Papa ametuma salamu za rambi rambi kufuatia na maporomoko ya ardhi nchini Colombia
Vatican News
Katika telegramu iliyoelekezwa kwa Askofu Mario Álvarez Gómez, Papa Francisco anatoa maombi yake kwa ajili ya mapumziko ya milele ya marehemu, kwa wale ambao wanajishughulisha na utafutaji wa waliopotea na wale walioathiriwa na janga hilo la asili ambalo hadi sasa limesababisha vifo vya baadhi ya watu 36, huku wengine 7 bado hawajapatikana.
“Nimehuzunishwa sana na msiba wa asili ambao umeathiri eneo la Chocó nchini Kolombia na kusababisha waaathirika wengi na uharibifu wa mali.” Hii ndio hisia ya Papa Francisko baada ya kusikia habari za maporomoko ya ardhi yaliyotokea siku ya Ijumaa tarehe 12 Januari 2024 kwenye barabara karibu na mji wa El Carmen de Atrato, huko Chocó (magharibi), ambayo yamesababisha vifo vya takriban 36 na watu 7 bado hawajapatika.
Akikabidhiwa salamu hizo kwa Askofu Mario de Jesús Álvarez Gómez, msimamizi wa kitume wa Jimbo la Quibdó, katika telegramu iliyotiwa saini na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, anabainisha kuwa “Baba Mtakatifu anatoa sala zake za dhati kwa ajili ya mapumziko ya milele ya marehemu. Papa pia anatoa sala zake kwa Bwana ili faraja kwa waliofiwa na wale wote wanaoteseka katika nyakati hizi za uchungu na kutokuwa na uhakika. Kwa njia hiyo hiyo, Papa Francisko anaomba uungwaji mkono kwa wale ambao wamejitolea kutafuta waliopotea.” Baba Mtakatifu Francisko akimwomba Bikira Maria kuwaombea kwa mwanae Yesu Kristo kwa ajili ya wote waliofikwa na janga hilo, amewapatia kwa upendo baraka za kitume zenye kufariji, kama ishara ya ukaribu wake wa kiroho,”zinahitimishwa salamu hizo kutoka kwa Baba Mtakatifu.
Gustavo Petro, Rais wa Cocombia, alitangaza maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika mji wa Idara ya Chocó kuwa janga la asili, ili kuharakisha uhamisho wa rasilimali kwenye eneo hilo. Katika taarifa baada ya kutembelea eneno hilo, Rais Petro alihakikisha kwamba atahamisha takriban dola milioni 128 kwa Wakala wa Kitaifa wa Miundombinu na taasisi inayosimamia barabara, Taasisi ya Kitaifa ya Barabara Kuu. Maporomoko yalifunika magari kadhaa ambayo yalisimamishwa, na mlima uliporomoka ambao hapo awali ulifunga barabara kuu kati ya Medellín na Quibdó, mji mkuu wa Chocó. Walakini, idadi kubwa ya waathirika ilitokea katika nyumba, ambapo karibu watu mia moja walikuwa wamejificha wakingojea hali mbaya ya hewa ipungue na kuanza tena safari yao salama.