Papa ateua Mratibu wa Siku ya Watoto duniani&Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kanisa kuu la Mt.Petro
Vatican News.
Katika kuelekea Siku ya I ya Watoto Duniani, Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 19 Januari 2024 amememteua Mratibu na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kanisa Kuu la Kipapa la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Padre Enzo Fortunato, (O.F.M. Conv.,) ambaye alikuwa tayari ni msemamji Mkuu wa Ofisi ya Vyombo vya habari wa Konventi Takatifu ya Assisi (Italia).
Ikumbukwea kuwa baada ya Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 8 Desemba 2023 katika Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, Baba Mtakatifu alitangaza kuwa litafanyika Toleo la kwanza la Siku ya Watoto duniani, tarehe 25 na 26 Mei 2024 kwa mpango huo uliofadhiliwa na Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Kama Yesu tunataka kuweka watoto katikati.” Baba Mtakatifu Francisko alisema kuwa: “Mpango huo unajibu swali: ni ulimwengu wa aina gani tunataka kuwapa watoto wanaokua? Kama Yesu tunataka kuweka watoto katikati na kuwatunza.