Tafuta

2023.12.21 Mji wa Osaka. 2023.12.21 Mji wa Osaka. 

Vatican itashiriki EXPO ya Osaka kunako 2025

Maonesho ya Kimataifa ya mada:"Kubuni Jumuiya ya Wakati Ujao kwa Maisha Yetu,"itafanyika nchini Japan kuanzia tarehe 13 Aprili hadi 3 Oktoba 2025.Vatica itashiriki kwenye hafla hiyo,shukrani kwa ushirikiano na Jumba la Kiitaliano na nafasi ya sanaa na utamaduni inayoitwa:"Uzuri huleta Matumaini".Askofu Mkuu Fisichella kamishna mkuu:"Mwanadamu bado anahitaji kutumaini."

Vatican News

Kupitia maonesho, usanifu wa kisanii na mitazamo ya kipekee, Banda la Vatican litatoa tafakari ya jinsi uzuri unavyoweza kuwa kichocheo cha matumaini, kuwaunganisha watu kwenye njia kuelekea mustakabali wa pamoja wa upyaisho wa kiroho. Zaidi ya hayo, mada inaingiliana na ile ya Jubilei 2025, yenye mada “Mahujaji wa Matumaini,” wakicheza jukumu la daraja linalounganisha matukio hayo mawili. “Mtu wa leo anaishi akiwa na matumaini mengi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, lakini, kama ilivyoelezwa tayari kwa mada ya Jubilei na ile ya EXPO pia inataka kuwasilisha umuhimu wa Tumaini, katika umoja, unaotoka kwa Mungu pekee. Mwanadamu bado anahitaji kutumaini alisisitiza Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la  Uinjilishaji – Kitengo cha  Masuala  Msingi ya Uinjilishaji Ulimwenguni. Maonesho ya Kimataifa ya  2025 yatafanyika Osaka, nchini Japan kuanzia tarehe 13 Aprili 2025 hadi 13 Oktoba 2025. Mada iliyochaguliwa kwa toleo hilo ni: “Kubuni Jumuiya ya Baadaye kwa Maisha Yetu,na  yenye mada ndogo tatu tofauti: “Kuokoa Maisha”, “Kuwezesha Maisha,” na “Kuunganisha Maisha.” Vatican, kutokana na ushirikiano na Jumba la Kiitaliano, itakuwepo kwenye hafla hiyo na nafasi inayotambulika ya kuandaa hafla za kiutamaduni ambayo Askofu Mkuu Fisichella kamishna mkuu alifafanua.

Makamishna wa Banda la Vatican la EXPO 2025 huko Osaka

Askofu Mkuu Rino Fisichella, aliyeteuliwa na Papa kuandaa na kutunza ushiriki rasmi wa EXPO la Banda  katika EXPO ijayo 2025 Osaka, Nchini  Japan, kama kamishna mkuu, aliyeteuliwa kuwa na manaibu makamishna wa hafla hiyo Monsinyo Pietro Bongiovanni, paroko wa Mtakatifu Salvatore huko Lauro na Padre Nuno Alexandre Henriques De Lima, paroko wa Kanisa Katoliki la Tamatsukuri, Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria la Osaka. Nchini Japan. Kwa njia hiyo Kamishna Mkuu Fisichella, ana imani katika msaada wao kusaidia na kuwakilisha Vatican katika maandalizi na kwa muda wa tukio zima anabainisha katika taarifa yake.

Banda lenye mada  ya Uzuri huleta Matumaini

Kaulimbiu ya Banda la Vatican itakuwa “Uzuri huleta Matumaini.” Kupitia uchunguzi wa sanaa na uzuri Banda linalenga kuwasilisha dhana ya kina kwamba uzuri katika nyanja nyingi, unaweza kuwa chanzo cha msukumo na matumaini ya ujenzi wa jamii zaidi ya baadaye yenye usawa na shirikishi. Uzuri daima umekuwa na jukumu la msingi katika uinjilishaji wa Kikristo, ukijifanya kuwa mwili tangu asili ya Ukristo katika kujieleza kwa kisanii. Kwa karne nyingi, sanaa imekuwa njia ya upendeleo ambayo kwayo Kanisa limeweza kueleza na kuwakilisha kina cha imani. "Via Pulchritudinis" ilikuwa chombo cha ufanisi zaidi cha kuwasiliana kwa dhahiri moyo wa imani kupitia uzuri wenyewe.” Imeeleza taarifa kwa vyombo vya habari,

Tafakari katika mtazamo wa Jubilei

Kupitia maonesho, usanifu wa kisanii na mitazamo ya kipekee, Banda la Vatican  litatoa tafakari ya jinsi uzuri unavyoweza kuwa kichocheo cha Matumaini, kuwaunganisha watu kwenye njia kuelekea mustakabali wa pamoja wa upyaisho wa kiroho. Zaidi ya hayo, mada inaingiliana na ile ya Jubilei 2025, yenye mada “Mahujaji wa Matumaini”, zikijikita zote mbili katika jukumu la daraja linalounganisha na kuunganisha matukio hayo mawili. “Mtu wa leo hii anaishi akiwa na matumaini mengi kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, alisisitiza Askofu Mkuu Fisichella. “Lakini, kama ilivyoelezwa tayari kwa mada ya Jubilei,  na ile ya EXPO pia inataka kuwasilisha umuhimu wa Tumaini, katika umoja, unaotoka kwa Mungu pekee. Mwanadamu bado anahitaji kutumaini.”

22 December 2023, 11:00