Majimbo ya Kilwa-Kisenga na Wamba DRC wamepata maaskofu wapya
Vatican News.
Jumamatano, tarehe 17 Januari 2024 Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa Padre Désiré Lenge Mukwenye, kuwa Askofu Mpya wa Jimbo katoliki la Kilwa-Kasenga Congo (DRC), hadi uteuzi huo alikuwa ni Msimamizi wa Jimbo hilo la Mzunguko wa Kikanisa.
Wasifu wake
Mheshimiwa Padre Désiré Lenge Mukwenye alizaliwa tarehe 2 Machi 1966 huko Lwanza. Alisomea Falsafa na Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu -Paul huko Kambikila, Lubumbashi. Baada ya mwaka mmoja katika Parokia ya Mtakatifu Andrea huko Kilwa, tarehe 31 Julai 1994 alipewa Daraja Takatifu ya Upadre.
Alishika nyadhifa zifuatazo na kuendelea na masomo zaidi: Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga huko Lupembe (1994-1998); Mwendesha Mashtaka wa Jimbo la Lubumbashi (1998-2002); mratibu wa Mtakatofu Maria Tumaini , Jimbo la Roma (2003-2008); Alihitimu masomo ya Biblia katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana Roma (2003-2008); Msihikiri wa Kanisa la Mamaria Mkingiwa dhambi ya Asisi la Roho Mtakatifu huko Torre Annunziata, Jimbo kuu la Napolis (2008-2011); Alipata Leseni Mafunzo ya Kiroho ya Biblia katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana (2008-2010); utafiti wa udaktari huko Münster, Ujerumani (2011-2012); Mwalimu na Mkurugenzi wa Kiroho katika Seminari ya Mtakatifu Paulo huko Lubumbashi (2013-2016); Shahada ya Uzamivu wa Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana (2016); Makamu Askofu Jimbo la Kilwa-Kasenga (2018-2021). Na tangu 2016 alikuwa ni Gambira wa Chuo Kikuu cha Kiteknolojia cha Katumba Mwanke na Profesa wa Seminari ya Lubumbashi na 2021, Amministratore Diocesano di Kilwa-Kasenga.
Askofu Mpya Jimbo la Wamba
Baba Mtakatifu Francisko Jumatano tarehe 17 Januari 2024 alikubali kujiuzulu kutoka katika huduma ya kichungaji ya Jimbo la Wamba (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) iliyotolewa na Askofu Janvier Kataka Luvete lkwa kufikia umri wake. Na wakati huo huo Baba Mtakatifu akamteua kuwa Askofu wa Jimbo hilo Wamba (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) Mheshimiwa Padre Emmanuel Ngona Ngotsi, M.Afr, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni mkuu wa Kanda wa Wamisionari wa Afrika – Kanda ya Afrika ya Kati.
Wasifu wake
Mweshimiwa Padre Emmanuel Ngona Ngotsi alizaliwa tarehe 1 Januari 1960 huko Bambu-Mines, katika Jimbo la Bunia (Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo). Alifunda katika mafunzo ya Falsafa huko Migodi ya Bambu, na, baada ya uzoefu wa mafunzo kazini huko Burkina Faso, aliendelea na Taalimungu katika Taasisi Katoliki ya Toulouse nchini Ufaransa. Baada ya kujiunga na Wamisionari wa Afrika huko Bambu-Mines, alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 22 Agosti 1990 huko Fataki, Bunia.
Nyadhifa nyingine
Alishika nyadhifa zifuatazo na kuendelea na masomo zaidi: Paroko Parokia (1990-1994) na kisha Paroko (1994-1996) huko Birni N'koni nchini Niger; Alihitimu masomo ya Sayansi Jamii katika Taasisi Katoliki ya Paris, Ufaransa (1996-1999); Paroko wa parokia ya Zinder nchini Niger (1999-2004); Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirika jijini Roma (2004); Msaidizi wa Mkuu wa Kanda ya Wamisionari huko Ouagadougou nchini Burkina Faso (2005-2008); Mkuu wa Kitengo cha Falsafa ya Mpadre wamisionari wa Afrika huko Ouagadougou (2008-2009); Mkuu wa Kanda ya Bukavu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (2009-2010); Mjumbe wa Baraza Kuu la Wamisionari wa Afrika huko Roma (2010-2016). Tangu 2017 amekuwa Mkuu wa Kanda wa Wamisionari wa Afrika huko Bukavu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ni mjumbe wa Baraza la Mapadre na Baraza la Washauri wa Jimbo Kuu la Bukavu