Kard.Filoni,Yerusalemu:Kanisa linatualika kuacha vurugu,chuki haitoki kwa Mungu
Vatican News
Ilikuonesha ukaribu wao kwa Nchi Takatifu kwa niaba ya washiriki wote wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu la Yerusalemu, viongozi walikwenda hija ya amani katika Nchi Takatifu kuanzia tarehe 28 Desemba 2023 na watahitimisha tarehe 3 Januari 2024. Kardinali Fernando Filoni, Mkuu wa Shirika la Ulinzi wa Kaburi Takatifu Yerusalemu yuko pamoja na Gavana Mkuu, Balozi Leonardo Visconti di Modrone na François Vayne, Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika siku hizi huko Yerusalemu kwa ajili ya mshikamano na ukaribu na Kanisa mahalia kama ishara ya wasiwasi na kujali, kwa mujibu wa taarifa kuhusu ziara hiyo.
Ishara ya msaada kwa Upatriaki wa Yerusalemu
Kwa niaba ya Shirika hilo, barua inaarifu, kuwa wanawasilisha kwa ujumla kama "ishara thabiti ya kuunga mkono Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, ambao ni ukweli wa kikanisa unawakilishwa na Shirika hilo na kuitwa kusaidia kwa sheria". Kwa njia hiyo tarehe 1 Januari 2024 siku ambayo inaadhimisha Siku ya Amani Duniani, wanaomba amani katika nchi hii inayoteswa.”Tarehe Mosi Januari 2024 pia Kardinali Filoni aliadhimisha Ibada ya Misa Takatifu ya Maadhimisho ya Bikira Maria Mama wa Mungu iliyoongozwa na Patriaki Pierbattista Pizzaballa katika Kanisa kuu la Upatriaki wa Kilatini huko Yerusalemu. Katika maadhimisho hayo, mara baada ya misa hiyo, Kardinali alitaka kuchangia baadhi ya tafakari zake, kwanza kabisa kuhusu kaulimbiu ya amani, “zawadi ya Mungu na mema ya msingi ambayo kila mmoja ameitwa kuitafuta na kuitetea kwa ujasiri. Hatuwezi kujiuzulu wenyewe kwa vurugu," alisema Kardinali Filoni, huku akiwahakikishia waamini wote waliohudhuria Misa ya "mshikamano na ukaribu" wa mashujaa na wanawake wa Kaburi Takatifu ambao wanasindikiza naye kwa sala kwenye "hija hii ya amani". Kardinali Filoni akiendelea alisema: "Katika nyakati ngumu kama hizi kwa Nchi Takatifu na kwa Kanisa zima ambalo lina Nyumba Mama yake hapa, ningependa kwaeleza kwa upendo na wasiwasi gani mashujaa wetu wote na wanawake wanaofuatilia matukio ya kushangaza ambayo yamewapata watu wa Israel na watu wa Palestina” kwa kuongeza ni watu wote ambao wanabeba mateso ambayo hayajawahi kutokea".
Sala ya amani
Kwa upande wake, “Kanisa linataka kuwa chombo cha amani na maelewano, huku likiwaalika kila mtu, kwa njia ya maombi ya dhati ya Baba Mtakatifu Francisko na Maaskofu wa dunia, kuachana na vurugu, tamaa na kutafuta njia ya kuishi pamoja kwa heshima wale wanaoishi katika Nchi hii ambayo Ufunuo wa Mungu kwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu ulianzia. Chuki si ya Mungu.” Kwa kuhitimisha kwa sala kwa Maria alisema: "baada ya kumshika Mtoto mchanga mikononi mwake, aliweza kushikana na kushikilia kwa magoti yake Nchi Takatifu, ambayo alikuwa binti mteule. Kwako, Mama, tunaikabidhi Nchi hii, inayopendwa na Bwana, ili iweze kufungua mioyo na akili za wale wanaohusika na amani na maelewano ya Watu."