Wanawake wa Kipalestina katika mazishi ya wanafamilia zao. Wanawake wa Kipalestina katika mazishi ya wanafamilia zao.  Tahariri

Siku 100 na ukaribu na anayeteseka

Hatuko upande wowote.Tuko upande wa Wapalestina wengi waliokufa chini ya vifusi vya Gaza,kati yao ni watoto 10,000.Tunasimama pamoja na watu wasio na hatia waliouawa kinyama huko kibbutzim tarehe 7 Oktoba.Tunasimama kwa uthabiti upande mmoja wa wale waathiriwa na wanaoteseka.

Andrea Tornielli

Kukumbuka wakati uliopita tangu mkasa uliotokea ni wa kusikitisha sana. Kukumbuka hilo wakati mkasa bado unaendelea ni mbaya sana. Tangu Oktoba 7, wanaume, wanawake na watoto 136 wameshikiliwa mateka na Hamas katika andaki za chini ya Gaza. Hakuna kinachojulikana juu yao na hali zao. Leo hii tunachapisha mchango wa kusisimua wa Rachel Goldberg Polin, uliojaa maumivu lakini pia wa upendo. Hakuna kilichojulikana kuhusu mwanawe Hersh, 23, tangu asubuhi hiyo ya kusikitisha, isipokuwa labda kupoteza mkono.

Tuko karibu na Rachel, si kwa sababu ya mateso yake tu yenye heshima, bali zaidi ya yote kwa yale anayosema na kuandika. Kwa ufahamu wake wa ujasiri kwamba hata upande wa pili wa uzio, kuna akina mama kama yeye ambao wanateseka. Na wengi wanaomboleza watoto waliowapoteza. Sauti yake ya ujasiri, katika muktadha ambapo hasira na kisasi hutawala, inaweza kuonekana kuwa peke yake. Lakini si hivyo. Ni kwa kutambua uchungu wa wengine tu, pamoja na wa mtu mwenyewe, kunaweza kuwa na utulivu na msamaha.


Maneno ya Racheli ni yetu pia. Ni yale ya Papa Francisko ambaye anatualika kwa “usawa.” Ukaribu wa wale wanaoteseka, kwa wale wanaokufa, kwa wale ambao wameachwa bila chochote. Ukaribu huu kwa wagonjwa wa pande zote mbili mara nyingi hufasiriwa kama usawa. Hatuna upande wowote katika vita hivi. Tunasimama, kwa usadikisho kamili, upande mmoja, ule wa waathrika, wanaoteseka. Tuko upande wa watu elfu 22 waliokufa chini ya vifusi vya Gaza, kati ya watoto elfu 10 waliouawa. Tunasimama pamoja na watu wasio na hatia waliouawa kinyama huko kibbutzim tarehe 7 Oktoba. Kwa sababu sadaka ya kila maisha ni jeraha lisiloweza kuzibika. Rachel alielewa hili. Na sisi pamoja naye.

Taariri ya Dk Andrea Tornielli kuhusu makala ya Bi Polin
13 January 2024, 15:33