Tafuta

2023.12.17 Papa amefikisha miaka 87 na watoto wa kituo cha Zahanati ya Mtakatifu Marta wamemfanyia sherehe. 2023.12.17 Papa amefikisha miaka 87 na watoto wa kituo cha Zahanati ya Mtakatifu Marta wamemfanyia sherehe.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa ameadhimisha miaka 87 ya kuzaliwa na Watoto wa Zahanati ya Mtakatifu Marta

Kama ilivyo sherehe ya kila mwaka,Dominika 17 Desemba 2023 familia zinazohudumiwa na Zahanati ya Kipapa wamempokea Papa katika Ukumbi wa Paulo VI kusheherekea miaka 87 ya kuzaliwa."Sisi tunapaswa kujiandalia siku kuu kubwa ambayo itakuwa juma lijalo,Noeli,Siku kuu ambayo sisi tunafikiria na tunakumbuka wakati Yesu alikuja.Alikuja kukaa na sisi.”

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Katika Dominika ya tatu ya Majilio, tarehe 17 Desemba 2023, ikiwa ni sambamba na siku ya kuzaliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi na mapema, imeandaliwa sherehe katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican na Kituo cha Afya cha Mtakatifu Marta( Dispensario Santa Marta. Ni Zahanati ya  Vatican ambayo kwa zaidi ya karne, kila siku inatoa msaada wa mama na  watoto wenye matatizo na kuhudumiwa na watu wa kujitolea, madaktari na wasio madaktari.

Miaka 87 ya Papa Francisko 17 Desemba 2023

Baba Mtakatifu akiwa katika ukumbi amewasalimia wote kwamba: “Ninawashukuru sana kuwaona ninyi…. Watoto wa kike na kiume hapa. Asante sana. Sisi tunapaswa kujiandalia siku kuu kubwa ambayo itakuwa juma lijalo, Noeli, Siku kuu ambayo sisi tunafikiria na tunakumbuka wakati Yesu alikuja. Alikuja kukaa na sisi. Tufikiri, tujiandae moyo wa Noeli, ili kumpokea Yesu.” Baba Mtakatifu akiendelea amesema kuwa: “Kila mmoja afikiri: Je nitamwomba Yesu nini? Nitamuomba nini Yesu katika Noeli hii. Sasa kila mmoja wenu afikiri kwamba: nitamomba Yesu nini? - kwa ukimya.” Papa ameongeza kusema: “Kwa macho yaliyofungwa, na mfikiri: nitamwomba nini Yesu. Mmefikiria tayari? Sawa. Mtaomba baadaye. Na niniwatakia Noeli Njema! Noeli Njema kwenu nyote! Na daima kwa tabasamu na Bwana awapatie kile mnachotaka. Asante!” Amehitimisha.

Circus ndogo ya watoto katika ukumbi wa Paulo VI
Circus ndogo ya watoto katika ukumbi wa Paulo VI

Zilikuwa ni zaidi ya familia 200 ambao wamempokea Baba Mtakatifu kwa hali ya furaha wakati wa kufika kwake mnamo saa 4.00. Kulikuwa na nyimbo na michezo ya watoto, na kwa hiyo onesho la (Circus), yaani Sarakasi kwao, baadaye vitafunwa na  keki kabla ya sala ya Malaika wa Bwana. Lakini juu ya yote ilikuwa ni kupeana mikono, tabasamu na kukumbatiana. Watoto hao walipokea zawadi zilizotolewa na wafadhili wa Zahanati kwa kuzingatia sikukuu ya Noeli inayokaribia.

Akiwa kama Babu yao Papa na watoto
Akiwa kama Babu yao Papa na watoto

Huu ni utamaduni ulioanza mnamo Desemba 2013, wakati wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Papa  Francisko baada ya kuchaguliwa katika kiti cha Kharifa wa Mtume Petro. Mwaka 2022 kulikuwapo hata familia za Ukraine (L’anno scorso erano presenti anche alcune famiglie ucraine)zilizokaribishwa mjini Roma. Baba alikuwa ametualika t"usiwasahau watoto wa Ukraine na wale wanaoteseka kutokana na ukosefu wa haki mahali pengine."

Mikumbatio kwa Papa
Mikumbatio kwa Papa

Zahanati hiyo iliyotamaniwa na Papa Pio XI, mnamo 1922 imekabidhiwa kwa Watawa wa Shirika la Mtakatifu Vincent wa Pauli. Anayeongozwa kwa sasa ni Sr. Anna Luisa Rizzello. Na rais wa Zahanati hiyo ni Kadinali KonradKrajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo.

Watoto wa Zahanati ya Kipapa wamshangilia Papa katika siku yake ya kuzaliwa 17 Desemba

 

17 December 2023, 11:37