Radio Vatican:kuanzia tarehe 8 Januari,masafa mbashara katika Facebook
Vatican news
Kila siku kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa masafa ya Papa yanafungua kamera zake na kutangaza kwenye Facebook katika sehemu ya kipindi cha asubuhi kiitwacho: 'Radio Vaticana con voi', yaani 'Radio Vatican na ninyi,' kinachotangazwa kwa Kiitaliano kuanzia saa 2.10 hadi 4.00. asubuhi. "Ni jaribio la kwanza kwa mtazamo wa Jubilei inayokuja. Tutatumia Ukurasa wa Facebook: vaticannews.it. Na dhamira yetu ni kuleta Habari Njema kwa ulimwengu na ukweli wa mitandao ya kijamii unaendelea kututia changamoto.”
Hayo ni maoni yaliyotolewa na Massimiliano Menichetti, Mhusika Mkuu wa Radio Vatican, Vatican News. Kwa mujibu wa maelezo yake kuhusu mbashara wa habari Vatican news alisema: “Tunajiweka katika huduma kwa wale ambao wanatafuta habari za Vatican, Kanisa na Ulimwengu, kwa shauku ya kusali na sisi, au kwa urahisi tu kusikiliza muziki mzuri, mfumo wa sauti shirikishi, video, maandishi, picha zinazojumuish lugha hamsini na moja. Papa Francisko anatusukuma ili 'tutoke nje' na hii inatutia moyo tusijifikirie kama watangazaji walio na umbali kati ya mmoja hadi mwingine badala yake, wa kuwa karibu, kwa mazungumzo na kutomwacha kamwe mtu yeyote peke yake.
“Radio Vaticana con Voi” kwa hiyo ni tukio la kila juma lenye nguvu sana, ambapo wanahabari watapata nafasi za kila siku kutoka Vatican, wageni na bila shaka wale wote wanaotusikiliza na ambao hadi sasa wameweza kutuma ujumbe kwa njia ya WhatsApp kupitia namba: +39 335 124 3722.
Na kwa hiyo kuanzia tarehe 8 Januari 2024, baada ya habari za kimataifa za saa 2.00 kamili, ni kuanza jaribio hili la kwanza la video: kamera zimefunguliwa saa 2.18, lakini hata hivyo wakati hautakuwa sawa kwani kupitia njia za kijamii tutatoa muda wa siku itakayofuata. Kwa kifupi ni jaribio la kweli, ambalo likitoa matokeo yanayotarajiwa tutapanua hadi programu nyingine katika ratiba ya Kiitaliano na kwa lugha nyinginezo, bila kuondoa uwezekano wa pia kukaa katika nafasi ya televisheni ya dunia ya kidijitali.” Alisisitiza Mhusika wa Radio Vatican, Vatican News.