Papa amemteuwa Padre Abel Liluala kuwa Askofu Mkuu wa Ponte-Noire
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 6 Januari 2024 amepoka barua ya kuomba kung’atuka katika shughuli za Kichungahji za Jimbo Kuu la Pointe-Noire, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC)iliyowakilishwa na Askofu Mkuu Miguel Ángel Olaverri Arroniz, S.D.B. na wakati huo huo akamteua Askofu Mkuu wa Jimbo kuu hilo hilo Mheshimiwa sana,Padre Abel Liluala, ambaye hadi uteuzi wake alikuwa Paroko wa Kanisa Kuu na Makamu Hakimu wa Jimbo Kuu la Pointe-Noire.
Wasifu wa maisha
Askofu Mkuu Mteule Abel Liluala, alizaliwa 23 Aprili 1964 huko Cabinda, Angola, karibu na Pointe-Noire. Baada ya Seminari Ndogo ya Tshela, katika Jimbo la Boma, alipata mafunzo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mtakatifu André Kaggwa huko Kinshasa DRC. Alisoma Taalimungu katika Seminari Kuu ya Moyo Mtakatifu huko Luanda, Angola na baadaye katika Seminari Kuu ya Emile Biayenda huko Brazzaville.
Alipewa daraja la Upadre tarehe 6 Februari 1994 kwa Jimbo kuu la Pointe-Noire. Mwaka 2010 alipata shahada ya udaktari katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu(Santa Croce) jijini Roma. Pia alikuwa mwanachama wa Chuo cha Washauri cha Pointe-Noire. Hadi uteuzi huo kwa hiyo alikuwa ni Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Mtume na Makamu katika Mahakama ya Jimbo Kuu la Pointe-Noire.