Tafuta

Kanisa la Myanmar Kanisa la Myanmar 

Mwenyeheri Paolo Manna:katika kumbukizi kutakuwa na sala na tafakari ya kimisionari

Katika fursa ya kuzaliwa kwa Mwenyeheri Padre Polo Manna,Mwanzilishi wa PUM,Chuo Cha Kipapa Urbaniano kimeandaa sala na tafakari tarehe 14 Januari 2024 katika Chuo Kikuu hicho kwa ajili ya kusikiliza ushuhuda na urithi wa kiroho wa kimisionariwa mmisionari huyo.Alikwenda umisionari huko Birmania(Myanmar).

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Dominika tarehe 14 Januari 2023, Chuo Kikuu cha Kipapa la Urabaniano kimependekeza tena ushuhuda na urithi wa kiroho na kimisionari wa Mwenyeheri Paolo Manna, Mwanzilishi wa Chama cha Umoja wa Kipapa wa Kimisionari(PUM). Katika hafla ya kumbukumbu yake kiliturujia ambapo  inakumbusha kuzaliwa kwake  (16/01/1872),ambayo itaadhimishwa Jumanne ijayo, Umoja wa Kipapa wa Kimisionari (PUM) pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Uhuishaji wa Kimisionari (CIAM) na Chuo cha Kipapa cha Urbaniana, wameandaa  jioni  moja kutoa muda wa   sala na tafakari kuanzia saa 12:30 jioni kwa  kuanza na masifu ya Pili ya Dominika  na baadaye saa 1.00 jioni  kufuatia  meza ya mduara  ambayo itajikita na mada: “Mwenyeheri Paolo Manna na mambo ya sasa ya uhuishaji na malezi ya kimisionari katika nyakati za Evangelii Gaudium.”

Watoa mada

Watoa mada katika meza ya mduara ni pamoja na Padre Vito del Prete (PIME), Padre wa kiroho wa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Paulo, Padre Armando Nugnes, Mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Urbaniana, Padre Dinh Anh Nhue Nguyen, (OFMconv), Katibu Mkuu wa PUM.  Dominika hiyo pia itakuwa fursa ya kuzama  kwa kina katika safari ya kibinadamu na kiroho ya Mwenyeheri Manna, nafsi yake ya kimisionari ya kitume ambayo alipata kukabiliana na nyakati nyingi za giza. “Kwa upande wa Mwenyeheri Paolo Manna ni mchakato wa uongofu unaoendelea, wa Mkristo na mmisionari. Safari hii haikuwa bila mateso, majaribu, migogoro, lakini wale wanaomwamini na kujikabidhi kwa Bwana daima wataibuka wenye nguvu, wapya zaidi katika Roho, zaidi kwa Mungu,” alifafanua  hayo Katibu Mkuu wa PUM.

Padre Manna huko Birmania kwa utume wa kimisionari

Akiwa na umri wa miaka 22, Padre Paolo Manna, baada tu ya kuwekwa  wakfu alikwenda Birmania (sasa ambayo ni Myanmar), ambako alipanda “mbegu” za Injili kati ya kabila la Ghekú; lakini aliugua na kulazimika kurudi nchini Italia. Katika miaka 12 ya kazi ya umisionari alirudi Italia mara tatu kwa sababu kubwa za kiafya; alikaa huko mara ya mwisho mnamo 1907, kwa majuto makubwa. Na “mwaka 1907 Padre Manna alijieleza kuwa “mmisionari aliyeshindwa;” Katika umri wa miaka 35, kiukweli, alirudi kutoka Birmania kuja Italia kwa mara ya tatu, kwa sababu kubwa za afya ambapo (alikuwa na TB yaani Kifua kikuu). Alikuwa na ndoto ya utume kati ya wasio Wakristo na ikamkataa. Ni moja wapo ya nyakati muhimu za maisha yake: katika taasisi ya umisionari hapakuwa na nafasi tena (wakati huo wazee na wagonjwa walirudi majimbo walimokuwa wamelazwa), kama tunasoma katika maandishi ya Padre Piero Gheddo kuwa: “Kutafakari kwa vitendo, iliyosimamiwa na PUM.  

Januari 23,2024,Misa kwa mapadre,Taasisi ya Kipapa ya Mt.Paulo

Katika msimu wa kiangazi wa 1908, Padre Paolo alikwenda Lourdes, kwa Bikira, ambaye alikuwa amejitolea sana kwa ibada yake, hakuuliza uponyaji wa mwili au hata kuona wazi katika maisha yake ya baadaye. Yeye aliomba kuwa katika upendo na Yesu na Maria, kwa utakatifu na usafi kwa ajili yake mwenyewe, wokovu wa milele kwa ajili yake na wapendwa wake wote. Kuhusu mustakabali wake kama “mmisionari aliyeshindwa”, aliajiachia mwenyewe kwa Maongozi ya Mungu. Padre Manna hawezi kuelewekaisipokuwa kuanzia katika imani yake kamilifu, isiyoweza kufutwa, iliyomwilishwa na sala ya kina: ubora wa msingi wa maisha yake ulikuwa utakatifu, ambao ulimfanya awe mtulivu na mwenye furaha katika majaribu na mateso mengi aliyopitia. Kwa hakika uwongofu wa Paolo Manna na ule wa Mtakatifu Paulo utakuwa katikati ya wakati mwingine wa sala iliyoandaliwa na PUM mnamo Jumanne tarehe 23 Januari 2024 pamoja na Misa na mahubiri ya kimisionari kwa mapadre wa Taasisi ya kipapa ya Mtakatifu Paolo.

13 January 2024, 14:29