2024.01.09 Askofu Mkuu Fisichella akionesha begi lililotengenezwa kwa ajili ya Mhujaji katika Jubilei ya 2025 atakaye kuja Roma. 2024.01.09 Askofu Mkuu Fisichella akionesha begi lililotengenezwa kwa ajili ya Mhujaji katika Jubilei ya 2025 atakaye kuja Roma. 

Jubilei 2025:Utengenezaji wa Begi rasmi wa Hija

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji,kitengo cha masuala msingi ya Uinjilishaji ulimwenguni na lenye jukumu la kuandaa Jubilei ya 2025, limeamua kwa mara ya kwanza wakati wa tukio muhimu kwa Kanisa bidhaa ya Begi rasmi ya Hija iliyoundwa kwa ajili ya wale wote watakaoamua kuanza hija kuja Roma.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

“Mhujaji anayejiandaa kwa ajili ya Jubilei ya 2025 anajua vyema kwamba kutembea ni uwezo wa kujua jinsi ya kuondoa na kuacha nyumbani uzito wa ziada ili kuwa na uwezo wa kubeba tu kile kinachohitajika kwa ajili ya uzoefu wake binafasi  wa imani na kutafakari.” Kwa sababu hiyo, Baraza la Uinjilishaji, Kitengo cha masuala ya msingi ya uinjilishaji ulimwenguni, na lenye jukumu la kuandaa Jubilei ijayo ya kawaida ya mwaka Mtakatifu  2025, limeamua, “kwa mara ya kwanza wakati wa tukio muhimu kama hilo kwa Kanisa, kutoa bidhaa iliyoundwa na iliyoundwa kwa wale wote wanaoamua kuanza  safari yao  ya hija kuja Roma kuwa na “ Begi rasmi wa Hija. Baada ya kuchunguza mipango mbalimbali, uchaguzi wa Baraza hili  uliangukia kwenye dhana iliyoundwa na kampuni ya Roma ya Stegip4.  

Begi ya mhujaji  wa matumiani kwa mwaka 2025
Begi ya mhujaji wa matumiani kwa mwaka 2025

Kwa njia hiyo  Mkuu wa Baraza la Kipapa la unjilishaji alikuwa na la kusema kuwa:  “Nilikubali kwa hiari mapendekezo ya baadhi ya makampuni ya Italia na ya kigeni kwa ajili ya utengenezaji na uuzaji wa begi rasmi la mahujaji kwa ajili ya  Jubilei ijayo mwaka wa 2025. “Ninajua vizuri jinsi ambavyo begi  linavyoweza kuwa muhimu wakati wa Hija na jinsi lilivyo muhimu kuhifadhi, na ishara za wakati na kuvaa, kama shuhuda  aliyejaa kumbukumbu za siku hizo za sala na tafakari, iliyojaa hisia na kwa hivyo isiyoweza kusahaulika.”, alitoa maoni yake  Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, kitengo cha masuala Msingi ya Uinjilishaji katika kuwasilisha uamuzi wa kuipatia Kampuni ya Stegip4 kutengeneza Begi rasmi za mahujaji.” Begi ambalo litauzwa hivi karibuni, na vifaa vyote vinavyounda seti nzima ya Hija(kofia ya ukingo pana, skafu, chupa ya maji na rozari ya mkononi), vyote vilitengenezwa kwa njia bora na endelevu.

Kituo cha maelezo kuhusu Jubilei 2025 kilichopo njia ya Conciliazione
Kituo cha maelezo kuhusu Jubilei 2025 kilichopo njia ya Conciliazione

“Lengo letu ni kupendekeza bidhaa iliyoundwa kwa ajili ya Jubilei rafiki kwa mazingira, yenye uwezo wa kutoa maoni chanya kutoka kwa vizazi vipya na mahujaji ambao tayari wameshiriki katika Jubilei au mahujaji wengine na ambao wanajua umuhimu wa kuwa na begi nyumba kila wakati,” alisema hayo Stefano D'Ambrosio, Mkurugenzi Mtendaji wa Stegip4. Kwa njia hiyo, pia Gino Conversi, mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Stegip4, akimshukuru Askofu Mkuu Fisichella kwa uaminifu aliopewa, aliongeza kusema kuwa: “Chaguo la Baraza la Kipapa la Uinjilishaji ni chaguo ambalo linatufanya tujivunie na ambalo huwakilisha umakini mkubwa wa Kampuni ya  Stegip4, kwa viwango vya ubora wa juu na kwa heshima kwa mfumo wa ikolojia. Hii ndiyo sababu tumeunda bidhaa inayochanganya ubunifu, biashara ya kimaadili na athari ya chini ya mazingira.” Kwa kuongezea alisisitiza kwamba: “Kupitia begi la mahujaji tulitaka kusema kauli mbiu ya Jubilei 'Peregrinantes in Spem', yaani Mhujaji wa Matumaini  kama mwaliko wa kujenga upya hali ya matumaini na uaminifu ili kuangalia vyema siku zijazo. Mustakabali wa kuzaliwa upya, ambao kila mtu lazima awajibike na kuubeba mabegani mwao, kama begi la kuweka kile ambacho ni muhimu kweli.”

Begi la mhujaji kwa Jubilei 2025
12 January 2024, 15:04