Vatican,mafungo ya kiroho ya Kwaresima 2024 ni ya kibinafsi
Vatican News
Kipindi cha mapumziko kwa ajili ya sala na maombi, kama ilivyo desturi, katika Kipindi kikuu cha Kwaresima. Kwa mara nyingine tena, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imeripoti tarehe 16 Januari 2024 kuwa Papa Francisko anawaalika Makardinali wakazi wa Roma, wakuu wa Mabaraza ya kipapa na wakuu wa Kanisa kuu la Roma kuishi katika mwanzo wa awamu hii ya mwaka wa kiliturujia kwa njia ya kibinafsi, katika kipindi cha mafungo ya kiroho tangu alasiri ya Dominika tarehe 18 Februari hadi alasiri ya siku ya Ijumaa tarehe 23 Februari 2024.
Shughuli za kipapa kwa juma la mafungo ya kiroho kibinafsi zinasitishwa
Katika Juma hilo kwa maelezo yanabainisha, kwamba shughuli zote za Papa zitasitishwa ikiwa ni pamoja na Katekesi ya Jumatano tarehe 21 Februari 2024. Kwa hiyo mwaka huu pia, kama ilivyotokea tangu kuzuka kwa janga la uviko mnamo 2020, mtindo wa kibinafsi wa mafungo ya Kwaresima unarudiwa tena, tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma na tangu mwanzo wa upapa, na mafungo ya kiroho yaliyofanywa kwa Jumuiya nzima na Papa na washiriki wake kutoka Curia Romana huko Ariccia, katika nyumba ya Divin Maestro inayosimamiwa na Watawa wa Mtakatifu Paulo ( Pauline).