasa tangu kifo cha Papa Benedikto XVI

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tovuti ya Mfuko wa Joseph Ratzinger - Benedikto XVI wanabainisha kuwa ratiba ya Dominika tarehe 31 Desemba 2023 saa 2.00 asuhuhi itaanzia katika Altare ya kiti cha Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Askofu Mkuu Georg Gänswein ambaye ataongoza Ibada ya Misa Takatifu ya kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kifo cha Papa mstaafu Benedikto XVI. Baada ya misa hiyo saa 4 asubuhi anatarajia kutoa tafakari kuhusu miaka ya mwisho ya maisha yaPapa Benedikto XVI na urithi wake, katika majengo ya Campo Santo Teutonico yaani ya majengo yaliyoko kwenye Makaburi ya Vatican. Kwa melezo zaidi inaweza kubonyeza hapa: http://www.fondazioneratzinger.va/content/fondazioneratzinger/it/news.html

 

30 December 2023, 13:32