Tafuta

2024.01.19  Papa amekutana na Bwana Gustavo Petro,Rais wa Jamhuri ya Colombia 2024.01.19 Papa amekutana na Bwana Gustavo Petro,Rais wa Jamhuri ya Colombia  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amekutana na Rais wa Colombia,Gustavo Francisco Petro Urrego

Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Colombia Bwana Gustavo Francisco Petro Urrego, ambaye baadaye amekutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa

Vatican News

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 19 Januari 2024 amekutana katika Jumba la Kitume mjini Vatican na Rais wa Jamhuri ya Colombia, Bwana Gustavo Francisco Petro Urrego, ambaye baadaye amekutana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa

Papa Francisko na  na Rais wa Colombia
Papa Francisko na na Rais wa Colombia

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari Vatican imebanisha kuwa wakati wa mazungumzo yao, na Sekretarieti ya Vatican, wameonesha kupendezwa uwepo wa mahusiano mema kati ya Colombia na Vatican, kwa kusisitiza ushirikiano chanya kati ya kanisa na Serikali kwa mtazamo wa uhamashishaji wa mazungumzo, wa haki kijamii na mapatano. Wakiendelea na mazungumzo yao, wamejikita juu ya hali halisi ya kijamii- kisiasa, na matukio ya uhamiaji na juu ya ulinzi wa mazingira katika Kanda.

 

19 January 2024, 17:07