Tafuta

2024.01.29 Askofu Mkuu  Edgar Peña Parra aliadhimisha misa huko Nicosia (Cyprus, 28 Januari 2024) 2024.01.29 Askofu Mkuu Edgar Peña Parra aliadhimisha misa huko Nicosia (Cyprus, 28 Januari 2024) 

Ask.Mkuu Peña Parra:tusijitoe katika ulimwengu uliogawanyika

Katibu Msaidizi wa Vatican ambaye amekuwa Cyprus kwa siku chache kwa ajili ya uzinduzi wa Ubalozi wa Batican,aliadhimisha hata Misa katika Kanisa la Msalaba Mtakatifu huko Nicosia Dominika tarehe 28 Januari 2024.“Yesu ndiye Mwalimu wa kweli anayejua kuongea na moyo na maisha ya kila mtu."

Osservatore Romano

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, naibu wa Sekretarieti ya Vatican alihubiri kwa waamini wa Jumuiya ya Kikatoliki ya Cyprus waliohudhuria misa iliyoadhimishwa katika Kanisa la Msalaba Mtakatifu huko Nicosia Dominika asubuhi  tarehe 28 Januari 2024 na kusema kuwa: “Ninyi ni ishara ya umoja katika utofauti, wa ushirika katika wingi, wa maelewano katika tofauti.”  Askofu Mkuu Parra, ambaye siku ya Ijumaa tarehe 26 alizindua Ubalozi wa Vatican, katika mji mkuu wa Nchi hiyo katika kuadhimisha miaka hamsini ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Cyprus na Vatican, katika mahubiri yake ya  Dominika ya 4 ya Mwaka B wa Kanisa alikumbuka mwaliko wa “kutojiuzulu wenyewe kwa ulimwengu uliogawanyika kama maneno yaliyotamkwa na Papa Francisko katika hekalu hilo wakati wa ziara yake kisiwani hivi karibuni.”

Askofu Mkuu Edigar Katibu Msaidizi wa Vatican wakati wa misa huko Nocoscia Cyprus
Askofu Mkuu Edigar Katibu Msaidizi wa Vatican wakati wa misa huko Nocoscia Cyprus

Akitoa salamu za Papa, ambaye alikaa hapo tarehe 2 na 3 Desemba 2021, Askofu Mkuu Peña Parra alitoa maoni juu ya usomaji huo, akisisitiza jinsi liturujia inavyotoa “maandiko muhimu sana kwa maisha yetu kama Wakristo.” Ya kwanza, kiukweli, iliyochukuliwa kutoka katika kitabu cha Kumbukumbu la Torati (18, 15-20), iliripoti ahadi aliyopewa Musa ambayo Bwana anajitolea kuendelea kuwa karibu na wanadamu, kukaa daima katika ushirika pamoja nao, ambayo inaonekana kwa ujumla: “Kwa sababu katika Kristo Aliye Juu zaidi sio tu anakuwa karibu nasi, lakini anakuwa mtu kama sisi, mdogo kati ya wadogo, mnyenyekevu kati ya wanyenyekevu. Anafanya hivyo ili kupunguza umbali, kuvunja vizuizi na kufundisha njia ya ushirika na umoja.”

Katibu Msaidizi wa Vatican akitoa baraka baada ya Misa huko Nikosia Cyprus
Katibu Msaidizi wa Vatican akitoa baraka baada ya Misa huko Nikosia Cyprus

Vivyo hivyo na kifungu cha Injili kutoka Marko 1, 21-28, kilichojikita juu ya mji wa Kapernaumu,  ambao ulikuwa ni mji wa kibiashara na makutano ya watu, katika eneo la Galilaya, eneo lililodharauliwa na la kando. Askofu Mkuu alisema kuwa “Hapa tunamwona Yesu akiingia kwa siri katika sinagogi la jiji, Mgalilaya kati ya Wagalilaya, kusikiliza Maandiko na kuomba pamoja na watu hawa wanyenyekevu, waliodharauliwa kwa sababu wanachukuliwa, na Wayahudi wachamungu wa Yerusalemu, viumbe duni, wasiostahili hata  kidogo,  na silo watiifu  na wakamilifu. Badala yake, Askofu mkuu alisema kuwa, Kristo, kama alivyokuwa amefanya huko Yordani (Mk 1, 9-11), anawakaribia kwa unyenyekevu, anabisha hodi kwenye mlango wao na kuomba kukaribishwa mahali pao pa kusali. Naye anazungumza nao, akifundisha kwa mamlaka na upendo.”

Akizingatia kipengele hicho cha mwisho, Katibu Msaidizi wa Vatican aliakisi jinsi ambavyo “katika maisha ya kila siku tunaweza kujikuta tunakabiliwa na mitazamo au vishawishi fulani vya kujirejea: kuhisi uhakika wa kujua kila kitu, labda kulingana na maoni yanayotolewa na televisheni, vyombo vya habari, mtandao.” Vijana hasa, alisema, “linapokuja suala la ulimwengu wa kidijitali na teknolojia, wao ni werevu zaidi kuliko watu wazima, wazazi na walimu, na hii inaweza kusababisha hali ya kujitosheleza na wakati huo huo hali ya kuwa duni kwa sehemu ya wale ambao ni wazee.” Wakati “Injili inaonesha kwamba Yesu anafundisha kwa mamlaka kwa sababu anajua Ukweli: ukweli kuhusu maisha, ukweli kuhusu Mungu, ukweli kuhusu mwanadamu, hisia halisi ya ukweli.”

Katibu msaizidi wa Vatican wakati wa kuzindua Ubalozi wa Kitume huko Cyprus 26  Januari 2024
Katibu msaizidi wa Vatican wakati wa kuzindua Ubalozi wa Kitume huko Cyprus 26 Januari 2024

Zaidi ya hayo, Askofu Mkuu aliongeza, kusema kuwa “Yesu anaishi kwanza ya yote anayofundisha, sikuzote na mfululizo. Anapozungumza, anafanya hivyo bila maslahi binafsi; kinachong'aa ni upendo wake, huruma yake kwa watu binafsi na kwa umati. Anajiweka kikamilifu katika utumishi wao na anaonyesha nguvu ya upendo wake katika kukutana na wagonjwa, waliopagawa, wenye dhambi. Hii ndiyo sababu Katibu Msaidizi  huyo alisema, “Yesu ndiye Mwalimu wa kweli anayejua kuongea na moyo na maisha ya kila mtu. Anaona matatizo yao halisi; yeye ndiye Mchungaji Mwema anayewaongoza kwenye njia ya haki.”

Kwa hiyo, aliendelea  kuwa Askofu Mkuu Peña Parra, “katika haya yote, ni upendo ambao hushinda kwa kubomoa kuta mbili zinazoonekana kuwa haziwezi kuzuilika. Mtu husimikwa na kiburi na majivuno ya wale wanaojiona kuwa bora kuliko wengine na kuwaweka kando. Nyingine polepole hujitokeza ndani ya moyo wa mtu, kwa shukrani kwa roho ya hila ya jeuri na chuki ambayo, ikiwa haitatambuliwa kwa wakati na kupingwa, hujiweka pale hadi kufikia hatua ya kuficha kila dalili ya ubinadamu. Upendo ndio unaoshinda: huu ndio ujumbe ambao Yesu anatufundisha, ili sisi, kwa upande wetu, tuendelee kuutangaza. Hivyo basi mawaidha kwa Wakatoliki wa kisiwa hicho - yenye alama ya mgawanyiko wa uchungu wa ukuta unaoonekana kutoka kwa kanisa ambapo Papa Francisko alikutana na wahamiaji waliokaribishwa huko  Cyprus - kuwa “ishara ya umoja katika utofauti. Kuwa kwako hapo pamoja  ni sauti inayorudia kwa kila mmoja, na kwetu sote, maneno hayo mazuri, yaliyojaa matumaini: “Tazama, mimi ni kaka yako, dada yako. Je, hunitambui?”

30 January 2024, 16:46