Tafuta

Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. 

Mwitikio kwa“Fiducia supplicans:”taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Ujumbe kwa vyombo vya habari uliotiwa saini na Kardinali,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzau ya Kanisa na katibu wake:Fundisho la ndoa halibadiliki,maaskofu wanaweza kufanya mang’amuzi kulingana na mazingira,baraka za kichungaji hazilinganishwi na zile za kiliturujia na ibada.

VATICAN NEWS

Uchapishaji wa tamko la fundisho la Fiducia supplicans juu ya maana ya baraka ya Kichungaji ya tarehe 18 Desemba 2023 mara moja ulichochea hisia tofauti kutoka kwa maaskofu binafsi na kutoka katika mabaraza mazima ya Maaskofu. Majuma mawili baadaye Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Kardinali Víctor Manuel Fernández na Katibu wake, Monsinyo Armando Matteo, wamerejea kwenye mada na taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari asubuhi ya tarehe 4 Januari 2024. Kwa mujibu wa marejeo hayo wanabainisha kuwa:“Matamshi ya kueleweka ya baadhi ya Mabaraza ya Maaskofu yana thamani ya kuakisi haja ya tafakari ya kichungaji ya muda mrefu. Kinachooneshwa na Mabaraza haya ya Maaskofu hakiwezi kufasiriwa kama upinzani wa kimafundisho, kwa sababu hati hiyo iko wazi na ya kawaida juu ya ndoa na ujinsia. Kuna sentensi kadhaa kali katika Tamko ambazo haziachi shaka.”

Katika taarifa hiyo inaorodhesha vifungu vyote visivyo na shaka vya hati ambayo ni wazi kwamba Fundisho la ndoa halibadiliki na kwa Kanisa Katoliki ni uhusiano kati ya mwanamume na mwanamke ndani ya ndoa tu ndio halali (Wasilisho, aya ya 4, 5 na 11). Kwa hiyo wanabainisha katika vyombo vya habari kuwa: “Ni dhahiri kusingekuwa na nafasi ya kujitenga wenyewe kwa mafundisho kutoka katika Tamko hili au kuliona kuwa la uzushi, kinyume na Mapokeo ya Kanisa au kufuru.”  Nakala ya hati, kama inavyojulikana, inafungua uwezekano wa kutoa baraka fupi na rahisi za kichungaji tu (si za kiliturujia au za ibada) watu washio pamoja wasio wa kawaida(sio wa muungano wao), “ikisisitiza kwamba hizi ni baraka zisizo na muundo wa kiliturujia ambazo haziidhinishi wala hazikubali kuhalalisha hali ambayo watu hawa wanajikuta nayo.”

Mwenyekiti na Katibu wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, wanatambua kwamba hati zinazofanana “zinaweza kuhitaji, katika nyanja zao za vitendo, muda zaidi au kidogo kwa matumizi yao kulingana na mazingira  mahalia na mang’amuzi ya kila Askofu wa Jimbo na Jimbo lake. Katika sehemu zingine hakuna ugumu wa matumizi ya kuanza haraka, kwa nyingine kuna hitaji la kutobuni kitu chochote huku wakichukua muda wote muhimu ili kusoma na kutafsiri.” Kila Askofu mahalia kiukweli, daima ana nguvu ya “upambanuzi kwenye eneo lake”, yaani, katika sehemu hiyo halisi ambayo anaijua zaidi kuliko wengine kwa sababu ni kundi lake. Busara na umakini katika muktadha wa kikanisa na tamaduni za wenyeji vinaweza kuruhusu mbinu tofauti za matumizi, lakini si ukanusho kamili au dhahiri wa njia hii ambayo inapendekezwa kwa makuhani.”

Kuhusu misimamo inayochukuliwa na Mabaraza mazima ya Maaskofu, ni lazima ieleweke katika muktadha wake: “Katika nchi kadhaa – kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari inakubali kuwa - "kuna masuala yenye nguvu za kiutamaduni na hata ya kisheria ambazo zinahitaji muda na mikakati ya kichungaji ambayo inakwenda zaidi ya muda mfupi. Ikiwa kuna sheria zinazolaani na kifungo, katika visa vingine kwa mateso na hata kifo kwa kitendo tu cha kujitangaza kuwa shoga, ni wazi kwamba baraka haitakuwa ya busara. Ni wazi kwamba Maaskofu hawataki kuwaweka watu wazi, wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kwenye vurugu. Inabakia kuwa muhimu kwamba Mabaraza ya Maaskofu hayaungi mkono fundisho tofauti na lile la Tamko lililotiwa saini na kuidhinishwa na Papa, kwani ndilo fundisho kama siku zote, bali wapendekeze hitaji la kusoma na mang’amuzi ili kutenda kwa busara ya kichungaji katika muktadha kama huo.”

Katika taarifa ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa  inasisitiza juu ya “upya wa kweli” wa Fiducia supplicans, ambao “unahitaji jitihada za ukarimu za mapokezi na ambayo hakuna mtu anayepaswa kujitangaza kuwa ametengwa, sio uwezekano wa kubariki wanandoa wasio wa kawaida. Ni mwaliko wa kutofautisha kati ya aina mbili tofauti za baraka: “liturujia au ibada” na “zile za papo kwa hapo au kichungaji.” “Tafakari ya kitaalimungu, inayojikita katika maono ya kichungaji ya Papa Francisko, inaashiria maendeleo ya kweli ikilinganishwa na yale ambayo yamesemwa kuhusu baraka katika Majisterio na maandiko rasmi ya Kanisa.” Kwa sababu hiyo, Kardinali Fernandez na Monsinyo Matteo, wanaeleza kuwa “maandiko ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa yamechukua hadhi ya juu ya “Tamko”, ambalo linawakilisha zaidi ya jibu au barua.

Mada kuu, ambayo hasa inatualika kwa namna ya pekee ya kuimarisha utendaji wetu wa kichungaji, ni uelewa mpana wa baraka na pendekezo la kuongeza baraka za kichungaji, ambazo hazihitaji masharti sawa na baraka katika muktadha wa kiliturujia au ibada. Kwa hivyo, zaidi ya mabishano, maandishi yanahitaji juhudi ya kutafakari kwa utulivu, kwa moyo wa wachungaji, bila itikadi yoyote.” Kila mtu ameombwa akue katika imani kwamba,“baraka zisizo na ibada sio za kuwekwa wakfu kwa mtu au wawili wanaozipokea, sio uhalalisho wa matendo yao yote, sio uthibitisho wa maisha wanayoishi.”

Taarifa hiyo basi inaendelea kutoa mfano rahisi wa baraka ya haraka isiyo ya kiibada na wala rasmi. Baraka hizi za “kichungaji” lazima “zaidi ya yote ziwe fupi sana (taz n. 28). Hizi ni baraka zinazodumu kwa sekunde chache, bila ibada na bila baraka. Iwapo watu wawili wanakaribia pamoja ili kusali, wanamwomba Mungu amani, afya na vitu vingine kwa ajili ya watu hawo wawili wanaoomba. Wakati huo huo wanaomba kama wanaweza kuishi Injili ya Kristo kwa uaminifu kamili na kwamba Roho Mtakatifu anaweza kuwaweka huru watu hawa wawili kutoka katika kila kitu kisicholingana na mapenzi yake Mungu na katika kila kitu kinachohitaji utakaso.

Aina hii ya baraka isiyo na ibada, pamoja na urahisi na ufupi wa umbo lake, hauhitaji kuhalalisha kitu ambacho hakikubaliki kimaadili. Ni wazi kwamba sio ndoa, lakini  pia sio “kibali” au uthibitisho wa chochote . Ni jibu la mchungaji pekee kwa watu wawili wanaoomba msaada wa Mungu. Kwa hiyo, katika kesi hii, mchungaji haweki masharti na hataki kujua maisha ya karibu ya watu hao.” Kwa hivyo, kila Askofu katika jimbo lake ana mamlaka ya kuanzisha aina hii ya baraka rahisi “kwa mapendekezo yote ya busara na uangalifu, lakini kwa njia yoyote hana mamlaka ya kupendekeza au kuanzisha baraka ambazo zinaweza kufanana na ibada ya kiliturujia.”

Wakati “katika sehemu zingine, labda, katekesi itahitajika, ambayo isaidie kila mtu kuelewa  ya kwamba aina hii ya baraka sio uthibitisho wa maisha yanayoongozwa na wale wanaoziomba. Kwa njia hiyo ishara hizi ni mbali na kuwa sakramenti au ibada. Ni maneno rahisi ya ukaribu wa kichungaji ambayo hayaleti mahitaji sawa na sakramenti au ibada rasmi." Soma zaidi:https://www.vaticannews.va/en/vatican-city/news/2024-01/dicastery-for-the-doctrine-of-the-faith-on-fiducia-supplicans.html

04 January 2024, 12:36